PostGE2025 Waziri Mkuu afanya ziara ya kushtukiza hospitali ya Mkoa Dodoma
Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
- ๐—”๐˜๐—ผ๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ฎ๐—ด๐—ถ๐˜‡๐—ผ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ช๐—ถ๐˜‡๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐—”๐—ณ๐˜†๐—ฎ, ๐— ๐—ฆ๐—— ๐—ป๐—ฎ ๐—ต๐—ผ๐˜€๐—ฝ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐˜‡๐—ผ๐˜๐—ฒ ๐—ป๐—ฐ๐—ต๐—ถ๐—ป๐—ถ
- ๐—ช๐—ฎ๐—ด๐—ผ๐—ป๐—ท๐˜„๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—ถ๐—ฝ๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ฒ๐˜‡๐—ฎ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ฏ๐—ผ๐—ฟ๐—ฒ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ต๐˜‚๐—ฑ๐˜‚๐—บ๐—ฎ ๐˜‡๐—ฎ ๐—ฎ๐—ณ๐˜†๐—ฎ

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 15, 2025 amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kuziagiza hospitali zote nchini zihakikishe wajawazito wanapofika hospitali wahudumiwe kwa haraka ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizaya ya Afya, Bohari ya Dawa (MSD) na Hospitali zote nchini ziweke vipaumbele vya kuwa na dawa kulingana na mahitaji ya eneo husika. โ€œ Haipendezi mwananchi kufika hospitali na kupatiwa vipimo vyote kisha anaambiwa dawa akanunue kwingine, kama duka binafsi linaweza kupata dawa hizo, inawezekanaje hospitali za serikali hapati? Naagiza Hospitali zote ziwe na dawa.โ€

Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wananchi nje ya hospitali hiyo baada ya kutembelea wananchi waliofika hospitalini hapo kupata huduma mbalimbali za kitabibu ambapo amesisitiza wananchi waendelee kuhudumiwa vizuri kwa kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini vikiwemo vifaa tiba na dawa.

Kadhalika Mheshimiwa Waziri Mkuu ameziagiza hospitali zote nchini zihakikishe zinakuwa na vifaa vya usafi binafsi vya dharura vikiwemo ndoo na beseni katika wodi za wazazi ili viwasaidie akinamama wasiokuwa na vifaa hivyo. โ€œUjauzito sio suala la dharura vifaa kama ndoo tunapaswa kuwa navyo katika hospitali zetu za serikali.โ€

Dkt. Mwigulu ametumia fursa hiyo kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika uboreshaji wa huduma za afya nchini. Waziri Mkuu akiwa hospitalini hapo, wananchi walimueleza kuwa wanahudumiwa vizuri na kwa uangalizi wa karibu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza hospitali zote nchini zizingatie maelekezo ya kutumia mifumo sahihi ya malipo katika taratibu za kutoa huduma ili kuwezesha Serikali kuendelea kuhudumia wananchi.

Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo kufuatia kuwepo kwa hospitali ambazo baadhi ya huduma wanapokea malipo kwa njia ya mtandao na nyingine malipo yanapokelewa malipo kwa njia zisizo rasmi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wagonjwa na wananchi wanaoguza ndugu zao wamempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora za afya.

โ€œTunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa tunapatiwa huduma nzuri kama tupo hospitali za private (binafsi).โ€ Kauli hiyo imetolewa na Dinna Enock, mkazi wa Makulu jijini Dodoma ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi.

IMG-20251115-WA0093(1).jpg
IMG-20251115-WA0098.jpg
IMG-20251115-WA0090.jpg
IMG-20251115-WA0091(1).jpg
IMG-20251115-WA0089(1).jpg
IMG-20251115-WA0096(1).jpg
IMG-20251115-WA0092(1).jpg
IMG-20251115-WA0094(1).jpg
IMG-20251115-WA0097(1).jpg
IMG-20251115-WA0095(1).jpg

-
 
Ha ha haa acha basi masikhara Tanganyika hatuna rais wala waziri

Labda akawe waziri mkuu wa BURUNDI!
 
huyo jamaa labda hajui tu lkn anaangushiwa zigo, d9 yeye ndiyo atakayesimamia serikali kuuwa watu na hivyo moja kwa moja kuwa responsible, sidhani kama wanaweza tu mpa power kirahisi kiihvyo ...
Acha kujitekenya na kujichekesha Mwenyewe kama zuzu
 
Safi sana kwa Mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba Mr Clean kwa kuanza kazi kwa kasi ili wananchi wapate huduma safi na stahiki. Tuna imani kubwa sana juu yake.
 
- ๐—”๐˜๐—ผ๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ฎ๐—ด๐—ถ๐˜‡๐—ผ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ช๐—ถ๐˜‡๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐—”๐—ณ๐˜†๐—ฎ, ๐— ๐—ฆ๐—— ๐—ป๐—ฎ ๐—ต๐—ผ๐˜€๐—ฝ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐˜‡๐—ผ๐˜๐—ฒ ๐—ป๐—ฐ๐—ต๐—ถ๐—ป๐—ถ
- ๐—ช๐—ฎ๐—ด๐—ผ๐—ป๐—ท๐˜„๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—ถ๐—ฝ๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ฒ๐˜‡๐—ฎ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ฏ๐—ผ๐—ฟ๐—ฒ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ต๐˜‚๐—ฑ๐˜‚๐—บ๐—ฎ ๐˜‡๐—ฎ ๐—ฎ๐—ณ๐˜†๐—ฎ

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 15, 2025 amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kuziagiza hospitali zote nchini zihakikishe wajawazito wanapofika hospitali wahudumiwe kwa haraka ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizaya ya Afya, Bohari ya Dawa (MSD) na Hospitali zote nchini ziweke vipaumbele vya kuwa na dawa kulingana na mahitaji ya eneo husika. โ€œ Haipendezi mwananchi kufika hospitali na kupatiwa vipimo vyote kisha anaambiwa dawa akanunue kwingine, kama duka binafsi linaweza kupata dawa hizo, inawezekanaje hospitali za serikali hapati? Naagiza Hospitali zote ziwe na dawa.โ€

Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wananchi nje ya hospitali hiyo baada ya kutembelea wananchi waliofika hospitalini hapo kupata huduma mbalimbali za kitabibu ambapo amesisitiza wananchi waendelee kuhudumiwa vizuri kwa kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini vikiwemo vifaa tiba na dawa.

Kadhalika Mheshimiwa Waziri Mkuu ameziagiza hospitali zote nchini zihakikishe zinakuwa na vifaa vya usafi binafsi vya dharura vikiwemo ndoo na beseni katika wodi za wazazi ili viwasaidie akinamama wasiokuwa na vifaa hivyo. โ€œUjauzito sio suala la dharura vifaa kama ndoo tunapaswa kuwa navyo katika hospitali zetu za serikali.โ€

Dkt. Mwigulu ametumia fursa hiyo kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika uboreshaji wa huduma za afya nchini. Waziri Mkuu akiwa hospitalini hapo, wananchi walimueleza kuwa wanahudumiwa vizuri na kwa uangalizi wa karibu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza hospitali zote nchini zizingatie maelekezo ya kutumia mifumo sahihi ya malipo katika taratibu za kutoa huduma ili kuwezesha Serikali kuendelea kuhudumia wananchi.

Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo kufuatia kuwepo kwa hospitali ambazo baadhi ya huduma wanapokea malipo kwa njia ya mtandao na nyingine malipo yanapokelewa malipo kwa njia zisizo rasmi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wagonjwa na wananchi wanaoguza ndugu zao wamempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora za afya.

โ€œTunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa tunapatiwa huduma nzuri kama tupo hospitali za private (binafsi).โ€ Kauli hiyo imetolewa na Dinna Enock, mkazi wa Makulu jijini Dodoma ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi.

View attachment 3502333View attachment 3502334View attachment 3502335View attachment 3502336View attachment 3502337View attachment 3502338View attachment 3502339View attachment 3502340View attachment 3502341View attachment 3502342
-
Atoe maelekezo, muda wa utekelezaji na ufuatiliaji na pia aongee na viongozi wa eneo husika ili ajue wajibu wa kila muhusika,,,zaidi ya hapo itakua ni siasa na kutoa shukran zisizokua na tija kwa wananchi .
 
Back
Top Bottom