Waziri Mkuu aagiza Mtwara kuchunguzwa kwa matokeo mabaya ya kidato cha pili

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameagiza uchunguzi ufanyike kufuatia matokeo mabaya ya kidato cha pili kwa mkoa wa Mtwara, Mkoa huo ulitoa shule 9 za mwisho kwenye matokeo ya kidato cha pili yaliyotoka wiki iliyopita

kinya18012017.jpg
 
Wachunguze nini wakati Serikali ndiyo chanzo na kuanguka kwa Elimu nchini? Watachunguza pia na ile iliyoshika nafasi ya pili ya tatu na ya nne n.k. toka mwisho? Au anataka Mtwara ichunguzwe kwa sababu ni kwao!? Acha ubinafsi Majaliwa nafasi yako ya Uwaziri Mkuu si kwa wana Mtwara pekee yao bali kwa Tanzania nzima. Elimu Tanzania nzima iko hoi bin taabani.
 
Sasa mkuu huyu aliewashusha vyeo hawa walimu waliopo unasemaje? na je hilo agizo la kushushwa vyeo bado lipo valid? na baada ya uchunguzi huo ukikamilika na ukakuta tatizo ni lingine tu kabisa huyu aliewashusha vyeo hawa walimu utamfanya nini?
utanijibu kwa vitendo mie nasubiri.na hapo ndo wananchi tunakupima tu.Faru john hatujasahau mind you.
 
Hivi huyu DCI ake na boyfriend wa Faru Hadija si alishawahi kuwa TAMISEMI huyu?! Ina maana hafahamu matatizo ya msingi ya pale alipokuwa juzi tu hapa?!
 
Watoe ajira waache ujinga wao. ...huo utafiti unapoteza pesa za walipa kodi bure tu
 
Shule nyingi hazina walimu wakutosha. Mitihani yenyewe machagilio mpaka hisabati. Kidato cha kwanza watoto hupelekwa baadhi hawajui hata kusoma. Kwa matokeo ya kidato cha Pili kuwa mazuri ni mipango, miundo na mifumo
 
Wachunguze nini wakati Serikali ndiyo chanzo na kuanguka kwa Elimu nchini? Watachunguza pia na ile iliyoshika nafasi ya pili ya tatu na ya nne n.k. toka mwisho? Au anataka Mtwara ichunguzwe kwa sababu ni kwao!? Acha ubinafsi Majaliwa nafasi yako ya Uwaziri Mkuu si kwa wana Mtwara pekee yao bali kwa Tanzania nzima. Elimu Tanzania nzima iko hoi bin taabani.

Huu ni ujumbe mzuri sana siyo kwake tu bali kwa viongozi wote

Acha ubinafsi Majaliwa nafasi yako ya Uwaziri Mkuu si kwa wana Mtwara pekee yao bali kwa Tanzania nzima. Elimu Tanzania nzima iko hoi bin taabani."
 
Mambo mengine ni yaajabu sana
Mtwara inajulikana ina mazingira magum ..walimu wachache huko

Sasa ijui kinachochinguzwa ni nini?
 
Huu ni ujumbe mzuri sana siyo kwake tu bali kwa viongozi wote

Acha ubinafsi Majaliwa nafasi yako ya Uwaziri Mkuu si kwa wana Mtwara pekee yao bali kwa Tanzania nzima. Elimu Tanzania nzima iko hoi bin taabani."
Inamhusu na mkubwa zaidi. Ubinafsi umetawala. Tanzania ni ya wote waache hizi sarakasi. Huyu bwana anasafiri kila siku yupo mkoa huu mkoa ule hao wakuu wa wilaya na mikoa waliwachagua wa nini? Mwalimu alionya swala la 'Kuuza sura' Fanyeni kazi bana tushachoshwa na matamko kila siku. Elimu muulize waziri wa Elimu uchunguzi wa nini wakati mchawi mnamjua.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Atutolee ujinga wake hapa yeye si alikuwa Naibu Tamisemi hajui matatizo ya elimu nchini? Cheap popularity.....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom