Waziri Mhagama: Serikali haitakaa ifute Mwenge wa Uhuru

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,061

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema Serikali haina mpango wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri Muhagama amelisema hilo Bungeni leo, Mjini Dodoma baada ya Mbunge mbunge wa Konde, Khatib Said Haji kuhoji,

Je? Bado kuna faida kwa watanzania kuendelea kukimbiza Mwenge wa Uhuru kila mwaka? Kama zipo ni faida gani? Kama hakuna faida,Je? Ni lini Mwenge huu utasitishwa?

“Faida za Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Kimataifa ni pamoja na kuhamasisha hali ya wananchi kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali katika taifa letu, pia ni chombo pekee cha kujenga mshikamano na kudumisha amani, pale ambapo Mwenge unapita na bila kujihusisha na itikadi za kisiasa, kuendelea kuhamasisha umuhimu wa Muungano kwa Watanzania wa nchi mbili wa nchi yetu, na kila mwaka kufungua kuweka maeneo ya msingi kama miradi mbalimbali ya wananchi, na kuhamasisha uzalendo na kuendelea kujitolea,” amesema Waziri Muhagama.

“Mwenge wa uhuru umeendelea kumulika hata nje ya mipaka yetu , umoja na mshikamao wa Watanzania ni matunda pia ya Mwenge wa Uhuru kwahiyo kutokana na mafanikio na faida zilizopatikana kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru Serikali inatambua kuwa zipo faida za kuendelea kukimbiza Mwenge huu wa uhuru, Hivyo basi Serikali haina mpango wowote wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwahiyo litakuwa ni endelevu na litaendelezwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine kwa kusisitiza misingi hii bila kuchoka.”
 
Jana nilikwenda kumsalimia rafiki yangu pale kijijini Lipokera (Jimbo la Peramiho). Basi nilifika kwenye kijiwe kimoja hivi na kuanza kumsifu Jenister Mhagama kwamba ni miongoni mwa mawaziri wachapa kazi. Cha kustaajabisha watu wote pale kijiweni waliondoka huku wengine wakishika pua kuashiria kwamba nilikuwa nimechafua hali ya hewa, na hivyo nikajikuta nimebaki na rafiki yangu John tu.
 
Wafute wa nini sasa??
Binafsi naona watafute njia bora ya kikimbiza mwenge wa uhuru mfano, kutumia ata gari tatu za wanajeshi zinatosha kuzunguka nchi nzima. Upite katika centre kubwa za wilaya basi.
 
Hivi kwa nini..tusipige kura ya maoni kuhusu Mwenge wa uhuru...yani wasio utaka mwenge watashinda kwa 90%
 
Ukijua kusoma na kuandika tu Mkuu huwezi kuona ujinga na ufujaji mkubwa wa pesa za walipa kodi mabilioni ya shilingi kukimbiza mwenge huku kukiwa na vipaumbele chungu nzima nchini ambavyo vingenufaika na hayo mabilioni ya pesa.
Mkuu upo very correct.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi kwa nini..tusipige kura ya maoni kuhusu Mwenge wa uhuru...yani wasio utaka mwenge watashinda kwa 90%
Umeshafuatilia kura zinavyopigwa bungeni?
Wanaoafiki....Ndiooo..
Wasioafiki......Ndioooooooooooooooio. Halafu unamsikia mkali Chenge akisema wanaoafiki wameshinda. Huwa nachoka. Labda hizo kura zipigiwe kwenye nyumba za Ibaada
 
Ukijua kusoma na kuandika tu Mkuu huwezi kuona ujinga na ufujaji mkubwa wa pesa za walipa kodi mabilioni ya shilingi kukimbiza mwenge huku kukiwa na vipaumbele chungu nzima nchini ambavyo vingenufaika na hayo mabilioni ya pesa.
Halafu wanakuja na agenda ya kupima ukimwi nyumba kwa nyumba wakati wao ndio wanabariki uenezaji wa ukimwi. Hii nchi imeoza haina mfano.,Mwenge ni kuhujumu na kudhulumu pesa za walipa kodi.
 
Kufuta wasiufute ila wasitulazishe kuuchangia , wauzungushe kwa fedha zao na si mishahara ya watu, kuna sehemu nasikia (Miheza) watu wanachangishwa mpaka pesa za kununua vitenge vya mwenge kwa amri, hilo si balaa sasa
 
"To be ignorant of what occured before you were born is to remain always a child. For what is the worth of human life, unless it is woven into the life of our ancestors by the records of history?" Ciero Orator
 
Jana nilikwenda kumsalimia rafiki yangu pale kijijini Lipokera (Jimbo la Peramiho). Basi nilifika kwenye kijiwe kimoja hivi na kuanza kumsifu Jenister Mhagama kwamba ni miongoni mwa mawaziri wachapa kazi. Cha kustaajabisha watu wote pale kijiweni waliondoka huku wengine wakishika pua kuashiria kwamba nilikuwa nimechafua hali ya hewa, na hivyo nikajikuta nimebaki na rafiki yangu John tu.
B

Bavicha msipoacha bangi mtaishia pabaya sana sijui kawaroga nani.
 
Nchi yetu haitakuwa na maendeleo kama hawa mafisadi wataendelea kung'ang'ania madarakani. Hawa wahuni ni kikwazo kikubwa sana cha Tanzania yetu kusonga mbele.

Halafu wanakuja na agenda ya kupima ukimwi nyumba kwa nyumba wakati wao ndio wanabariki uenezaji wa ukimwi. Hii nchi imeoza haina mfano.,Mwenge ni kuhujumu na kudhulumu pesa za walipa kodi.
 
Back
Top Bottom