Waziri Mhagama ataweka siasa pembeni Wizara ya Utumishi kweli?

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Huyu mama nilivyokuwa ninamwona ni kama Mwanasiasa sana sana. Ukiangalia level ya elimu yake kwenye web ya Bunge unaelewa kuwa huyu ni Mwanasiasa na ndiyo maana aliwekwa kuongoza Ofisi ambayo ina potifolio nyingi za kisiasa.

Mfano alipokuwa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) mambo yote hayo yalikuwa yanasimamiwa kisiasa Zaidi angaia mambo ya Sera ni siasa, Bunge ni siasa tu, Uratibu wa shughuli za Serikali ni siasa tupu, ya taarifa za mambo ya kazi na kiajira ni siasa haswa.

Angalia issue ya vijana - yote hiyo ni siasa hutumika kuwahadaa vijana hawa na CCM haitaki kabisa hata ile Sheria ya Baraza la Vijana ifanye kazi. Ukienda kwenye issue ya walemavu - ni suala sensitive ambalo linapaswa siasa sana ndani yake.

Angalia issue ya kikokotoo nalo limekuwa likibebwa kisiasa na huyu Mama ndiyo alikuwa akilisimamia kwa umakini wa hali ya juu kwa kutumia mbinu za kisiasa ili lisije ivuruga CCM na utawala wake.

Sasa amepelekwa Utumishi na Utawala Bora - kwa maana mambo yote ya kiutumishi na utawala ikiwepo Usalama wa Taifa yanakuwa yanaratibiwa na yeye.

Kule alikuwa akishughulika pia na mambo ya Tume ya Uchaguzi na Msajili wa Vyama vya Siasa - huko kote utaalamu ni kama uliachwa pembeni.

Je, mama SSH anataka pia mambo ya kiutumishi na Usalama wa Taifa yaendeshwe kisiasa zaidi? Mama Mhagama ndiyo chanzo cha Utendaji mbaya wa Tume ya Uchaguzi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa kwa sababu yeye maisa yake yote ya utendaji wake hutanguliza siasa mbele. Sasa kama Utumishi wa Umma nao unaenda kuendeshwa kisiasa tutarajie nini mbele?

Kwangu mimi ninaona SSH hakuwa makini kwa kiasi chake kumpeleka huyu mama pale! Hakika! Bora Pindi Chana au Ndalichako wangekuwa pale huyu angebaki kudeal na Sera, Bunge na Uratibu au Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu aendeleze ndoa yake na Mifuko ya Pensheni pia!
 
Umekosea tu mwishoni uliposema Ndalichako angefaa aletwe utumishi. Mimi binafsi sijawahi kumkubali kbs huyo Ndalichako mama gani wambuzi muda wote kauzu namna ile unataka atuharibie ndondo makazini
 
Umekosea tu mwishoni uliposema ndalichako angefaa aletwe utumishi....Mimi binafsi sijawahi kumkubali kbs huyo ndalichako mama gani wambuzi muda wote kauzu namna ile unataka atuharibie ndondo makazini
So kati yake na Mhagama kwa kuwa Utumishi unaona Mhagama ni zaidi? Mie nilitumia neon afadhali angekuwa ila sio kuwa ninamaanisha naye ni mzuri huko
 
Hao wote uliowataja hawafai. Ndalichako ni mtu wa Kigoma, hawa wana roho mbaya na chuki nyingi. Pale wangemwacha Mchengerwa ndo maana wafanyakazi wamaekata tamaa na wamelalamika sana kupelekwa Jenista pale.

Mchengerwa alikuwa mtu mchapakazi, mwenye huruma na alikuwa na uchungu na wafanyakazi sana na pia alikuwa mfuatiliaji. Mama kaharibu sana kumpeleka Jenista pale na ataiharibu sana hiyo Wizara.

Familia ya Jenista wote ni wanasiasa kasoro baba yake tu ambaye si mwanasiasa tena yeye ni mcha Mungu sana na muda wake mwingi yuko kwenye mauwala ya dini lkn upande wa mama wote ni wanasiasa na hawako smart. Hivyo watumishi wasipoendelea kupaza sauti wameumia.

Yeye na Devota Likokola wote wana vinasaba vinavyofanana. How possible kama hata nyumba zao zilikuwa na shida leo hii anamweka kwenye wizara nyeti kama hiyo?
 
Bora Pindi Chana au Ndalichako wangekuwa pale huyu angebaki kudeal na Sera, Bunge na Uratibu au Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu aendeleze ndoa yake na Mifuko ya Pensheni pia!
Kama mambo ndivyo yalivyo bora ameondoka sehemu hii ya pensheni maana anaua wastaafu kabla ya umri wao wa kufa
 
Huyu mama nilivyokuwa ninamwona ni kama Mwanasiasa sana sana. Ukiangalia level ya elimu yake kwenye web ya Bunge unaelewa kuwa huyu ni Mwanasiasa na ndiyo maana aliwekwa kuongoza Ofisi ambayo ina potifolio nyingi za kisiasa...
 
Huyu mama nilivyokuwa ninamwona ni kama Mwanasiasa sana sana. Ukiangalia level ya elimu yake kwenye web ya Bunge unaelewa kuwa huyu ni Mwanasiasa na ndiyo maana aliwekwa kuongoza Ofisi ambayo ina potifolio nyingi za kisiasa...
Ndalichako? DrJoseph Musukuma ni bora
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom