Waziri Membe jiandae kukanusha

jamaa ana confidence kweli kwenye kukanusha mambo
 
Hivi Membe bado hajaoteshwa urais? Maana siku zinaendelea kuyoyoma. Kama bado namshauri aanze kulala bungeni kama mzee wa Gombe ndoto ya urais itakuja humo humo?
 

Hapa nitahitaji kuelimishwa zaidi.....mara nyingi (kulingana nahabari za kivita nilizowahi kuzipitia)waandishi (wanokuwa kwenye uwanja wa mapambano) huwa wanaambatana na vikosi vya majeshi husika kwenye mapigano hayo. Ama wanakuwa upande huu ama upande ule (wanakuwa wanalindwa na upande husika). Mfano kwa mtafaruku wa Ukreine ...utakuta majeshi ya serikali iliyowekwa na US+EU inakuwa na waandishi ama wa BBC,et.al wakati wale wa ukreine ya mashariki wanakuwa na waandishi wa RT, et.al.

Sasa naomba kukuuliza, hao waandishi hao wa kimataifa wanaotengeneza Documentary wako upande wa Wafugaji ama upande wa Wakulima?
.

Hili Mh. Membe hatahusika kukanusha ni waziri wa mambo ya ndani anatakiwa kulisemea.
 
Membe aka Waziri wa Mambo ya Nje na Makanusho
 
Yaani ni aibu sana,waandishi wetu wazalendo wamelala usingizi wakisubiri bahasha za khaki.Hivyo bado tupo mbali sana na hawa wazee wa bahasha.

waandishi wetu wapo bize na kambi za urais ndugu
 

Mkuu kwa uelewa wangu ni kuwa kule Karatu na kwingineko kwenye tafrani hizi ni mapigano na sio vita. Kule hakuna itikadi au sera ambayo kundi moja na lingine yanakinzana bali ni kuona kila mmoja anaonewa ndio maana huwezi kusikia anadhurika mtu asiye husiana na kilimo au ufugaji.
Hizi documentary sio za kuzibeza hasa zinazoandaliwa na waandishi huru kutoka nje kwani zimetufumbua macho kwenye mambo mengi. Kumbuka ile ya Mapanki, Mauaji ya Albino, pembe za ndovu nk.
 
hyu mmakonde kazi kulambalamba ulimi kama chatu ndio maana joka la ndimu
 
Nilidhani umeandika namna gani ya kumaliza mgogoro wa kiteto kumbe unaandika kusifia wandishi wa kimataifa nenda na wewe wakakuhoji.

Matatizo yakizidi ni lazima kiongozi augue busha.
 
hivi hyu Membe elimu yake ikoje,nasikia kichwani ni empty kabisa
 
Katika mawaziri vilaza Membe ni mmoja wapo! Nilisikia alipokua akisema kuhusu wivu wa mataifa ya nje kuhusu uwekezaji na blah blah baada ya kashfa ya meno ya tembo ya wachina!!

Nikashangaa eti huyu nae anagombea urais! Lakin katika nchi yenye vilaza asilimia kubwa kama yetu lolote linawezekana!
 

walijuaje kama mauaji yatatokea kiteto hadi waanza kuandaa hiyo documentary!? any way waambie wakamilishe ya boko haram kule naija, wakimaliza watengeneze ya kule libya, then waende somalia, kenya then waje Tz watakua nazo za kutosha kwa ajili ya tv zao pambaf zao!
 

Kwahiyo unafurahia Tanzania ikisemwa vibaya na wasioitakia mema?
 
Kwahiyo unafurahia Tanzania ikisemwa vibaya na wasioitakia mema?

kuna mtu asiye itakia mema tanzania zaidi ya CCM???au mema gani unaongelea hapa? Wizi wa meno ya tembo,escrow,epa,madawa ya kulevya ,au nini? Labda ufunguke kidogo.
 
Kwahiyo unafurahia Tanzania ikisemwa vibaya na wasioitakia mema?

kuna mtu asiye itakia mema tanzania zaidi ya CCM???au mema gani unaongelea hapa? Wizi wa meno ya tembo,escrow,epa,madawa ya kulevya ,au nini? Labda ufunguke kidogo hata kama hukujaaliwa akili timamu.
 
Kuna rafiki yangu askari yupo kule kila siku ananipa taarifa za vifo, cha kushangaza viongozi wako kimya tu utafikiri kule siyo Tanganyika.
 
Kwahiyo unafurahia Tanzania ikisemwa vibaya na wasioitakia mema?
kwa inshu kama hiyo ya kiteto wangekuwa wana nia nzuri hawa viongozi wa Tanganyika wangeshachukua hatua...wanaofichua ndo wanaitakia mema wanataka tujirekebishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…