barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,865
Waziri Makame Mbarawa amekutana na vyombo vya habari ktk jengo la VIP Terminal II na kuelekezea kadhia ya jengo la abiria kuungua(Terminal Bulding II)(
Jengo hilo la abiria lilianza kuungua usiku wa tarehe 12 January 2017 majira ya saa tano usiku.Mpaka sasa chanzo cha moto kinatajwa kuwa ni itilafu ya umeme(japo uchuguzi bado unaendelea) katika moja ya vyumba TB II eneo la kuwasili abiria toka nje ya nchi.
Vyumba vilivyoathirika ni kile cha "Lost and Found" ambacho hutumika kuweka mizigo ya abiria iliyopotea na kupatikana au ile mizigo iliyosahauliwa na wateja na wakati mwingine mizigo ile iliyopoteza "connection".(Huduma ya "Lost and Found hutolewa na kampuni ya Swissport,ambayo imekuwa ikilakamikiwa kwa uwizi na upotevu wa mizigo ya abiria,mimi ni muhanga wa uwizi huu)
Chumba kingine kilichoathirika ni kile cha "CUSTOMS AND EXCISE".Hapa ndipo hutunzwa mizigo na vifurushi.Ni eneo ambapo mizigo toka nje ya nchi iliyoshindwa kulipiwa ushuru au kusubilia taratibu za kulipiwa ushuru(kodi) huifadhiwa.Chumba hiki kipo chini ya Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi Tanzania(TRA)
Moto huo umeteketeza eneo la paa na kufanya shughuli zote za uwanja kusimama na kuhamia uwanja wa zamani wa Terminal One.Eneo la Terminal Two umeme ulizimwa na hivyo mambo yote kuhamia uwanja mdogo ambao kawaida hutumika kwa VIP na ndege ndogo za kukosi kwenda mbugani,Zanzibar na maeneo mbalimbali.
Pongezi kwa Kikosi cha Jeshi la Zimamoto Viwanja vya ndege,ambao walifika mapema na kwa wakati na kuweza kuuthibiti moto huo.
Mpaka kufikia mchana,baadhi ya shughuli za usafiri kama uegeshaji wa ndege,check in counters na nyinginezo ziliendelea salama ktk eneo la TBII,huku jengo likiwa na sehemu na sehemu zisizokuwa na umeme hivyo kuleta joto kali.
Taarifa kamili itatolewa juu ya chanzo na madhara yaliyopatikana baada ya sehemu hizo kuungua.
Note:Kwa uhalisia tu,jengo hilo limechakaa sana,lina miaka zaidi ya 30 na ukarabati wake ni wa kuungaunga.Ukiangalia wiring yake,mfumo wa maji taka na maji safi,ni dhahiri kuwa jengo hili ni chakavu na lolote linaweza kutokea wakati wowote.Bila shaka kwa "alarm" hii ya moto,serikali italizama upya jengo hili na kuliwekea mikakati.Linatia aibuuuu....Ipo siku abiria watamwagikiwa na maji ya kinyesi kwa ubovu wa mfumo wa maji taka.