digalangosha
JF-Expert Member
- Aug 30, 2013
- 1,554
- 2,265
Mimi ni miongoni mwa wananchi tunaoishi Dodoma maeneo ya MSALATO utakapojengwa uwanja mpya wa ndege.
Katika maeneo yetu walikuja watu wa Tanesco na kuweka alama baadhi ya maeneo kwa kigezo kuwa wanataka kupitisha njia ya umeme mkubwa hapo. Leo imepita miaka zaidi ya mitatu (3) Tanesco Dodoma wanasema tusiendeleze maeneo yetu lakini tukiwauliza mbona hawaji kuthaminisha maeneo yenyewe, wanatujibu kuwa bado wapo kwenye mchakato kwa miaka mitatu na ushee.
Mh. Najua hii ishu utakua bado hujaambiwa lakini ipo na wananchi wa huku wanataka waje kuandamana. Sasa ya nini kadhia yote hii wakati ni kitu chakuongea tu kama watachukua maeneo tukubaliane au kama wamehairisha waseme pia watu tupimiwe viwanja tuanze kujenga.
Uongozi wa eneo husika hauoneshi jitihada yeyote zaidi ya kuwa madalali wa kuuza viwanja vya watu...
Naomba kuwasilisha