Waziri Makamba unachokifanya kwenye Bwawa la Nyerere, hii dhambi itakutafuna milele

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Hivi mnafanya hivi kumkomoa mwendazake au kunufaisha mabeberu?

Mimi sikuwahi kumpenda mwendazake hadi leo na sitokuja kumpenda ila kwenye suala la madini, SGR na Bwawa la Nyerere nilimuunga mkono maana huo ni utaifa na ni suala la utaifa.

Ila kwakweli kwenye Bwawa la Nyerere mnayoyafanya yanasikitisha sana na yanaumiza moyo?Kuna wakati najiuliza mnafanya kwa faida za nani? Hivi mnamkomoa mwendazake au?

Kwasababu, Mmmnh! Watanzania wenzangu hebu nisaidieni kuelewa kitu hapa!! Mwaka 2021 ilifikikia 37% sasa tupo 2022 74%. Then tunaambiwa mpaka 2024 ndiyo likamilike! Sasa hii iko vp ndugu wadau? Kimahesabu imebaki 26% kama nipo sahihi? Swali moja kubwa na kidogo linashangaza kwanini ndani ya mwaka mmoja kazi ifanyike kwa 37% na 26% iliyobakia igarimu muda wa miaka miwili?()

Ukweli ni kuwa mwenye bwawa angekuwepo saivi lishawashwa ila Hawa wajanja wanaamua watupige kimya kimya tu!

Nahisi hakuna mradi mkubwa aliouacha mzee ambao umekamilika mpaka Sasa!

Hii Tanzania bado tunahitaji Rais ambaye ni katili zaidi ya Putin ndo mambo yataenda au? Huyu makamba sio mtu nzuri kabisa, narudia huyu jamaa nahisi naye sijui km ana uzalendo hata kidogo huyu jamaa nitakua wa mwisho kumuamini huyu jamaa

Najua Wanataka mradi wa Magufuli wautumie kwenye kampeni za Uchaguzi, wananchi watawakataa, wanajua hamjajenga ninyi, ni magufuli kajenga, Kama mngefahamu ni kheri Kama mngekamilisha kwa Wakati ili wananchi wauone mradi ukifanya kazi kwa wakati mwafaka na wapate huduma kwa Uharaka ikiwemo Usafiri wa Reli (SGR).

Mimi sikuwahi kumpenda magufuli, na.sitokuja kumpenda ila hili suala la SGR, Nyerere dam, na madini nilisimama nae bega kwa bega maana hayo ni maslahi ya taifa lakini kwa hili ni kama mnapambana na huyo mzee wa watu mnapambana ili tu muharibu yale mema yake machache mliyoyaacha.

Hakika Makamba kwa hili la bwawa nitazidi kukuchukia sana roho inaniuma sana imebid nipaki gari pembeni nasikia uchungu sana hadi natetemeka kwa hasira maana nina taarifa kwamba hata haya matatizo ya umeme unapata mgawo, ishu ya taifa gas/mihan unapata huko.

Kinachotia hasira unaichelewesha na kuuharibu huu mradi wa kitaifa wa Nyerere kwa maslah yako binafsi na chuki zako binafsi juu ya kilichofanyika lakini ipo siku yako inshallah mungu anawaona mjuwe mnachokifanya ni kibaya sana

Mnisamehe wakuu ila nina hasira sana.

1666376319685.jpg
 
Unarudia rudia kusema hukuwa ukimpenda Magufuli, hivi wabongo nani katuambia kuwa unatakiwa umpende au umchukie kiongozi? Ndio maana tunashindwa kuwakosoa baadhi ya viongozi kwa sababu ya kuwapenda na kuona kuwakosoa ni tafsiri ya kuwachukia na tunashindwa kupongeza kwa kuhofia kuonekana unampenda huyo kiongozi.

Ni ujinga mtupu.
 
Amewapa baadhi ya makampuni ya majenereta muda wa kujipanga.

Kuna makampuni mengi sana yapo na yanalipa kodi vizuri na 10% za kutosha kwa vigogo.

Kila benki au jengo kubwa lolote lina jenereta la APM, PIVOTECH au MANTRAC so kuwaharibia biashara zao utasababisha hasara ya kutosha.

Inabidi uwepo muda wa kujipanga na njia nyingine ya kufidia biashara zao.
Kila Bank au jengo kubwa Lina generator kubwa. Hizi zilizo Kwisha kufungwa hadi kwenye Ma hospital Bado anachukua 10%?

Kote zilipo Generator ,Makamba amehusila kwenye manunuzi?
 
Kwenye hili la bwawa kulikuwa na bado kuna mihemko ya kujichanganya kuhusu muda halisi na kasi ya ujenzi.
Huko siku za nyuma, ukiwa site, kama una akili ya kawaida, Ukisikia maelezo ya wanasiasa, unashangaa kwa sababu kwa hali halisi isingewezekana.
Kwa bahati mbaya sana, siasa zetu ni za kufuata mkumbo kama nyumbu, wataalamu wakiwa kundini.
Ni muhimu taarifa zitolewe na wataalamu ili wanasiasa wapate ukweli na pia wasiwajibike kwa udanganyifu bila sababu za msingi.
 
Najua Wanataka mradi wa Magufuli wautumie kwenye kampeni za Uchaguzi, wananchi watawakataa, wanajua hamjajenga ninyi, ni magufuli kajenga, Kama mngefahamu ni kheri Kama mngekamilisha kwa Wakati ili wananchi wauone mradi ukifanya kazi kwa wakati mwafaka na wapate huduma kwa Uharaka ikiwemo Usafiri wa Reli (SGR).
Nani aliyekwambia wanashinda uchaguzi kwa Sanduku la Kura?
 
Back
Top Bottom