Waziri Maiga shughulikia haraka: Ubalozi wa Ujerumani nchini kubandika ukutani Ramani ya Tanzania inayoonyesha Ziwa Nyasa liko Malawi.

Daimler

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
556
973




Ubalozi wa Ujerumani nchini, umebandika ukutani, Ramani ya Tanzania inayoonyesha Ziwa Nyasa likiwa ndani ya Mipaka ya Malawi badala ya Mpaka wa Tanzania na Malawi kuwa katikati ya Ziwa.
Ujerumani ndiyo Mtawala wa kwanza wa Tanzania, kipindi hicho ikiitwa German East Africa (DOAG), kupitia Mkataba wa 1886 (Anglo-German Agreement) ulioweka Mipaka ya ukanda wa Pwani na Kenya, kabla ya Mkataba wa 1890 (Helgoland Treaty) kumalizia kuweka mipaka ya Uganda, DRC, Zambia (Rhodesia), Malawi (Nyasaland) na Msumbiji (Mozambique). Heligoland Treaty ndiyo ililiweka Ziwa Nyasa kwa Wamalawi.
Hata hivyo, baada ya Waingereza kuiweka Tanganyika Territory chini ya Mandate, alijikuta akitawala Malawi na Tanganyika na hapo ndipo walipobadili Mpaka na kuuweka katikati ya Ziwa Nyasa.


Anyway, siko hapa kurefusha mada hii, muhimu ni lazima marafiki wa Tanzania, i.e. wote wenye Ubalozi hapa Tanzania, wahakikishe Ramani zinazoonekana kwenye Ofisi zao ni zile zinazotolewa ama kukubaliwa na Tanzania na si mwingine yeyote.
So, Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine Mahiga shughulikia haraka suala hilo.

https://cdn.auckland.ac.nz/assets/humanrights/Research/MalawiTanzania-NZCHRLPP-final.pdf


Ramani ya Tanzania.
 
kama wajeruman waliweka mipaka na kuonyesha ziwa liko Malawi na waingereza nao wa
kaonyesha ziwa liko upande wa Tanganyika Basi wenye maamuzi ya kuamua ziwa LA nani ni wajerumani au waingereza, wakae waamue nani mumiliki halali wa ziwa Nyasa/Malawi.
 
Majungu mengine ya kimaku mnamchukia possible hapo mnaanza kuleta fitna mbona makubwa kama ya jiwe anavovunja katiba na kunyayasa watu hamusemi shut hole
Wewe si Mtanzania naona unawashwawashwa. Oohh no, hapo ndo kipimo cha elimu yako. Unalinganisha demokrasia (mambo ya ndani) na national interest? Elimu yako ni duni sana kulinganisha hivi vitu viwili. Halafu itokee Malawi atuvamie utaenda kupigana kweli? Mtataka Tanzania ishindwe kwa kuwa kuna mtawala hamumtaki? You're a failure.
 
Mnapobagua jambo lipi liongelewe lipi liachwe huwa nashindwa kuwaelewa Lumumba heroes.
 
Ccm na mambo mengine mngekuwa mnachunguza hivi watu wasiojulikana wangekuwa washakamatwa.Yaani umezoom ,umetafuta reference weee.asante.Na mambo ya muhimu kwa mustakabali wa nchi muwe mnazoom hivohivo mnachunguza out of the box
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…