Waziri Maghembe, wazalendo wa mitandaoni wasikuzidi maarifa

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Waziri mwenye dhamana ya utalii Profesa Jumanne Maghembe, umepewa wizara nyeti sana, yenye changamoto nyingi kwa uchumi wa nchi hii. Majirani zetu Kenya, kwa umahiri mkubwa wameweza kuitumia wizara kama ya kwako, katika kuvutia watalii wengi.

Kenya walishawahi kuweka Tangazo la utalii kwenye channel ya supersports. Mtu anaangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza, halafu wakati wa mapumziko anamsikiliza kiongozi mmoja wa serikali ya Kenya anayevielezea kwa ufasaha mkubwa vivutio vyote vya Kenya.

Naamini waziri Maghembe kwa usomi ulionao, unao uwezo wa kuvielezea vivutio vyote tulivyonavyo, kupitia tangazo moja lenye kuutangaza utalii wetu.

Gharama za tangazo haziwezi kuwa ghali sana kiasi cha serikali kukosa kabisa fedha kwenye channel kama ile ya supersports. Wizara ya utalii ina kila sababu ya kupeleka pendekezo wizara ya fedha na ikiwezekana hata ikulu kwenyewe, ili fedha ya kuutangaza utalii wa nchi iweze kutengwa.

Wakati makusanyo ya kodi yakitegemewa kuongezeka kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, nadhani huu ni wakati muafaka kwa waziri Maghembe kuingia kazini wewe mwenyewe, katika kuitangaza Tanzania na vivutio vingi tulivyojaliwa na Mungu. Kenya waliweza kwanini sisi tushindwe?.

Waziri Maghembe usikubali vijana wa kitanzania wenye maarifa ya matumizi wa mitandao wakakuzidi uwezo wa kuitangaza Tanzania na vivutio vyake. Tafadhali ingia kazini ili ulinde heshima ya nchi hii.
 
Back
Top Bottom