Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Miaka kadhaa iliyopita, serikali ya Kenya iliutangaza utalii kitaalam sana. Waliingia gharama ya kurusha tangazo la dakika chache lenye kuutangaza utalii wao kupitia channel maarufu ya supersports. Fedha waliyoitumia katika matangazo iliweza kurudi na faida juu kwa sababu ya ongezeko kubwa la watalii.
Serikali ya awamu ya nne iliweza kufanya jambo kama lililofanywa na Kenya, baada ya kuweza kuitangaza Tanzania kupitia bango la matangazo la uwanja wa timu ya Sunderland inayocheza ligi kuu ya Uingereza. Wakati mechi ikiendelea, tangazo la umeme kuhusu Tanzania lilionekana pembeni ya uwanja. Lakini naamini kwamba ikiwa Waziri Profesa Jumanne Maghembe na wasaidizi wake kwa pamoja wanaweza kujipanga na kuandaa tangazo la utalii kupitia channel ya supersports au nyingine ya kiwango hicho, na yeye mwenyewe waziri akaingia kazini kwa kuitangaza Tanzania. Hizi fedha zinazopatikana kupitia ongezeko la kodi, zitumike katika kuutangaza utalii wa nchi yetu kimataifa.
Ukiitazama Kenya ukiwa kwenye ndege wakati unatoka Afrika ya Kaskazini, sehemu kubwa ya kaskazini ya nchi hiyo ni kame, yaani kavu kabisa, hauna mvuto "haipigiki picha". Lakini sehemu kubwa ya Tanzania ukiitazama kutokea angani "inapigika picha", yaani inavutia. Waziri Maghembe aingie kazini kiubunifu, aitangaze nchi hii. Haipendezi kuona Kenya wenye sehemu ndogo yenye rutuba na ubora kulinganisha na sisi, wanaweza kuivutia dunia, halafu sisi tunabakia kusikika tukilalamikia mauaji ya Tembo na Nyati. Tupambane na maharamia wa wanyama, lakini kuna upande wa fursa za kitalii, huu tusikubali ukatupita.
Waziri Jumanne Maghembe ingia kazini sasa honeymoon imekwisha, nchi inakudai ubunifu, inakudai utendaji wa kazi wenye tija na tofauti kulinganisha na wote waliokutangulia katika hiyo ofisi.