Waziri Maghembe Awasimamisha Kazi Watumishi Watano wa Hifadhi ya Ngorongoro, 15 Wahamishiwa Wizara

iCode

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
760
440
Leo Mh Waziri wa Maliasili na Utalii amefanya ziara ya kushtukiza katika makao makuu ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na kusimamisha kazi wafanyakazi wengi na wengine wanahamishiwa wizarani kwa majukumu Mengine,

Suala la kutumbua majipu hapa NCAA linatarajiwa kuwa endelevu kwani kwa muda mrefu sasa Shirika hili la Umma limefanywa Shamba la bibi..

Ikumbukwe Kwamba Mwaka wafanyakazi wa idara mbalimbali walifukuzwa kabisa, akiwepo Veronica Ufunguo, Justice Muumba, Mallya na wengine wengi.

Kwa kiasi cha majipu yaliyotumbuliwa sasa Ngorongoro itaanza kujirudi kuwa Shirika lenye heshima yake.

1.jpg


Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Profesa Jumanne Maghembe amewasimamisha kazi watumishi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuwahamisha wengine 15 kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha na ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa Umma.

Mh.waziri Maghembe amechukua hatua hiyo baada ya kutembelea na kukutana na wafanyakazi wa mamlaka hiyo na amesema hatua zingine zitafuata kwa watumishi hao ambao wote watano ni wa idara ya uhasibu.

Kuhusu watumishi wanaohamishwa ambao ni wa idara mbalimbali ikiwemo uhandisi,utalii na ikolojia Mh.Prof.Maghembe amesema hatua hiyo inalenga kutoa nafasi ya kuendelea kufanyika kwa uchunguzi zaidi juu ya tuhuma mbali mbali zinazowakabili.

Mhifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro Bw.Fredy Manongi pamoja na kukiri kuwa mamlaka inakabiliwa na changamoto mbalimbali amesema kwa sasa tatizo kubwa ni ujangili unaofanyika katika maeneo ya mipakani japo amesema wanaendelea kuzikabili.

Hii ni ziara ya kwanza ya Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe katika mamlaka hiyo ambayo amesema ni mwendelezo wa utekelezaji wa azma ya serikali ya kuimarisha uwajibikaji,ukusanyaji wa mapato na kuimarisha shughuli za uhifadhi.
 
Maghembe huyu huyu Waziri Mzigo anapata wapi Ujasiri wa Kutumbua??


Hata Wananchi tunashangaa kuwa Magufuli ilikuwaje akamchagua huyu mtu.
 
Ila hizi Habari hata mie nimezichoka Sasa, coz mijipu ipo tele lakini haijaguswa, but vijipu upele ndo vinatumbuliwa tena kwa ulazima
 
Kwa kweli vilio vimetawala hapa Ngorongoro, wengi wameskip Lunch na wamerudi majumbani na majonzi mazito.
 
Kwa kweli vilio vimetawala hapa Ngorongoro, wengi wameskip Lunch na wamerudi majumbani na majonzi mazito.
Ungetutajia kabisa na majipu yaliyotumbuliwa...NCAA watu wanapiga tu pesa na kazi hawafanyi..
 
Back
Top Bottom