Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,770
- 1,173
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameshiriki hafla ya maadhimisho ya Miaka 108 ya Jamhuri ya Finland, iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 05 Desemba, 2025.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Kombo ameipongeza Finland kwa mafanikio makubwa iliyofikia katika kuleta maendeleo ya wananchi wake, kudumisha amani na umoja wa kitaifa.
Aidha, Mhe. Kombo alieleza msimamo wa Tanzania kuhusu masuala ya ulinzi wa amani na usalama wa wananchi wake na mali zao, kwa nyakati zote kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Balozi wa Finland nchini Mhe. Theresa Zitting aliishukuru Tanzania kwa ushirikiano na urafiki wake, akisisitiza kuwa Tanzania ni nchi nzuri, yenye watu wazuri na rasilimali nyingi, zinazopelekea haja ya mataifa haya mawili kuangalia fursa zaidi za ushirikiano wa kidiplomasia.