Waziri Kigwangala ikuingie kichwani kwako, Wanyama, Mbuga hazileti Watalii!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Mkitaka Watalii wafurike Tanzania wekezeni kwenye Fukwe, matamasha kama vile Sauti za Busara Unguja na vitu kama hivyo hizo Mbuga ni kiduchu sana, watu wa first World wanapiga kazi mwaka mzima kisha anataka kukwea pipa kwenda kuondoa stress ufukweni kuogelea, kurelax na totos na kufurahia maisha, hakuna kijana wa Kizungu au Japani anataka kuja kuona Simba au sijui Twiga Ngorongoro.

Hivyo mkitaka Watalii wa kufa mtu achaneni na ujinga wa Serengeti sijui Katavi kamateni fukwe kuanzia za Bahari hadi Maziwa makuu tengenezeni Matamasha kajifunzeni Zanzibar, BTW > 60% ya Watalii wanaokuja TZ wanakwenda Zanzibar na siyo Katavi, au Ngorongoro, ...

Mkuu ni aina ya utalii tu. Ukistaajabu ya serengeti, utayashangaa ya watalii kibao wanaoenda kushuhudia nyani wa Rwanda

Kingine beach tourism ipo worldwide tofauti na utalii wetu thou siwezi kupinga bado hatujautumia ipasavyo
 
Unaweza nipa idadi ya Watalii wanaokwenda Rwanda kushangaa Sokwe? P.Kagame ni mtu wa propaganda sana, hivyo usimwamini sana, lkn kama una namba ya Watalii wanaofurika Rwanda ingesaidia isitoshe hata Kenya kwa mfano Watalii wengi wanakwenda shauri ya Mombasa, Malindi na Lamu na siyo Mbuga.
 
Mkitaka Watalii wafurike Tanzania wekezeni kwenye Fukwe, matamasha kama vile Sauti za Busara Unguja na vitu kama hivyo hizo Mbuga ni kiduchu sana, watu wa first World wanapiga kazi mwaka mzima kisha anataka kukwea pipa kwenda kuondoa stress ufukweni kuogelea, kurelax na totos na kufurahia maisha, hakuna kijana wa Kizungu au Japani anataka kuja kuona Simba au sijui Twiga Ngorongoro.

Hivyo mkitaka Watalii wa kufa mtu achaneni na ujinga wa Serengeti sijui Katavi kamateni fukwe kuanzia za Bahari hadi Maziwa makuu tengenezeni Matamasha kajifunzeni Zanzibar, BTW 60% ya Watalii wanaokuja TZ wanakwenda Zanzibar na siyo Katavi, au Ngorongoro, ...
Naomba nikupinge mkuu.

Hata hizo fukwe huwezi kushindana na maldives, indonesia, brazil, spain, hawaii etc kuna fukwe nzuri balaa, same kwa hayo matamasha yapo mengi kupita maelezo mazuri mara 100 kushinda ya znz.

Kinachotakiwa ni kutafuta vitu vya kipekee, vitu ambavyo havipatikani kokote duniani ila hapa kwetu tu.

Mfano Angalia thanda island, ipo Tanzania ila ni private island kubook tu kukaa hapo unatakiwa ufanye deposit ya dola $70,000 ambayo ni kama milioni 150, ni kisiwa cha kipekee miundo mbinu ya helicopter, wanyama kama tasa na vitu vyengine ambayo hupati kwengine.
Thanda-Island-Aerial-01.jpg

Hii ni hulka yetu binadamu kinapotokea kitu ambacho hakipatikani kokote duniani basi tunamiminika ili na sisi tuonekano tumeshiriki.

Boresheni na tangazeni hivi vitu watu watakuja.
 
Chief-Mkwawa,

Unaweza mbona Zanzibar wanajaa? Kuna ndege zinakuja hazitui popote hadi Zanzibar, isitoshe Mji kama Bagamoyo tungeweza ugeuza ukawa wa Matamasha tu mfano tamasha la sanaa lilikuwepo lkn lilikuwa linafadhiliwa na Muzungu na lilibamba kiasi chake, BTW ushawahi kutembelea Sauti za Busara Zanzibar 13-16/02?
 
Unaweza nipa idadi ya Watalii wanaokwenda Rwanda kushangaa Sokwe? P.Kagame ni mtu wa propaganda sana, hivyo usimwamini sana, lkn kama una namba ya Watalii wanaofurika Rwanda ingesaidia isitoshe hata Kenya kwa mfano Watalii wengi wanakwenda shauri ya Mombasa, Malindi na Lamu na siyo Mbuga.

Kenya wapo mbele yetu kwenye beach tourism japo tuna long and stable coastline kuwazidi. Huu ni udhembe wetu binafsi

Kingine ambacho hujakielewa ni kuwa, watalii wanapenda EXPERIENCES na haijalishi wataipata wapi hivyo hata kama una mbuga au lolote lazma uwekeze katika hilo. Kitu ambacho tumeshindwa

Leo hii Arusha ilitakiwa kuwa EA city ya utalii yaani mtalii atoke mbugani then akamalizie Arusha. Bad enough baadhi huopt kwenda Nairobi au wakamalizie Zenji maana hatuna mji uliokaa fresh
 
Kwenda kuangalia Gorillas ni $1500 kwa mtu mmoja,Na wakitoka hapo wanaenda kufanya dark tourism(kucheki mafuvu/genocide sites/memorials),mambo wazungu wanayopenda wanayajua wenyewe.

Mwaka jana walipata tourist 1.7mil wa kuangalia vitu hivyo vya ajabu ajabu.
Mkuu ni aina ya utalii tu. Ukistaajabu ya serengeti, utayashangaa ya watalii kibao wanaoenda kushuhudia nyani wa Rwanda

Kingine beach tourism ipo worldwide tofauti na utalii wetu thou siwezi kupinga bado hatujautumia ipasavyo

dodge
 
Kwenda kuangalia Gorillas ni $1500 kwa mtu mmoja,Na wakitoka hapo wanaenda kufanya dark tourism(kucheki mafuvu/genocide sites/memorials),mambo wazungu wanayopenda wanayajua wenyewe.

Mwaka jana walipata tourist 1.7mil wa kuangalia vitu hivyo vya ajabu ajabu.

dodge

Ahsante kwa kuweka vitu straight maana huwa sipendi kubishana kwa vitu vilivyo obvious..

Uchawi wa mtalii ni EXPERIENCE bhasi. Mtu anayedhani wazungu wanaenda zenji sababu ya coast bhasi atakuwa hajui role ya stone town (historical) na cultural tourism.

Mtu hashindi ufukweni ni lazma kuna time atataka experiences nyingine. Hapo ndipo tunafeli
 
Ushauri mzuri,
Kwenda mbugani inakuwa nyongeza tu ya kwenye kifurushi cha kuhudhuria matamasha na kula raha kwenye fukwe.
 
Wanaofanya bookings data zao zinaonyesha Simba na mlima Kilimanjaro ni kivutio kuliko ZnZ.

Mtu atoke kote huko aache kwenda destination zenye beach resort za kueleweka aje Tanzania which is going to be more expensive kwake.

Kitu unachoweza kuki market nacho Zanzibar ni it’s historical significant hiko ndio kivutio sio beach that’s just an added bonus.

Another factor asilimia kubwa ya watalii wanaokuja Africa ni middle class, these are not the ppl who go to Ibiza and other cheap destination for their beach holidays kwa ivyo kama unataka kuwavutia through beach resort you would need to carter for all their taste na sidhani kama tuna investors wenye hela hizo au service sector iliyotayari kwenda na demand la kundi hilo.
 
Sasa beach zetu huku ukikutwa unachakata totozi kwny gari/mchangani police hawa hapa na matochi yao unaanza kumulikwa na pingu juu,huo utalii wa beach utatoka wapi.

dodge
wewe ni mdau wa sex tourism..
 
Barbarosa,
Beach tourism inaendana na biashara za ukahaba,nenda Copa Cabana,Mombasa,Zanzibar,Gambia,Mexico,Ibiza,Monaco,Capetown n.k.Mktaka watalii wajazane kwa utalii wa fukwe basi mhararishe ukahaba, halafu msije kushangaa watoto wa kike wa umri mdogo wakipata mimba na wavulana wakiwa mashoga na hapo ndio utamsikia Zitto akija na ujinga wa kusema mwanafunzi anyeshika mimba awe darasa moja na malaika
 
Ahsante kwa kuweka vitu straight maana huwa sipendi kubishana kwa vitu vilivyo obvious..

Uchawi wa mtalii ni EXPERIENCE bhasi. Mtu anayedhani wazungu wanaenda zenji sababu ya coast bhasi atakuwa hajui role ya stone town (historical) na cultural tourism.

Mtu hashindi ufukweni ni lazma kuna time atataka experiences nyingine. Hapo ndipo tunafeli
Uko sawa sana mkuu,hata kwenye seminars za mambo ya utalii hua tunaambiwa mtalii analipia 'EXPERIENCE' na sio kitu kingine chochote na msisitizo miaka yote hua unawekwa hapo tu,hivyo vingine ni ziada tu.

dodge
 
Back
Top Bottom