Waziri Kabudi, kabugi tena

Waziri Kabudi, kabugi tena

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
828
Reaction score
2,108
Baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Dr.Vincent Biruta kumuumbua Waziri wetu wa mambo ya nje Prof.Kabudi kuhusu mkutano wa wakuu wa nchi za EAC, vijana wa MATAGA wamehoji uhalali wa taarifa hiyo. Raifiki yangu mmoja ambaye ni Mbunge wa CCM amenitext "kaka nina wasiwasi na hiyo taarifa. Fuatilia sources zako vizuri. Taarifa ya EAC haiwezi kutolewa na Waziri wa Rwanda"
_
Rafiki yangu mwingine aliyepo masomoni China akaniambia "kaka kuwa mzalendo bwana. Ina maana unamwamini waziri wa Rwanda kuliko unavyomwamini Kabudi?"
_
Napenda kujibu kama ifuatavyo;

Kuhusu credibility ya taarifa hiyo it's very simple to prove. Ukienda kwenye website rasmi ya EAC utagundua nani mkweli kati ya Biruta na Kabudi. Taarifa iliyopo kwenye website hiyo inaeleza mkutano huo si wa Nothern Corridor bali ni wa wakuu wote wa nchi za EAC. Lengo ni kujadiliana kuhusu COVID19.

Mkutano wa kwanza (Extra Ordinary Summitt for EAC Heads of State) ulipangwa kufanyika April 15 lakini ukaahirishwa. Mkutano wa pili (Heads of State Consultative meeting) ukafanyika May 12 kwa njia ya mtandao ambao ulikua wa mashauriano kwa wakuu wa nchi za EAC kuhusu COVID19. Kwahiyo ukweli ni kwamba hatukutaka kushiriki kwa sababu zetu wenyewe na sio kusingizia "Nothern Corridor" au "Kitchen Corridor"
_
Pili ni kuhusu uzalendo. Nadhani kunahitajika shule kdg kuhusu uzalendo. Kuna watu wanaamini kutetea viongozi wako hata wanapoongea ujinga huo ndio uzalendo. No thank you.! Huo sio uzalendo ni uzwazwa.

Uzalendo ni kusimama na nchi yako na kutetea lile lililo sahihi. Kama kiongozi wako amekosea ukimkosoa kwa hoja wewe ni mzalendo. Lakini ukimtetea katika ujinga wake ili uonekane mzalendo wewe ni zwazwa tu kama mazwazwa wengine.

Friedrich Nietzsche aliwahi kusema "Mtu mwenye ufahamu mzuri si tu kwamba atawapongeza marafiki zake wanapofanya vizuri, bali pia atawakosoa wanapokosea."
_
Kama tunataka kuwa wazalendo tumwambie Kabudi aombe radhi kwa kulidanganya taifa kwa mbwembwe na tashwishwi. Na pia ajifunze kwamba hawezi kudanganya watu wote kwa nyakati zote. Dunia imebadilika. Ukidanganya leo, kesho utaumbuka tu. Usimjaribu BWANA Mungu wako, wala usiijaribu teknolojia.!
 
Mods nisaidieni ku-edit hiyo heading isomeke "WAZIRI KABUDI KABUGI TENA"
 
Mambo mengine hata ukiyajadili hayakusaidii...Vaa barakoa kapige kazi.
 
Screenshot_20200514-165931.png

Waambie hao majirani watawaua raia wao kwa njaa bure wawafungulie wakapige kazi, Corona bado ipo ipo tu. Hayo mambo ya Kabudi na mikutano mnapoteza muda wenu bure.
 
Viongozi wanapoongea ujinga na wasikilizaji wakafurahia na kushangilia huo ujinga basi kiongozi anawaona wasikilizaji ndio wajinga zaidi...

Huu ujinga sijui utaisha lini?
 
Mkuu nakupongeza kwa shule uliowapa Mataga leo. Ila ukibadilisha avatar yako basi watu watakuchukulia very serious kuliko hata Kigogo! Ombi langu ni hilo kwako. Ukombozi wa nchi hii utletwa na watu ambao ndio sisi.
 
Back
Top Bottom