Waziri Juma Aweso tunaomba uitazame na kutuondolea utapeli unaondelea Tanga UWASA

Waziri Juma Aweso tunaomba uitazame na kutuondolea utapeli unaondelea Tanga UWASA

Namche Bazar

Senior Member
Joined
Apr 8, 2019
Posts
122
Reaction score
179
Wakuu habari za asubuhi?

Mwaka 2022 nililipa kuunganishiwa maji kwenye nyumba yangu nilikaa zaidi ya miezi 4 bila kuwekewa huduma niliyolipia hadi ikapelekea kununua vifaa vyote vya kuunganishiwa maji isipokuwa mita pekee ndio nilipewa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira(TANGA UWASA) kwa kifupi nilipoteza pesa zangu kununua vifaa vingine huku tayari nikiwa nimeshalipia TANGA UWASA.

Mwaka huu pia nimelipia miezi miwili nyuma lakini hadi leo hii wanasema hawana vifaa kwa ajili ya kuunganishiwa maji wateja wapya.

Swali langu ni kwamba hawana storekeeper anajua minimum stock na maximum stock?

Haiwezekani miaka nenda miaka rudi wao kila siku vifaa vya kuunganishia wateja maji hakuna,huku wakiwa tayari wameshachukua fedha za wateja,huku kwenye maduka ya mtaani vifaa vyote wao tatizo ni nini hadi waseme kuwa vifaa hakuna??

Au wanachukua fedha za wateja na kuzizungushia kwanza (kufanyia biashara zao) na kupata faida kwanza kisha baada ya miezi ndio fedha hizo zinaenda kununua vifaa??

Kwa kifupi ni uzembe na uhuni wa kiwango cha PhD kuchukua fedha ya mtu kwa miezi kadhaa bila kumpa huduma stahiki.

Ninaomba wenye mamlaka hasa Waziri wa Maji Jumaa Aweso na timu yake achunguze hili suala kuondoa tabia mbaya za kitapeli zinazoendelea TANGA UWASA.
.
Lazima wawe na heshima na fedha za wateja,pia huduma ya maji ni ya haraka sio kuleta usanii.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom