Waziri Jenister Mhagama: Hakuna Serikali ya Magufuli

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Akitumia Kanuni ya 67 ya Kanuni za Kudumu za Bunge kumpa taarifa Mbunge,Waziri Jenister Mhagama amesema kuwa Tanzania hakuna Serikali ya Magufuli bali kuna Serikali ya CCM.

Mbunge aliyekuwa anapewa taarifa ni Mbunge wa Kilwa Kusini,Selemani Bundala almaarufu kama Bwege. Bwege alikuwa akiita Serikali ya Magufuli alipokuwa akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi. Waziri Mhagama alitaja Katiba iliyofanikisha CCM kuchaguliwa na kuunda Serikali. Bwege aliikataa taarifa hiyo ya Waziri!

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba, Dar es Salaam.
 
Boss bado tunatamani kujua mwisho wa Lugumi, na lini sukari itashuka bei.

Achana na hizo story zingine
Mambo ya Lugumi sahau, zitatengenezwa episode za kutosha, na Bunge likishamaliza Vikao vyake ndiyo usahau kabisa.
 
Akitumia Kanuni ya 67 ya Kanuni za Kudumu za Bunge kumpa taarifa Mbunge,Waziri Jenister Mhagama amesema kuwa Tanzania hakuna Serikali ya Magufuli bali kuna Serikali ya CCM.

Mbunge aliyekuwa anapewa taarifa ni Mbunge wa Kilwa Kusini,Selemani Bundala almaarufu kama Bwege. Bwege alikuwa akiita Serikali ya Magufuli alipokuwa akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi. Waziri Mhagama alitaja Katiba iliyofanikisha CCM kuchaguliwa na kuunda Serikali. Bwege aliikataa taarifa hiyo ya Waziri!

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam
CCM ni ile ile. Kama ilivyokuwa, ndivyo ilivyo na ndivyo itakavyokuwa... Kutegemea kuona mabadiliko ndani ya CCM, au mabadiliko nchini kupitia CCM ni ndoto za Alinacha!!!
 
Kazi kweli kweli.Mheshimiwa J. Mhagama,Serikali ya CCM ya awamu ya tano inaongozwa na nani?Dunia inatambua chama au kiongozi wa nchi?

CCM ikivurunda utakua tayari kusimamia hii kauli yako? Maswali yangu yakufikie popote ulipo mheshimiwa Waziri wetu.
 
Huyo Jenister naye atakuwa amelewa. Kwani Rais ni nani? Nani anayeunda serikali? Kwani ni makosa kusema kuwa Serikali ya Magufuli?
 
Kwa mtazamo wangu wote walikuwa sahihi. Kusema serikali ya Magufuli ni sawa na kusema Serikali ya CCM ni sawa na kusema Serikali ya Hapa Kazi Tu ni sawa
 
Nilimsikiliza nikasema hili suala linahusu ofisi yake au amejitolea kujibu.

Maana maelezo aliyotoa ni utata mtupu...
ukikimbia nchale...ukisimama nchale...wangekauka tu ... si kila kitu cha kujibu
 
Yule 'Bwege' alikuwa anampa muda JPM kabla ya kuanza kumpima...na ndio maana amekubali kuwa hii serikali si ya CCM ni ya JPM...kwa JPM hii ilikuwa bingo

Sasa huyu mheshimiwa kusema kuwa si ya JPM ni ya CCM alikuwa ame calculate asemacho au amejisemea tu...???

Huku mitaani watu wakikebehi kuwa CCM ni ile ile...???!!!
Sielewi nia yake ilikuwa kukinusuru chama na kumtosa JPM au nini????

Kuji differentiate na CCM kwa JPM ni mtaji so far....
 
Back
Top Bottom