PostGE2025 Waziri Dkt. Kijaji: Tujali utu na maslai ya Mtanzania

PostGE2025 Waziri Dkt. Kijaji: Tujali utu na maslai ya Mtanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amewataka watumishi wa wizara na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuhakikisha wanazingatia maslahi na utu wa Mtanzania wanapotoa huduma kwa wananchi.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo jijini Dodoma mara baada ya kuripoti kazini na kufanya mazungumzo na menejimenti ya wizara, muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema ni muhimu watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia utu na maslahi ya wananchi ili kuhakikisha wanapata huduma bora na maendeleo wanayostahili.

Amefafanua kuwa Ilani ya CCM imeweka mkazo katika ustawi wa watu, na ustawi huo hauwezi kupatikana endapo changamoto kama wanyamapori waharibifu hazitatatuliwa.

Ameongeza kuwa falsafa ya Kazi na Utu ya Rais inahitaji mtumishi kumweka mwananchi mbele: "unapomhudumia mtu, jiulize ungependa kuhudumiwa vivyo hivyo? Huo ndio msingi wa kazi yetu." amesema Dkt. Kijaji

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Hamad Hassan Chande ameishukuru menejimenti na watumishi kwa mapokezi mazuri na kusisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa kuzingatia utu.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbas, ameahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya ili kufanikisha malengo ya wizara na serikali, hususan katika kuhudumia wananchi na kutangaza vivutio vya utalii.

 
Back
Top Bottom