16 September 2023
KAZI YA KUIMARISHA TUTA KUZUIA MAJI KUTOROKA CHINI YA UKUTA WA BWAWA LA JNHPP RUFIJI
Engineer amueleza naibu waziri mkuu mheshimiwa Dr. Doto Biteko jinsi wanavyopambana kukabiliana na tishio la usalama ambalo ni changamoto ya maji kuweza kupenya chini ya bwawa la Julius Nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 91.72
Naibu waziri mkuu ameelezwa kwa kina kitaalamu kazi mkakati ya kuziba mianya inayoweza kuruhusu maji kupenya chini ya ukuta wa bwawa na kuharibu bwawa hilo la JNHPP Rufiji Stiegler's Gorge ambalo maji yamesha anza kujazwa toka mwaka 2022.
Mhandisi wa bwawa amesema kuwa bwawa hilo ambalo tayari maji yamejaa, chini ya ukuta na tuta la bwawa kuna mwamba ambao ndiyo msingi unaobeba ujazo huo mkubwa wa maji pamoja na ukuta na tuta .
Changamoto ni kuwa mwamba huo una nyufa na vipenyo vinaoweza kupitisha maji na kutishia stability ya ukuta wa bwawa pia tuta. Hivyo wameanza kutumia mbinu ya kawaida ya kiuhandisi inayoitwa grout curtain kuimarisha mwamba ambao ndiyo msingi wa bwawa hili kubwa.
Zoezi hili ya kutengeneza pazia la cement linatakiwa kurudia katika sehemu nyingi, kwa lugha rahisi mfano kama unavyo drill kutafuta maji ya kisima kirefu lakini katika mradi huu wa JNHPP ni ili kujaza cement maalumu ktk vipenyo na nyufa za mwamba kuhakikisha stability ya msingi wa ukuta wa bwawa unakamilika kuondoa tishio la bwawa kubomoka .
Changamoto iliyopo inafanana na ile ya Bwawa la Aswan lililojengwa Egypt ambalo wahandisi waliamua kuweka pazi la cement yaani grout curtain kutengeneza msingi mgumu kuzuia bwawa kubomoka. Video hii chini inaeleza jinsi pazia la cement yaani grout curtain linavyofanyika