Waziri Biteko: Suluhisho mojawapo la Uhaba wa Umeme ni kukamilika kwa mradi wa Bwawa la Nyerere

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,319
24,218
16 September 2023
KAZI YA KUIMARISHA TUTA KUZUIA MAJI KUTOROKA CHINI YA UKUTA WA BWAWA LA JNHPP RUFIJI

Engineer amueleza naibu waziri mkuu mheshimiwa Dr. Doto Biteko jinsi wanavyopambana kukabiliana na tishio la usalama ambalo ni changamoto ya maji kuweza kupenya chini ya bwawa la Julius Nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 91.72

Naibu waziri mkuu ameelezwa kwa kina kitaalamu kazi mkakati ya kuziba mianya inayoweza kuruhusu maji kupenya chini ya ukuta wa bwawa na kuharibu bwawa hilo la JNHPP Rufiji Stiegler's Gorge ambalo maji yamesha anza kujazwa toka mwaka 2022.

Mhandisi wa bwawa amesema kuwa bwawa hilo ambalo tayari maji yamejaa, chini ya ukuta na tuta la bwawa kuna mwamba ambao ndiyo msingi unaobeba ujazo huo mkubwa wa maji pamoja na ukuta na tuta .
1694922229926.png

Changamoto ni kuwa mwamba huo una nyufa na vipenyo vinaoweza kupitisha maji na kutishia stability ya ukuta wa bwawa pia tuta. Hivyo wameanza kutumia mbinu ya kawaida ya kiuhandisi inayoitwa grout curtain kuimarisha mwamba ambao ndiyo msingi wa bwawa hili kubwa.

Zoezi hili ya kutengeneza pazia la cement linatakiwa kurudia katika sehemu nyingi, kwa lugha rahisi mfano kama unavyo drill kutafuta maji ya kisima kirefu lakini katika mradi huu wa JNHPP ni ili kujaza cement maalumu ktk vipenyo na nyufa za mwamba kuhakikisha stability ya msingi wa ukuta wa bwawa unakamilika kuondoa tishio la bwawa kubomoka .

Changamoto iliyopo inafanana na ile ya Bwawa la Aswan lililojengwa Egypt ambalo wahandisi waliamua kuweka pazi la cement yaani grout curtain kutengeneza msingi mgumu kuzuia bwawa kubomoka. Video hii chini inaeleza jinsi pazia la cement yaani grout curtain linavyofanyika
 
Bwawa la Julius Nyerere lajazwa maji asilimia 43, kuzalisha umeme mwakani​

ALHAMISI , 6TH JUL , 2023
NA MWANDISHI WETU
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imebainisha kuwa mpaka kufikia mwezi Juni 2024, Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) litaanza kutoa huduma ya uzalishaji wa umeme.

MAKAMBA%20WEB%20.jpg

Waziri wa Nishati January Makamba
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nishati January Makamba, amesema kuwa bwawa hilo lenye Mita za ujazo bilioni 30 mpaka siku ya jana maji yaliyoingia ndani ya bwawa hilo yalikuwa na Mita za ujazo bilioni 13.8 sawa na asilimia 43 hivyo ni hatua nzuri ya utekelezaji wa ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) lililopo rufiji.
"Ndani ya msimu mmoja wiki iliyopita tulifikia kina cha chini cha kuzalisha umeme katika Bwawa wa Julius Nyerere, kina cha bwawa lote lile ni Mita 184 kutoka usawa wa bahari, kina kinachotakiwa ili bwawa lianze kuzalisha umeme ni mita 163. 61 kutoka usawa wa bahari maana yake ni kwamba tumefika na tumepita kina kinachotakiwa kuzalisha umeme," amesema Waziri Makamba
Aidha, Makamba amesema kuwa serikali imeanza mchakato wa kujadili usalama wa bomba la kusafirisha mafuta linalotoka Kigamboni Tanzania mpaka Ndola Zambia ambalo mwanzoni lilikuwa likisafirisha mafuta ghafi na hivi litasafirisha mafuta ya dizeli
 
MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE WAFIKIA ASILIMIA 80.2​

MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE WAFIKIA ASILIMIA 80.2
1694925021033.png

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, amesema kuwa utekelezaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha umeme wa kiasi cha megawati 2,115 umefikia asilimia 80.2.

Naibu Waziri Byabato ameyasema hayo tarehe 17 Januari, 2023, wakati Wizara ya Nishati ikitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.

“Kwa sasa utekelezaji wa mradi unaenda kwa kasi ambapo hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2022 umefikia asilimia 80.22, aidha mnamo tarehe 22 Desemba, 2022 zoezi la kuanza kujaza maji katika bwawa la JNHPP lilifanyika kwa kufunga mageti ya njia ya mchepusho.” Amesema Byabato

Kuhusu kazi ya ujazaji maji katika Bwawa la JNHPP amesema kuwa, hadi kufikia tarehe 16 Januari, 2023 kimo cha maji cha Bwawa kilifikia mita 112.48 kutoka usawa wa bahari kutokea kimo cha mita 74 tarehe 22 Desemba 2022.

Naibu Waziri ameongeza kuwa, utekelezaji wa mradi wa JNHPP unaenda sanjari na utekelezaji wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 400 kutoka eneo la mradi hadi Chalinze mkoani Pwani na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Chalinze ambapo kwa ujumla miradi hiyo inaendelea kutekelezwa kwa kasi.

Kuhusu malipo kwa mkandarasi wa mradi huo amesema kuwa, tayari Serikali imeshalipa asilimia 74.7 ya malipo hayo ambapo gharama za mradi huo ni shilingi Trilioni 6.5.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dunstan Kitandula amepongeza Serikali kwa utekelezaji wa mradi huo ikiwemo hatua ya kuanza kujaza maji kwenye bwawa hilo.

Aidha amesisitiza mradi huo kuendelea kutekelezwa kwa kasi ili asilimia za utekelezaji zilizobaki zikamilike kwa wakati.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Source : tovuti : nishati.go.tz
 
Yaani huyo waziri wa nishati ndio wa kutoa ushauri wa kitaalamu kwenye ziara mbele ya makamera?! Siasa nyingine bana.
 
Kwa nini zoezi la kuimarisha mwamba ambao ndio msingi halikufanyika kabla ya kujenga ukuta na kuanza kujaza maji?.

Kuna engineer mmoja mzawa siku za mwanzoni kabisa za mradi huu, alilielezea hili japo sio kwa kina na kuhakikisha kuwa wamechunguza na kugundua kuwa mwamba wz chini ni imara kuweza kuhimili pressure na ujazo maji yatakayozuiwa na ukuta....Alijibu kisiasa?

Hivi hayo maji yakiweza kupenya kwa chini, hilo Tsunami litakalotokea si litaangamiza bonde lote la Rufiji? ... 🤔
 
22 December 2023

TUKIO LA KUANZA KUJAZA MAJI BWAWA LA NYERERE RUFIJI STIEGLER'S GORGE

View: https://m.youtube.com/watch?v=oIL8TCb1LjQ

Mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme tanzania (Tanesco), Bw. Maharage Chande ameeleza hatua kwa hatua kuhusu ujenzi wa bwawa la Nyerere (JNHPP) na faida zitakazopatikana baada ya kukamilika kwa mradi huo unaotarajiwa kuzalisha megawati 2,115.

Bw. Chande ameyasema hayo leo desemba 22, 2022 wakati mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan akishuhudia tukio.
 
Kwa nini zoezi la kuimalisha mwamba ambao ndio msingi halikufanyika kabla ya kujenga ukuta na kuanza kujaza maji?.

Kuna engineer mmoja mzawa siku za mwanzoni kabisa za mradi huu, alilielezea hili japo sio kwa kina na kuhakikisha kuwa wamechunguza na kugundua kuwa mwamba wz chini ni imara kuweza kuhimili pressure na ujazo maji yatakayozuiwa na ukuta....Alijibu kisiasa?

Hivi hayo maji yakiweza kupenya kwa chini, hilo Tsunami litakalotokea si litaangamiza bonde lote la Rufiji? ... 🤔

= kuimarisha

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Shikamooo January

16 September 2023
KAZI YA KUIMARISHA TUTA KUZUIA MAJI KUTOROKA CHINI YA UKUTA WA BWAWA LA JNHPP RUFIJI

Engineer amueleza naibu waziri mkuu mheshimiwa Dr. Doto Biteko jinsi wanavyopambana kukabiliana na tishio la usalama ambalo ni changamoto ya maji kuweza kupenya chini ya bwawa la Julius Nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 91.72

View: https://m.youtube.com/watch?v=gfQCF6pL-U0

Naibu waziri mkuu ameelezwa kwa kina kitaalamu kazi mkakati ya kuziba mianya inayoweza kuruhusu maji kupenya chini ya ukuta wa bwawa na kuharibu bwawa hilo la JNHPP Rufiji Stiegler's Gorge ambalo maji yamesha anza kujazwa toka mwaka 2022.

Mhandisi wa bwawa amesema kuwa bwawa hilo ambalo tayari maji yamejaa, chini ya ukuta na tuta la bwawa kuna mwamba ambao ndiyo msingi unaobeba ujazo huo mkubwa wa maji pamoja na ukuta na tuta .
View attachment 2751860
Changamoto ni kuwa mwamba huo una nyufa na vipenyo vinaoweza kupitisha maji na kutishia stability ya ukuta wa bwawa pia tuta. Hivyo wameanza kutumia mbinu ya kawaida ya kiuhandisi inayoitwa grout curtain kuimarisha mwamba ambao ndiyo msingi wa bwawa hili kubwa.

Zoezi hili ya kutengeneza pazia la cement linatakiwa kurudia katika sehemu nyingi, kwa lugha rahisi mfano kama unavyo drill kutafuta maji ya kisima kirefu lakini katika mradi huu wa JNHPP ni ili kujaza cement maalumu ktk vipenyo na nyufa za mwamba kuhakikisha stability ya msingi wa ukuta wa bwawa unakamilika kuondoa tishio la bwawa kubomoka .

Changamoto iliyopo inafanana na ile ya Bwawa la Aswan lililojengwa Egypt ambalo wahandisi waliamua kuweka pazi la cement yaani grout curtain kutengeneza msingi mgumu kuzuia bwawa kubomoka. Video hii chini inaeleza jinsi pazia la cement yaani grout curtain linavyofanyika

View: https://m.youtube.com/watch?v=0VaCxQnrAFY
 
Ni wakati wa wahandisi wabobezi wazalendo kutafuta jibu, maana wahandisi ndiyo wanaoweza kukabiliana na changamoto iwe kubwa kiasi gani wao hutafuta ufumbuzi.

TOKA MAKTABA
29 May 2020

"Timu ya Taifa ya Wahandisi" kikosi Mahiri cha Wahandisi wazawa katika mradi wa JNHPP / STIEGLER'S GORGE RUFIJI

Mhandisi Robert Kabudi mwenye miaka 20 ya kusimamia miradi mikubwa ya ujenzi nje ya Tanzania pamoja na wahandisi wengine mahiri wazalendo wapo ktk mradi wa ujenzi wa Bwawa la Umeme la Rufiji linatotegemewa kuzalisha 2115 MW wa umeme Tanzania. Mhandisi Robert Kabudi anaitaja timu hiyo ya watu 21, kikosi anacho kibainisha kama timu ya kutizamwa duniani.

Timu hiyo ya wahandisi wa kiTanzania walio na ujuzikazi kwa vitendo, kuna mhandisi aliyepata kusimamia mradi wa kiwanja cha ndege cha Dubai kilichokuwa na bajeti ya zaidi ya US$ 3.5Bn. Miradi mikubwa ya Qatar, Abu Dhabi, Botswana , World Cup Africa Kusini 'wachezaji' wake waTanzania wazalendo wahandisi walishiriki ktk ujenzi huko ughaibuni.

Wahandisi hao chini ya kitengo cha Tanroads Engineering Consultanting Unit TECU wana kiu ya kuongeza CV zao ktk mradi huu wa Rufiji wenye bajeti kubwa kuliko iliyotumika ktk ujenzi wa Uwanja Mkubwa Mpya wa Ndege Dubai na hivyo si tu kuitambulusha Tanzania bali hata wahandisi wazalendo kwa ulimwengu kukitokea mradi wowote mkubwa nje ya Tanzania.

Soma zaidi source :

16 September 2023
KAZI YA KUIMARISHA TUTA KUZUIA MAJI KUTOROKA CHINI YA UKUTA WA BWAWA LA JNHPP RUFIJI

Engineer amueleza naibu waziri mkuu mheshimiwa Dr. Doto Biteko jinsi wanavyopambana kukabiliana na tishio la usalama ambalo ni changamoto ya maji kuweza kupenya chini ya bwawa la Julius Nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 91.72

View: https://m.youtube.com/watch?v=gfQCF6pL-U0

Naibu waziri mkuu ameelezwa kwa kina kitaalamu kazi mkakati ya kuziba mianya inayoweza kuruhusu maji kupenya chini ya ukuta wa bwawa na kuharibu bwawa hilo la JNHPP Rufiji Stiegler's Gorge ambalo maji yamesha anza kujazwa toka mwaka 2022.

Mhandisi wa bwawa amesema kuwa bwawa hilo ambalo tayari maji yamejaa, chini ya ukuta na tuta la bwawa kuna mwamba ambao ndiyo msingi unaobeba ujazo huo mkubwa wa maji pamoja na ukuta na tuta .
View attachment 2751860
Changamoto ni kuwa mwamba huo una nyufa na vipenyo vinaoweza kupitisha maji na kutishia stability ya ukuta wa bwawa pia tuta. Hivyo wameanza kutumia mbinu ya kawaida ya kiuhandisi inayoitwa grout curtain kuimarisha mwamba ambao ndiyo msingi wa bwawa hili kubwa.

Zoezi hili ya kutengeneza pazia la cement linatakiwa kurudia katika sehemu nyingi, kwa lugha rahisi mfano kama unavyo drill kutafuta maji ya kisima kirefu lakini katika mradi huu wa JNHPP ni ili kujaza cement maalumu ktk vipenyo na nyufa za mwamba kuhakikisha stability ya msingi wa ukuta wa bwawa unakamilika kuondoa tishio la bwawa kubomoka .

Changamoto iliyopo inafanana na ile ya Bwawa la Aswan lililojengwa Egypt ambalo wahandisi waliamua kuweka pazi la cement yaani grout curtain kutengeneza msingi mgumu kuzuia bwawa kubomoka. Video hii chini inaeleza jinsi pazia la cement yaani grout curtain linavyofanyika

View: https://m.youtube.com/watch?v=0VaCxQnrAFY

Maelezo mengi sisi hatutaki, sisi hatutaki nyufa katika bwawa letu na hela trillions of Tshs zimetumika, hayo hawakuyajua wakati wa kujenga mwamba wa msingi hadi wajue baada ya nyufa kutokea, Bwawa letu liwe imara for centuries wasilete utani
 
Ni kweli bora uongozi ufafanue mikakati ya kukabiliana na changamoto hii katika mradi hadi ukimtazama Naibu Waziri Mkuu lugha yake ya mwili body language ana wasiwasi.

Jingine hili la January Makamba kuhamishwa wizara toka Nishati kwenda Mambo ya Nje ni kutokana na hii changamoto. Na pia Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen L. Byabato kuhamishwa pamoja na bosi wake January Makamba ni jambo fikirishi sana ukiunganisha na ziara hii ya Naibu Waziri Mkuu bwawa la JNHPP Rufiji kisha kuambiwa changamoto hii kubwa.

Sababu nne Rais Samia kufanya mabadiliko Baraza la Mawaziri

1 Sept 2023 — Sasa wizara hiyo imepewa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki ambaye ni Stephen Byabato, aliyetokea Nishati. Sababu....
 
Back
Top Bottom