PreGE2025 Waziri Aweso: Aitaka DAWASA kuwaunganishia maji wananchi watakaonufaika na Mradi wa Maji wa Bangulo kwa ufanisi na uaminifu

PreGE2025 Waziri Aweso: Aitaka DAWASA kuwaunganishia maji wananchi watakaonufaika na Mradi wa Maji wa Bangulo kwa ufanisi na uaminifu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuwaunganishia maji wananchi watakaonufaika na Mradi wa Maji wa Bangulo kwa ufanisi na uaminifu, na kuhakikisha hakuna mianya yoyote ya rushwa itakayojitokeza kwani kuunganishiwa maji ni haki ya msingi ya mwananchi.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Waziri Aweso ameyasema hayo Jumanne, Machi 18, 2025, alipotembelea mradi huo uliopo mtaa wa Bangulo Hali ya Hewa, katika kata ya Pugu Station, wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam. Mradi huo unatarajiwa kunufaisha wananchi 450,000 wa kata mbalimbali za wilaya hiyo na wilaya jirani.

 
Back
Top Bottom