Waziri Augustine Mahiga: Tamko la Rais ni sheria!

Ndiyo maana ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu. Amri yake haihojiwi lazima itekelezwe kwa mamlaka yake ktk Ulinzi na Usalama wa Taifa. Na ana "kinga" ya kutoshitakiwa.
Ana kinga ya kutoshtakiwa kwa yale atakayofanya akiwa madarakani ambayo yapo katika mamlaka yake kisheria (jurisdiction). Kwahiyo akifanya jambo nje ya mamlaka yake (ultra vires) anashtakika na kupandishwa mahakamani vizuri tu. Mamlaka ya Rais na mipaka yake inawekwa na katiba. Kisheria hakuna mtu aliye juu ya katiba.
 
Amezuia mikutano ya vyama vya Siasa, iliyowekwa kikatiba na ameweka utaratibu wake mwingine wa kufanya mikutano hiyo na ametoa sababu ya kufanya hivyo, nani amemshitaki? Wanasheria wamelijua hilo ndio maana wako kimya.
 
Huyo mzee naye ndo maana hujikojolea hovyo hovyo!
 
Jee kujua kuna msongamano wa watu magerezani, ilibidi kwenda kulishuhudia Mwanza. Mbona hapo Keko karibu ya magogoni pamefurika
Hiyo ndiyo inaitwa "east or west, home is best"

Kama kuna magereza mengi nchini, lakini Rais ameamua kwenda kuliangalia gereza la "nyumbani" kwake
 
Baba wa Taifa alisema, “Katiba ya nchi inanipa madaraka makubwa sana. Akija mtu na kuyatumia vibaya madaraka hayo makubwa sana basi atakuwa kama mungu.”

Hakukosea hata chembe. Imagine kama angekuwa bado yuhai jinsi angemchana huyo nduli na dikteta tena bila kukwepesha si hawa waovu wengine Mkapa na Kikwete wanahofia hata kukohoa kwa jinsi wanavyomuhofia huyo mwendawazimu.

 
Ndiyo maana tulifanya kosa kubwa kuipoteza fursa nzuri sana ya ile Rasimu ya Katiba ya Warioba na kwa namna huyu unayemwita nduli anavyoendesha nchi hii kwa sasa ni ndoto kuipata Katiba mpya!
 
Reactions: BAK
Naam hawa wahuni na mainterahamwe waliona kifo cha ccm hivyo wakaamua kupora majadiliano yale.

Ndiyo maana tulifanya kosa kubwa kuipoteza fursa nzuri sana ya ile Rasimu ya Katiba ya Warioba na kwa namna huyu unayemwita nduli amavyoendesha nchi hii kwa sasa ni ndoto kuipata Katiba mpya!
 
Yuko sahihi tamko lolote la Mheshimiwa Rais linakuwa sheria kwa sababu lazima litekelezwe. Ndiyo maana Rais hawezi kuongea jambo lolote hadharani kisha ukasema ni maoni yake. Rais hana maoni binafsi. Hivyo chochote anachoongea kwa umma kina impact.
Hahaha huu ujinga hata mimi nimeona.
 
Keshakuwa mganga njaa tu. Akili kubwa haiwezi kuacha nchi ikaendeshwa kwa mihemko na matamko. Ukweli ni kuwa, akili kubwa hata ambazo tulizijua na kuzipenda zamani hasa ndani ya Lumumba, kwa wengi sasa hivi hazipo. Tumekubali kuunda kwa bidii taifa LA wanafiki. Taifa linalothamini na kusifia UGANGA njaa kama ndio MBINU ya kisasa badala ya akili na busara. Amen.
 
Wanasheria watz walinyamazishwa. Katikatu ya vitisho vya maguvu ya dola, Lissu aliongea
Amezuia mikutano ya vyama vya Siasa, iliyowekwa kikatiba na ameweka utaratibu wake mwingine wa kufanya mikutano hiyo na ametoa sababu ya kufanya hivyo, nani amemshitaki? Wanasheria wamelijua hilo ndio maana wako kimya.
 
Sasa,mrundikano huo MBNA upo nchi zima.
Ccm,wanajikanyaga kanyaga sana.kiburi cha jiwe
 
Wanasheria watz walinyamazishwa. Katikatu ya vitisho vya maguvu ya dola, Lissu aliongea
Kila mu anauwezo wa kuongea. Mwanasheria tunamtegemea atumie ujuzi wake kwa kuchukua hatua za kimahakama. Lissu anaesimama mahakamani kumtetea mtusi wa mitandaoni anashindwaje kutetea nguvu ya katiba mahakamani? (Kama kweli imekiukwa)
 
Lakini hapaswi kuongea kitu "against" Katiba yetu ya nchi na ndiyo sababu kabla ya kuanza kutekekeza madaraka yake ya Urais, anaapa kuwa ATAIHESHIMU na KUITII Katiba ya nchi yetu. Full Stop

Sijui kama kweli hujui kwamba Tanzania ilishakuwa banana republic muda mrefu sana kabla ya awamu hii. Nchi imekuwa ikiendeshwa kwa “busara za rais”. Mahiga is smart; anaijua hali halisi. Rais ndiyo katiba; ndiyo sheria hadi siku mtakapofanikiwa kurejesha utawala makini nchini.
 
Nijuavyo mimi ni kuwa kauri ya Rais ni amri na sio sheria,ndio maana anaweza akaongea kitu huku anacheka na baada ya muda mchache kitu kile alichokiongelea kinatekelezwa,na ingekuwa kauri ya Rais ni sheria basi nafikiri watu wangekuwa wanahukumiwa kwa kunukuu baadhi ya kauri za Marais walioyatamka hasa kwenye taasisi husika (Mahakama)
 
Hahahahaaa...nimependa hapo..'kama ni mtu wa harahaharaka huwezi kumwelewa'
 
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…