Waziri apiga marufuku mifugo kuchanjwa kiholela. Ataka Wataalamu watumike badala ya Wafanyabiashara

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amepiga marufuku halmashauri zote nchini, kutotumia wafanyabiashara kuchanja mifugo.

Waziri huyo ametaka mikataba ya halmashauri na wafanyabiashara hao kuvunjwa mara moja.

Ndaki alibainisha hayo jana alipofanya ziara ya siku moja mkoani Shinyanga katika josho la kuogeshea mifugo la Kijiji cha Mipa Wilaya ya Kishapu.

Akiwa katika kijiji hicho, alishuhudia uogeshaji mifugo na utoaji wa chanjo ya homa ya mapafu kwa ng’ombe. Wafugaji walimlalamikia kuwa baadhi ya ng’ombe kijijini hapo, wamekuwa wakivimba na wengine kufa baada ya kupatiwa chanjo.

Ndaki akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul alisema kuanzia sasa chanjo zote nchini, zitatolewa na wataalamu wa wizara waliothibitishwa.

Ndaki aligoma kushuhudia zoezi la uchanjaji lililokuwa limeandaliwa, kutokana na kukasirishwa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kutokuwa na takwimu yoyote ya idadi ya ng’ombe waliovimba na wengine kufa baada ya kuchanjwa.

“Kuanzia sasa halmashauri zetu zote ni marufuku kutumia wafanyabiashara kuchanja mifugo yetu, halmashauri zitumie wataalamu wa wizara ambao wamethibitishwa ili waweze kuchanja mifugo ya wananchi wetu,” alisema.

Aliongeza “Hao wafanyabiashara kama mmeingia mikataba nao, hiyo mikataba ivunjeni haraka. Hatuwezi kuchezea akili za watu namna hii. Hatuwezi kutuma wafanyabiashara waende kuchanja ng’ombe, halafu ng’ombe hao wanavimba na kufa halafu taarifa hatuna.”
 
Hivi hapa nchini tuna jumla ya mifugo milioni ngapi vile? Je tunao vertenary officers wa kutosha kila kijiji au kata? Tofauti ninayoiona kati ya wafugaji wa kanda ya ziwa na Wamasai au wamang'ati ni kwamba Wamasai kwanza wako makini sana na magonjwa ya mifugo na dawa wanazijua na kuzinunua wenyewe, wakimuita bwana mifugo labda ni kwa cases kubwa kubwa. Pia wengine wana majosho yao au wana spray wenyewe mifugo yao. Kanda ya ziwa wako so dependant kwa serikali wakati mifugo ni yao wenyewe. Mimi wakati niko sekondari vertenary mmoja pale kijijini alinifundisha uhudumiaji wa mifugo mpaka nikawa napiga sindano zile za kawaida, kuwapa mifugo dawa za minyoo etc...
 
Back
Top Bottom