Waziri Angellah Kairuki: Watumishi waliobainika na vyeti feki na kuhisi wameonewa, waandike barua

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Watumishi waliobainika na vyeti feki na kuhisi wameonewa, Waziri Angellah Kairuki amelieleza Bunge kuwa watatakiwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu na nakala kwa baraza la mitihani.

Amesema barua hizo ziambatanishwe na nakala za vyeti vilivyomo kwenye faili lake la ajira na vitapitiwa kwa umakini zaidi.

Ameonya kuwa endapo mtu atakata rufaa wakati anaujua ukweli adhabu itakuwa kubwa zaidi.

My take: Sasa kama itaonekana rufaa yao baadhi kuwa sahihi na hawakuwa na vyeti feki..! Nani atapaswa kuwajibika kwa hilo? Ni vema sheria kuangalia pande zote ili kuondoa usumbufu..!

Chanzo: Mwananchi
 
Mamlaka za uaji kazi yao nini?
Mbona waziri anamaliza muda wake wa kazi kwa swala dogo sana!!!!?

Wakiandika wote barua si mtachambua na kushughulikia mpaka 2022?
 
Watumishi waliobainika na vyeti feki na kuhisi wameonewa, Waziri Angellah Kairuki amelieleza Bunge kuwa watatakiwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu na nakala kwa baraza la mitihani.

Amesema barua hizo ziambatanishwe na nakala za vyeti vilivyomo kwenye faili lake la ajira na vitapitiwa kwa umakini zaidi.

Ameonya kuwa endapo mtu atakata rufaa wakati anaujua ukweli adhabu itakuwa kubwa zaidi.

Chanzo: Mwananchi
Kama anaonya aanze kujionya yeye au kujiuzuru maana hayuko makini. Unataka upande mmoja uwe na haki tu mwingine hapana. Huu ni ujinga mkubwa
 
Kweli sasa naamini kuwa nchi yetu ya Tanzania ilifikia pabaya sana tena sana!!!
Hatari sana, kumbe ndio maana tulikuwa hatusongi mbele!!!!
Sina huruma na watu Wa aina hiii!!
 
Anapiga biiitiii....
Akwende zake...
Anadhani akiongea maneno makali watu wataogopa kufatilia haki zao...
Wana haki ya kulalamika km kweeli wameonewa
 
kama umefoji vyeti tulia..kama unahisi umeonewa peleka vithibitisho vyote sehemu husika..mbona simple tu
 
kama umefoji vyeti tulia..kama unahisi umeonewa peleka vithibitisho vyote sehemu husika..mbona simple tu
Kazi rahisi tu.. Kama mimi napeleka barua ikiambatana na nakala kwa baraza la mitihani, huo mkwara hamna shida.
 
Back
Top Bottom