mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,586
- 11,225
Wakuu ikiwa ni miezi michache kupita tangu nilipo ripoti ufisadi wa kutisha kiwanda cha karatasi Mgololo, wizara ya viwanda iliuandikia uongozi wa kiwanda kueleza kuwa waziri atatembelea kiwanda hicho.Ziara hiyo ilitakiwa kufanyika mapema wiki hii.
mwanzo nilipata taarifa za maandalizi makubwa yanayofanywa kumpokea mgeni huyo siku inayofuata. Hata hivyo ziara hiyo iliota mbawa na waziri hakuja.
Niliwasiliana na (mnaa) wangu kujua kwanini waziri hakuja. Mnaa wangu ni mtu wa karibu na maafisa wa kiwanda. Alinitonya kuwa ziara hiyo ilipokelewa na ushirikina wa kutisha kutoka kwa uongozi wa kiwanda.
Mnaa wangu akanijulisha kuwa "Dawa zilimwagwa njia ambayo waziri angepita kuanzia sawala mpakagololo" Taarifa Nyeti kutoka kwa meneja inadai kuna mahirizi ya kihindi yalijazwa ofisini.Licha ya kuwa serikali haiamini mambo haya ukweli ni kuwa waziri angetua angekuwa na nafasi finyu kutoa maamuzi magumu.
Haieleweki mpaka sasa Kama kuna mtu alimtonya waziri kuhusu unyama unao andaliwa hivyo kumzuia asije ama hii midawa imemzuia asije.Hata hivyo tetesi kutoka wizarani zinadai kuwa ziara hiyo itafanywa ghafla.
Kiwanda cha karatasi mgololo kilipata kuwa kiwanda kikubwa Sana afrika mashariki na Kati.Kilijengwa miaka ya 1980 kwa jasho la Wakulima wakati wa utawala wa mwalimu.Kilikuwa ni cha tatu kwa ukubwa duniani kikitanguliwa na kile cha katatasi Norway na chakaratasi South Africa.
kilibinafsishwa mwaka 2003 kwa kampuni ya Rai Group katika kile kinachotajwa kuwa mkataba wenye utata mkubwa.
My take: Kuna uozo ! uozo usio tamkika! serikali isifumbie macho kiwanda cha karatasi mgololo.