Ndugu zangu wana JF napenda kuwauliza kuwa Mhe. Waziri ana mamlaka gani kumsimamisha kazi mtumishi wa umma?.
Nijuavyo mimi kisheria kama mtumishi anatuhumiwa basi ataandikiwa barua ikitaja orodha ya tuhuma zinazomkabili
(2) Mtuhumiwa atatakiwa kujibu tuhuma dhidi yake kwa muda atakaopewa.
(3) Kama majibu ya tuhuma zake hazijitoshelezi basi.
(4) Atasimamishwa kazi kwa muda .
(5) Mwajiri ataunda Tume ya uchunguzi dhidi ya tuhuma zake na Tume itapewa muda maalum kumaliza kazi iliyopewa.
(6) Tume itarudisha matokeo ya uchunguzi kwa mwajiri na mapendekezo kukiwa na ushahidi tosha ya hatua inayotakiwa kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.
(7) Hatua kuchukuliwa kufuatana na mapendekezo ya Tume.
Wote tunafahamu kuwa sheria zipona mbona sheria hizi hazitumiki ili watumishi wapate haki zao. Mfano hai ni yule Mtendaji Mkuu wa WMA. Katika nchi yeyote inayofuata demokrasia lazima kuwepo na UTAWALA BORA