Waziri akiri kununua nyumba ya mabilioni!

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,591
1,599
Waziri Maige amekiri kununua bonge la mjengo maeneo ya Mbezi Beach kwa mabilioni!
Fuatilia mwenyewe kweye huu uzi ujionee wanaojiita wenzetu wanavyolitafuna hili taifa wakati sisi tukiambiwa tukaze mikanda!
Waziri akiri kununua nyumba ya mamilioni
sosi ni mwananchi...
Waziri akiri kununua nyumba ya mamilioni Send to a friend
Wednesday, 25 April 2012 22:42




0diggsdigg

nyumba-maige.jpg
NI EZEKIEL MAIGE, ADAI ALIINUNUA KWA DOLA 410,000, LEMBELI APINGA, ASEMA ALIINUNUA KWA DOLA 700,000 TASLIMU
Fidelis Butahe na Daniel Mjema
SIKU chache baada ya gazeti hili kuripoti taarifa za uchunguzi kwamba kuna mawaziri wawili ambao wamenunua nyumba mbili zenye thamani ya Sh1.8 bilioni, mmoja wa mawaziri hao, Ezekiel Maige wa Maliasili na Utalii ameibuka na kukiri.Maige aliliambia gazeti hili jana kuwa nyumba yake hiyo iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam, ameinunua kwa Dola za Marekani 410,000 (takriban Sh656 milioni) ambazo anadai kuwa ni mkopo kutoka Benki ya CRDB.

Hata hivyo, wakati Waziri Maige akieleza kuwa nyumba hiyo ina thamani hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli amedai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba ilinunuliwa kwa fedha taslimu Dola 700,000 za Marekani (takriban Sh1.1 bilioni).

Awali, habari zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa Waziri Maige alinunua nyumba hiyo kutoka kwa Kampuni ya Savana Real Estate.

Mmoja wa madalali wanaouza nyumba za kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Athuman (Ustadhi) alilithibitishia gazeti hili kwamba Waziri Maige amenunua nyumba moja kati ya nne zilizoko sokoni.

Hata hivyo, dalali huyo hakutaka kueleza alinunua nyumba hiyo lini na kwa gharama gani baada ya kueleza kuwa yeye si msemaji wa kampuni hiyo.

“Nyumba zipo nne na mbili zimeshauzwa. Maige kanunua nyumba moja. Nyumba nyingine mbili bado hazijauzwa na kwa sasa tunamalizia kuziwekea milango na bustani,” alisema Athuman.

Akizungumza na gazeti hili jana, Waziri Maige alisema hakununua nyumba hiyo kwa Dola 700,000 kama inavyodaiwa, bali alinunua kwa Dola za Marekani 410,000.

Mbali ya kukiri, alifafanua jinsi alivyoinunua na kuonyesha nyaraka mbalimbali huku akieleza kuwa sehemu ya fedha alizonunulia, zilikuwa za mkopo kutoka Benki ya CRDB.

Alisema mwaka 2005 alipoanza kuwa mbunge alipata mkopo na yeye na wenzake watatu, waliunda kampuni ya kusafirisha mzigo ya Splendid Logistic na kuanza kununua magari matatu na baadaye magari hayo yaliongezeka na kufikia saba.

maige%20ezekielwaziri.jpg
Waziri wa Maliasili na Utalii,Ezekiel Maige

Alisema Septemba, 2010 mwenzao mmoja alijitoa katika kampuni hiyo na hivyo wakaamua kugawana mali kwa kuzingatia mtaji wa kampuni. Alipata magari mawili na mwenzake manne na kuongeza kuwa gari moja kati ya hayo saba lilipata ajali.

Alisema baada ya hapo aliamua kuanzisha kampuni nyingine ya kusafirisha mizigo ambayo inaendeshwa na mke wake... “Kampuni hiyo inaitwa Mem Logistic na ina magari mawili.”

Alisema magari hayo aliyakodisha kwa kampuni nyingine ya Bravo Logistic ambayo kila mwezi inamlipa Dola 20,000.

Alisema alipochaguliwa tena kuwa mbunge mwaka 2010 aliamua kutoongeza magari katika kampuni yake na kuanza kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

“Baada ya uchaguzi nilichukua mkopo wa Sh200 milioni katika Benki ya CRDB, baadaye Ofisi ya Bunge ilinikopesha Sh90 milioni kwa ajili ya kununua gari, fedha hizo zote nilizichukua na kuzihifadhi,” alisema Maige.

“Hizo fedha nilikaa nazo nikawa nataka kujenga nyumba baadaye nikaona nitafute nyumba ya kununua tu. Baadaye dada yangu, Angelina Ngarura ambaye ana kampuni ya kuuza matrekta, Dar es Salaam alinifuata na kuniomba fedha hizo kwa ajili ya kuzizungusha na tukakubaliana kuwa atakuwa akilipa riba ndogo kwa makubaliano kwamba siku yoyote nikizihitaji nitazichukua,” alisema.

Alisema ndipo alipopata nyumba iliyokuwa ikiuzwa Dola 450,000 lakini alikubaliana na muuzaji na kuuziwa kwa Dola 410,000.

Alisema katika ununuzi huo, hakuwa na kiasi hicho cha fedha kwani nyingine zilikuwa katika mzunguko katika kampuni ya dada yake na hivyo kuamua kwenda kukopa Dola 200,000 katika CRDB.

Alisema baada ya kupewa fedha hizo za mkopo, hati ya nyumba hiyo ilibaki benki kwa makubaliano kwamba akishindwa kulipa, benki itaichukua.

“Tuliingia mkataba na CRDB kulipia nyumba ile kwa miaka minne na mpaka sasa hivi nalipia Dola 5,127 kila mwezi, haya yote yapo kwa Kamishna wa Maadili,” alisema Maige.

Huku akionyesha mikataba ya ununuzi wa nyumba hiyo, nyaraka za mkopo wa benki, Maige alisema awali, alikuwa na magari mawili ambayo aliamua kuyauza na kununua gari nyingine aina ya BMW kwa Sh70 milioni.

Alidai kwamba kama kuna mali kinyume na hizo yuko tayari kuapa hata kwa Biblia Takatifu na kusisitiza kuwa hivi sasa kuna mapambano ya kisiasa ndiyo maana shutuma dhidi yake zinaibuka kila kukicha.

“Ukisikia mali zangu tofauti na hizo ni uongo ndugu yangu na kwa mkopo niliochukua wakati nikiwa mbunge sina hela mpaka Juni 2015,” alisema na kuongeza:
“Nikijiuzulu ubunge leo hii maana yake ni kwamba itakuwa kazi kweli na sitaweza kulipa mkopo. Sijakopa kwa kivuli cha ubunge wangu, nimekopa kama Maige kwa sababu kiwango cha kukopa bungeni nimeshakimaliza.”

Maige alidai kuwa hivi sasa habari mbaya zinaibuka dhidi yake akidai kwamba kuna watu ambao hata hivyo, hakuwataja kwamba ndiyo wanaopanga mikakati ya kumhusisha na mambo mbalimbali ili aonekane si mwadilifu katika jamii.

Lembeli: Amenunua taslimu

Wakati Maige akisema alikopa fedha hizo benki, Lembeli alidai kwamba anazo taarifa kwamba waziri huyo alinunua nyumba hiyo kwa fedha taslimu.

“Nilianza kusikia na baadaye kuthibitishiwa. Kuna watu waliokuwa na nyaraka wakasema wana ushahidi kuwa nyumba hiyo ni ya mheshimiwa waziri,” alisema Lembeli na kuongeza:

“Baadaye nikasoma kwenye magazeti kwamba mawaziri wawili vijana, wamenunua nyumba za mabilioni, sasa kama watu wanasema sioni sababu ya kupuuza madai hayo.”

Lembeli alisema si kosa kwake na wengine kuamini taarifa hizo kwa kuwa watu waliompa walizitetea kwa ushahidi na waliamua kufuatilia suala hilo baada ya kukumbana na ukiritimba mwingi walipokuwa wakitafuta huduma wizarani.

“Usipowatendea watu haki, hakika watakufuatilia na mimi sina sababu ya kutilia shaka kauli ya watu hao kwamba nyumba hiyo ni ya Maige na imenunuliwa kwa Dola 700,000,” alisema.

 
Sababu kubwa ya kiwete kuwatetea hawa mawaziri wezi ni kwasababu anawatumia hao hao naye kufanikisha wizi wake wa maliasili za Taifa toka kwenye madini mpaka kwenye wanyama pori!!Sasa wote tujiulize wale wanyama pori waliopelekwa na ndege ya jeshi toka Qatar, je walichukuliwa bila ya mkuu wa nchi kuwa na taarifa? Uchunguzi juu ya swala hili uliamriwa na bunge mbona mpaka sasa kuko kimya kwanini? Kichwa kikioza mwili mzima lazima utaoza na ndio matatizo tuliyonayo katika utawala wa nchi hii!!
 
kudhibiti ufedhuri huu lazima nchi yetu ichukue vipengele vilivyomo kwenye ktb ya china inayousu uhujumu uchumi
 
Sababu kubwa ya kiwete kuwatetea hawa mawaziri wezi ni kwasababu anawatumia hao hao naye kufanikisha wizi wake wa maliasili za Taifa toka kwenye madini mpaka kwenye wanyama pori!!Sasa wote tujiulize wale wanyama pori waliopelekwa na ndege ya jeshi toka Qatar, je walichukuliwa bila ya mkuu wa nchi kuwa na taarifa? Uchunguzi juu ya swala hili uliamriwa na bunge mbona mpaka sasa kuko kimya kwanini? Kichwa kikioza mwili mzima lazima utaoza na ndio matatizo tuliyonayo katika utawala wa nchi hii!!

Kutokana na kukosekana kwa uadilifu viongozi wataendelea kuwa wezi huku wakisingizia kuwa wamekopa pesa benki na kwamba mashambulizi juu ya mali zao ni vita ya kisiasa zaidi. Kutokana na utamaduni huu wa kutofuata maadili ya uongozi maendeleo ya nchi yataendelea kudumaa siku hadi siku.
 
Kwa nchi zilizoendelea huwezi kununua nyumba ya kiasi hicho bila kueleza umepataje hizo hela,kwa mfano ni mtoto wa EL alipotaka kununua nyumba UK,nafikiri wote tunajua jinsi alivyotakiwa kuthibitisha vyanzo vya mapato,mimi nilitarajia Mheshimiwa kijana atupe na makato ya kodi ya biashara anazofanya ili kujiridhisha na kipato cha biashara zake,haya mambo ya kusema nilimpa dada azungushe sio sababu na pia kukopa benki sio tija kwani benki kama CRDB ni chaka la mafisadi.hatujasahau EPA zilivyopita kwenye benki hiyo,na kukopa benki ni janja tu ya kujifanya hawa waheshimiwa kwani wana pesa za kumwaga ,wanatumiakukopa ili kudanganya umma,sasa huyo ni Magige mtru wa juzi tu je sijui bwana misamaha ana bingo kiasi gani,tafakari
 
sasa nimeendalea kupata mwanga kwa nini kwanini baba riz kaweka washikaji zake kwenye nafasi mbalimbali za uongozi,hy ni sababu wapate ulaji kwa urahisi.watu wamejenga kwenye open space mkuu kakaa kimya tuu,raia wananyang'anywa ardhi na kupewa wageni baba riz anatabasamu tu,watanzania tugangamale nchi inatafunwa tu na wajanja,sasa kama huyu maige si juzi kapata huo uwaziri lkn anamiliki mabilioni fisadi papa huyo,watanzania tuhakikishe katiba inayokuja lazima iwe na vipengele vya kudhibiti mafisadi wasipate tena mwanya kama walionao sasa.nawasilisha
 
Maige in fisadi hakuna gari kwenye logistics la kulipwa dolla 20,000 kwa mwezi ni muongo. Magari mengi ni kati ya dollar 6,000-10,000.Ni transporter kichaa mwenye kufanya biashara kichaa huyo.Hii kampuni ya Bravo Logistics pengine inaweza kukubali kulipa hizo DOLLAR 20,000 kwa SABABU YA MASLAHI YA BIASHARA YA MAGOGO KWENDA ULAYA NA CHINA.Kumbukeni kuwa wizara hii inahusika na mali asili ikiwemo misitu.Na ufisadi mkubwa upo kwenye misitu na magogo na mkaa na Maige anahusika moja kwa moja. Bravo inasafirisha magogo mengi tu na uhifadhi maeneo ya bandarini kurasini.
 
Dollar 20,000.00 ,kwa mwezi. mzigo hadi DRC ni dollar 6,500-10,000 na inasafiri mwezi mzima,huyo mkodishaji anakodisha kwa 20,000 mbona anapata hasara. come on man...
 
Sheria ya wahujumu uchumi ilifutwa?? Mimi naona irudi kama ilifutwa. Hawa wote wafilisiwe kwanza ndio kingine kifuate!!!
 
Back
Top Bottom