Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 92,232
- 111,751
Akizungumza na Nipashe jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, alisema viongozi hao wanatakiwa kutumia busara zaidi kuliko kuwakomoa watumishi pale wanapokosea kwa kuwaweka mahabusu.
“Watumishi wengi wakiwamo waganga wakuu, walimu wamekuwa wakiwekwa ndani na wakuu wa mikoa ama wilaya kwa madai ya kutowajibika, lakini lazima ieleweke kila mmoja majukumu yake,” alisema Simbachawene.
Simbachawene alisema kwa mujibu wa sheria, pamoja na wakuu wa mikoa kuwa na mamlaka ya kumweka mtu mahabusu kwa saa 48 na mkuu wa wilaya saa 24, lakini ni pale mhusika anapokuwa katika hatari ya kushambuliwa na kudhuriwa na wananchi.
Alisema ingawa viongozi hao wana mamlaka ya kumweka mtumishi mahabusu kwa muda huo, lakini wakati huo lazima mchakato wa kimahakama uwe unaendelea.
“Haitakiwi kuamuru mtumishi wa serikali kumweka mahabusu kwa nia ya kumpa adhabu, njia nzuri ni kumhifadhi humo kwa nia nzuri kwa lengo la kumuepushia na madhara ambayo yanaweza kumpata,” alisema Simbachawene.
Matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika baadhi ya mikoa na wilaya, na Simbachawene amesema huenda wengi wao hawafahamu sheria zilizopo.
Waziri Simbachawene alisema kazi ya wakuu wa mikoa ni kusimamia ulinzi, usalama na amani katika maeneo hayo, huku wakiwajibika pia katika serikali za mitaa, kuangalia na kusimamia mali za umma.
Alisema kwa upande wa wakuu wa wilaya, kazi yao kubwa ni kuhoji jambo ambalo halijasimamiwa kisheria, huo ukiwa wajibu wao ikiwa ni utekelezaji kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande mwingine, Simbachawene alisema kwa miaka mingi wananchi walikuwa wakiipigia kelele serikali kwa kutowachukulia sheria watumishi ambao hawaenendi na maadili ya kazi zao.
“Lakini baada ya serikali ya awamu ya tano kuanza kuwachukulia hatua watumishi wasio waadilifu, wananchi hao hao wameanza kugeuka na kuilaumu serikali," alisema.
"Lazima hapa tuangalie pande zote mbili.”
Baadhi ya wakuu wa wilaya wa serikali ya awamu ya tano, wamekuwa wakilalamikiwa kwa kutumia mamlaka yao kuwaweka mahabusu watumishi wa serikali hususani waganga wakuu, wauguzi na walimu kwa madai ya kulalamikiwa na wananchi maneno yao ya kazi.
Chanzo: Nipashe