Wazili makame mbarawa umewasaliti wana ttcl

WAPOMA

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
689
175
:A S-baby:Kwa mdomo wako wewe mwenyewe na bwebwe nyingi uliongelea kwa kirefu matatizo yanayoikabili TTCL na ulitamka bila kusita kuwa uongozi unachangia na ukawataja kwa vyeo nafasi mbili ndani ya TTCL ambazo ni tatizo kwa TTCL kusonga mbele na AHADI yako ya kwanza kwa wana TTCL katika mikoa karibia yote uliyotembelea ilikuwa kuwapatia CEO mpya kabla ya April walichosahau kuuliza na wewe ukasahau kutamka ni mwaka gani;April imepita mpaka leo Desemba bado kimya, Hakika umewasaliti wana TTCL.Kijana January Makamba mkumbushe ahadi aliyotoa na mwambie kuwa TTCL kuendelea kuongozwa na viongozi wasiofaa inazidi kudidima.:israel:


[h=3]Makamba afumua menejimenti TTCL[/h]Na Mariam Mziwanda

NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameahidi kufumua uongozi uliopo katika Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kutokana na shutuma za ubadhirifu yakiwemo matumizi mabaya ya uongozi.


Makamba aliyasema hayo Dar es Salaam jana mara baada ya kupokea ripoti kutoka kwa wafanyakazi wa shirika hilo zilizoeleza vitendo viovu vinavyofanywa na viongozi wa shirika katika kuhujumu mali za umma.

Alisema kuwa, mbali na mikakati ya Serikali iliyopo kulipatia viongozi madhubuti shirika hilo pia amewasiliana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kuwachukulia hatua viongozi wanaohusika na ubadhirifu huo.

"Mimi kama raia na kiongozi nimetoa taarifa TAKUKURU tayari, imekua bahati kwangu leo nimepokea ripoti za wafanyakazi ambazo zina vielelezo vya kutosha juu ya tuhuma za viongozi ambao ni wabadhirifu na wana matumizi mabaya ya uongozi hii itarahisisha zaidi uchunguzi na sheria kuweza kutumika,"alisema.

Aliongeza kuwa, juhudi hizo zitakwenda sambamba na kuhakikisha hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamni viongozi hao zinafikiwa hivyo amewataka wafanyakazi wengine wenye vielelezo waunge mkono kwa maslahi ya taifa.

Makamba alidai kusikitishwa na udhaifu wa uongozi uliopo katika shirika hilo ambao unajieleza kuwa hakuna heshima wala staha ya shirika hivyo kufananisha mfumo wa kazi baina ya viongozi na watumishi kuwa sawa na makuli bandarini.

Alisema, Serikali ina wajibu wa kuona shirika hilo linarudi katika mfumo bora wa mashirika ya umma hivyo ni lazima mabadiliko hayo ya uongozi yaende sambamba na nafasi hizo kutangazwa ili kupata uongozi wenye sifa na imara hatimaye shirika liweze kurudisha hadhi na kuaminika.

"Kwa hali iliyopo sasa shirika ni baya na imefikia sasa haliwezi hata kukopesheka, hivyo tunatambua mtaji uliopo ni mdogo.

"Lakini kwa harufu ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya uongozi tumesitisha hata kutoa dhamana mpaka pale litakapokaa sawa na kuweza kuamika ili liweze kukopesheka," alisema Makamba.

Alisema, mabadiliko hayo yatakwenda sambamba na Serikali kulitoa shirika hilo katika ubia na Kampuni ya Airtel ili kuongeza nguvu ya ufanisi na uhuru wa maslahi ya shirika hilo.

Makamba alieleza harakati hizo za kuondokana na ushiriki wa Airtel katika ubia na TTCL zinasubiri maamuzi ya Msajili wa Azina ili kuweza kulipa tathimini ya thamani ya ushiriki.

Pia aliitaka bodi ya shirika hilo kukutana mapema wiki hii na kutoa taarifa kwa CAG ili aweze kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za shirika huku akiitaka bodi hiyo pia kuhakikisha inawapumzisha viongozi waliopo ili kuruhusu uchunguzi huru.

Makamba alimtaka Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Said Amir Said kuhakikisha hakuna mfanyakazi anayeonewa kwa utendaji wake wa kazi hasa kuwajibishwa kwa kuhamishwa kituo ili kuruhusu ubadhirifu wa mabilioni ya fedha kuendelea.

Pia alielezea kusikitishwa na hali mbaya iliyopo TTCL ya kukosa hata dola 2,000 za kuunganisha wateja huku wizi wa mikonga ya simu na mitambo ukiendelea.

Awali wafanyakazi wa shirika hilo wakiongozwa na Lucas Ishengoma walimueleza Naibu waziri huyo mchezo mchafu uliopo hasa Kanda ya Kaskazini, Dar es Salaam ambapo viongozi wamekuwa wakifanya watakavyo.

"Tunaelewa fika kuwa bajeti ya shirika letu ni sawa na mbwa asiyebweka, kwani inaongozwa na matakawa ya viongozi na sasa hivi kwa kuwa Kanda ya Kaskazini tukiongozwa na meneja tunaonekana tunafuatilia sana mapato na matumizi na tunaonekana tunakiherehere cha utendaji wa kazi.

"Tayari taarifa za meneja kuhamishiwa Mwanza tunazo ili aletwe rafiki wa mabosi, wale vizuri, lakini tunachosema tumechoka huyo mnayemleta hatumtaki kakaeni naye makao makuu,"alisema

Walisema kuwa, wakati uliopo hauna tofauti na ukoloni wa Mwarabu ndani ya shirika hilo kwani kazi ya uongozi ni kupitisha mikataba hewa ambayo haina maslahi kwa taifa huku wakiomba mapato ya mkongo wa taifa wa mawasilaino ambayo hayawafikii.

Naye Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Said Amir Said aliwaeleza wafanyakazi hao kuwa mabadiliko yoyote yatakayofanywa na Serikali watayapokea hivyo ni vyema mchakato kuanza mapema.
Makamba ataka TTCL ichunguzwe


na Waandishi wetu


Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknoloji, January Makamba, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuichunguza Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Makamba alitoa agizo hilo jana baada ya kukutana na wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao waliwasilisha matatizo, changamoto na kuwataja hadharani watu wanaoihujumu kampuni hiyo ikiwemo menejimenti.
Alisema endapo yaliyosemwa na wafanyakazi yatabainika kuwa ni ya kweli, hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwaburuza mahakamani.
"Hawa ni wa kufungwa pingu si wa kuwalea, ni lazima wawajibishwe kama ni kweli kuna watu wanaihujumu kampuni kwa kiasi hiki na mimi taarifa nilikuwa nazipata siku nyingi na wafanyakazi waliniomba nikutane nao ili wanielezee shida zao," alisema.
Aliongeza kuwa kutokana na mazingira yaliyopo kwa sasa katika kampuni hiyo hatoshangaa kuona kwamba bodi inakataa kupitisha uamuzi wa kufanyiwa ukaguzi ndani ya kampuni hiyo.
Aidha alisema kuwa anatarajia kuvunja uongozi mzima wa kampuni hiyo na kuweka mpya huku akielezea pia uchunguzi utakaofanyika utategemeana na maamuzi ya bodi ambayo atakutana nayo keshokutwa.
Awali wafanyakazi wakiwakilishwa na Lucas Ishengoma, walisema walikusanya sh bilioni 79.9 katika ofisi ya Dar es Salaam, Mkoa wa Kusini, lakini sh bilioni tatu hazikuonekana na kwamba zimetafunwa na wajanja.
"Kila mwezi tunafanya majumuisho na tulipata sh bilioni 7.9 Dar es Salaam, Mkoa wa Kusini, tulipotaka kujua fedha ziko wapi uongozi ukawa unatisha watu kuhamishwa na kuwabambikia kesi. Hii ni hatari waziri, ingilia kati," alisema.
Alisema wanataka kubadilishiwa meneja wao Karim Babhia kupelekwa Mkoa wa Mwanza kutokana na kuhoji fedha zilipokwenda, kitendo alichoeleza kuwa ni cha unyonyaji.


Kijana Jnuary natumaini sasa umeyasikia mwenyewe,Mshauri huyo Mzanzibar ili mchukue hatua mapema ya kuikoa TTCL

MUNGU IBARIKI TTCL.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,348
3,080
TTCL inahujumiwa kweli kweli, viongozi wa TTCL wapo kwenye pay roll za makampuni mengine ya simu
 

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,681
7,245
:A S-baby:Kwa mdomo wako wewe mwenyewe na bwebwe nyingi uliongelea kwa kirefu matatizo yanayoikabili TTCL na ulitamka bila kusita kuwa uongozi unachangia na ukawataja kwa vyeo nafasi mbili ndani ya TTCL ambazo ni tatizo kwa TTCL kusonga mbele na AHADI yako ya kwanza kwa wana TTCL katika mikoa karibia yote uliyotembelea ilikuwa kuwapatia CEO mpya kabla ya April walichosahau kuuliza na wewe ukasahau kutamka ni mwaka gani;April imepita mpaka leo Desemba bado kimya, Hakika umewasaliti wana TTCL.Kijana January Makamba mkumbushe ahadi aliyotoa na mwambie kuwa TTCL kuendelea kuongozwa na viongozi wasiofaa inazidi kudidima.:israel:

Mkuu punguza jazba. Tatizo sio CEO. Chunguza utabaini
 

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,382
1,343
Na wewe ndugu yangu unafikiri Tanzania bila kujuana inawezekana, mheshimiwa waziri Makame Mbarawa ni Mzanzibari pure na pia huyo CEO wa TTCL ambae alianza kwa kukaimu ni Mzanzibari so it will take ages and ages for sure kumtoa huyo ndugu yake kwenye power just trust me. Maana huyo jamaa CEO alikuwa meneja wa TTCL- Mbeya then enzi zile Dk. Maua Daftari ni naibu waziri wa mawasiliano ndo akampa shavu jamaa kuja kuwa CEO wa TTCL akitokea kwenye nafasi ya menaja wa mkoa sasa ndo hapo utashangaa sana kwamba ndani ya TTCL kweli alikosekana mtu mpaka ikabidi wampatie jamaa aliekuwa meneja wa TTCL wa mkoa, du so sad but that is how we work and all you need is to be patient baaaaaaaaaaaaaaasi
 

hetu

Senior Member
Jun 21, 2010
109
28
tatizo la ttcl ni uongozi, na hii inaanzia kwa CEO. Kwasababu ameshindwa kusimamia uongozi wachini. mameneja wa mikoa wamelala maofisini badala ya kufuatilia utendaji wa wafanyakazi walio choni yao.
mfano halisi ni mimi mwenyewe, niliomba kufungiwa TTCL broadband internet ofisini kwangu ni wiki sita sasa toka nilopie na bado sijafungiwa. nilipolipia walinipatia vifaa vyote lakini kuunganishiwa internet imekuwa shida, kilasiku ni danadana. mara fundi hayupo mara tunakuja kukufungia lakini hawafiki.
Sasa katika dunia hii ya ushindani wakibiashara unategemea shirika litakua kweli?.
Shirika bado liko usingizini, wanafikiri bado wako pekeyao. TTCL inahitaji mageuzi makubwa ya kiuongozi.
 

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,359
2,329
Wazili or Waziri? Turekebishie hapo ili tuchangie accordingly
mbona Mbarawa hukuandika Mbalawa??
 

Dash

Member
Jan 10, 2008
24
10
Juzi nimeona Mheshimiwa waziri akipokea msaada wa computer na dola elfu kumi kutoka Huawei, sasa kweli jamani hawa jamaa wa kichina wakitaka kazi hapo TTCL uongozi wa TTCL utaweza kweli kuwakatalia kitu hawa jamaa wakati waziri amefadhiliwa kwenye jimbo lake huko Pemba? Kwenye nchi zingine hili jambo lisingewezekana, lakini naona bongo hapa bila hata aibu waziri anafadhiliwa na suppliers katika sekta anayoiratibu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom