Wazee Washutumu Wanasiasa Kuvuruga Amani Tarime. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee Washutumu Wanasiasa Kuvuruga Amani Tarime.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Jun 10, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wazee Washutumu Wanasiasa Kuvuruga Amani Tarime.
  Imeandikwa na Samson Chacha, Tarime.

  WAZEE wa mila kutoka koo 13 za Kabila la Wakurya wilayani Tarime wameshutumu kile walichosema kitendo cha baadhi ya viongozi wa kisiasa kuingia wilayani humo kuchochea vurugu na kuondoka wakiwaacha wananchi wakivurugana kwa misingi ya kisiasa.

  Wamelaani na kukemea kitendo cha vijana wa Nyamongo kumshambulia Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine na Mwenyekiti wa Halmashauri, Amosi Sagara walipokwenda kuwafariji wafiwa katika msiba wa watu waliouawa kutokana na uvamizi wa Mgodi wa North Mara.

  Wakiwa chini ya Mwenyekiti , Sinda Nyangore na viongozi wa dini wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania Dayosisi ya Kati Dodoma , wazee hao wapatao 50 waliwaonya viongozi wa vyama vya siasa hususani wa upinzani wanaotoka nje ya wilaya kwenda Tarime kuchochea vurugu.

  Tamko hilo lilitolewa juzi katika kikao cha pamoja cha wazee hao kilichofanyika mjini hapa. Kilihudhuriwa pia na Mratibu wa Mila wa Koo hizo, Enock Chambiri, Katibu Msaidizi wa wazee, Moris Mongosi na Askofu Amos Mhagachi.

  Katika tamko lao walishutumu kitendo cha baadhi ya viongozi wa kisiasa kuingia wilayani humo kuchochea vurugu na kuondoka wakiwaacha wananchi wakivurugana kwa misingi ya kisiasa.

  Walisema hali hiyo imekuwa ikisababisha wananchi kutumia muda mwingi wakizozana kisiasa badala ya kufanya Maendeleo .

  “Kwani wakati wa Siasa umekwisha na viongozi wa vyama vya Siasa wasipewe vibali vya mikutano na maandamano Tarime,” ilisema sehemu ya tamko hilo.

  “Hawa wenzetu wa vyama vya upinzani kutoka Singida , Arusha na kwingineko wanakuja kufanyia mazoezi ya uchochezi kwetu hapa Tarime , kwa nini wasiyafanyie kwao kwani hakuna machimbo ya madini ,” alihoji Chambiri.

  Askofu Mhagachi katika kikao hicho alisema kuwa "Watu Waovu wakishika Madaraka Amani inatoweka ,tujihadhari sana na wachochezi hao wanaotoka nje ya wilaya kwa kisingizio cha vyama vya siasa, vyama hivyo vinatakiwa kuhubiri amani na kushindana katika hoja za kuleta maendeleo wala sio kuleta uchochezi kwa kabila la Wakurya Tarime”.

  Aliendelea kusema, “Hata Kanisani na Misikitini tunahubiri amani kwa watu wote. Hatuhubiri uchochezi kwa watu.Bila amani hakuna maendeleo”.

  Miongoni mwa mambo waliyoyaomba yatekelezwe na Serikali ni pamoja na kuwatengea wachimbaji wadogo wa dhahabu maeneo yao katika eneo la Nyamongo ili kupunguza matatizo ambayo yamekuwa yakijitokeza katika Mgodi wa North Mara unaomilikiwa na Barrick Afrika ikiwa ni pamoja na kuvamiwa mara kwa mara.

  Wazee hao wameomba pia wawekezaji katika mgodi huo kufanya vikao vya pamoja na wananchi vijiji vinavyouzunguka na kuwapa kipaumbele vijana wa maeneo hayo ili kupunguza malalamiko.

  Swali:
  Mauaji ya Nyamongo nayo yalisababishwa na viongozi wa Siasa!?
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  hahahahahahahahaahaha Bishop Muhagachi at work!!!!!!!!!!!!!! hawa wazee hawawezi kushawishi uma kuwa wanasiasa ndo walifanya mauaji nYamongo kutelekeza maiti na kurundika vijana wengi ndani hapo Tarime. Mhagachi anatekeleza aliyotumwa na best yake yaani mkulu wa nchi hakuna la ziada. Ikumbukwe kuwa haya si mauaji ya kwanza wala fujo za kwanza kutokea Nyamongo na Tarime kwa ujumla, wasitake kutwambia kuwa yale maji ya mto Tigiti yaliwekwa kemikali na wanasiasa. Hawa wazee kabla ya kufanya mradi huu wa Mhagachi na best yake wana mengi ya kuwaeleza wanaTarime na watanzania kwa ujumla. NIgemshauri Askofu huyo afanye kazi aliyoitiwa badala ya kutumikishwa for the sake of friendship huku ndugu zake wakiwa hawana matumaini ya kesho.
   
 3. mbasajohn

  mbasajohn JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hahahaha politics is politics lakn kama wazee nao wanakuwa politician ths is unbelievable! 2we wakwel jaman wanasiasa walikuja baada ya mauaji na vngnevyo sasa uksema wapinzan wamesababisha mauaji huu n uongo!
   
 4. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,977
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  Wengeenda kwenye mkutano bila t-shirt za yanga na kofia za chagua kikwete ningewaelewa.isitoshe hamna hata mzee mmoja nlieona akiongea.nlichoona walikua wamekaa kwenye kochi nyuma kumepambwa kitambaa cha rangi za njano na kijani.huku wakimsikiliza Mhagachi akisoma maandishi.lakini huyu mhagachi nashangaa hakuwakusanya wazee kulaani kemikali zilizomwagwa kwenye vyanzo vya maji wala mauaji ya wapigania haki.kazi kwelikweli.Kusimamia mazishi ndo vurugu?aibu yenu ccm.
   
Loading...