Wazee wailaumu serikali maisha yao kuwa duni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wailaumu serikali maisha yao kuwa duni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Oct 3, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wazee nchini wamesema serikali haijawa na nia ya dhati ya kushughulikia changamoto zinazowakabili, hivyo wametaka itungwe sheria itakayosimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Wazee.

  Walisema hayo jana katika risala yao kwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, ambayo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza yakiongozwa na kaulimbiu isemayo: "Maisha Marefu Hujenga Mustakabali wa Taifa Letu."

  Akisoma risala hiyo kwa niaba ya wazee wenzake, Theresia Mehela, alisema ikiwa ni miaka 51 tangu uhuru wa Tanganyika, miaka tisa tangu kutungwa kwa Sera ya Taifa ya Wazee na miaka saba tangu kubuniwa kwa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (Mkukuta), maisha ya wazee yameendelea kuwa duni.

  Alisema pia hadi sasa hakuna takwimu sahihi za idadi ya wazee na wengi wanapoteza maisha kwa kukosa chakula, makazi bora na matibabu na kwamba, japokuwa ipo sera inayoelekeza wazee kupatiwa matibabu bila malipo, hospitali nyingi zimeshindwa kuheshimu.

  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, alisema serikali imekwishaandaa muswada wa sheria ya wazee na kwamba, unatarajiwa kuwasilishwa bungeni Aprili, mwakani kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa kuwa sheria kamili.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira, ambaye alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete, alisema Sera ya Taifa ya Wazee ni waraka wa kwanza unaoonyesha nia ya kushughulikia kero zao, hivyo kinachotakiwa ni kwa mamlaka zinazohusika kuitekeleza.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,308
  Trophy Points: 280
  hawa si ndio wazee wa wanaotumika kulaani mabadiriko nchini? kumbe wameachwa haha wakawaulize wenzao wa east africa kama huwa wanasikilizwa wao waendelee kuwatumikia ccm tu na si vinginevyo

  Mabadiriko ndio yatakayowasaidia
   
 3. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,155
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wasinyamaze, mi wananiboa sana, si hawahawa ndo wanasema kuwa wao wamekunywa maji ya bendera ya kijani, sasa wanalalamika nini si waendelee kunywa maji ya bendera ya kijani tu
   
 4. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hawa ndiyo walikuwa wakijinadi kuwa ni mtaji wa kuwaweka CCM madarakani, sasa wameachwa wanaanza kupiga mayoe. Wale wazee wa East Africa waliotelekezwa walifikiri wanaigiza move.
   
 5. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Kwani maraisi toka chama Dhaifu huongea nao nini?Afadhali Nyerere chini ya ustawi wa jamii aliwawekea nyumba za wazee marais waliofuatia hawakuendeleza kitu.

  Hivyo vizee zikipewa pilau na soda , na kumwona rais thaifu hupagawa hadi kushindwa mwambia shida zao.Sasa nani atawasaidia?
   
 6. M

  MR.PRESIDENT Member

  #6
  Oct 3, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ndio maana huwa nawaonea huruma hawa vijana wa ccm wa sasa maana baadae watalia kama hao wazee.Kama mkapa analalamika kuwa wastaafu wamesahaurike sembuse hao wazee.Akipandacho mtu ndicho atakachovuna
   
Loading...