Wazee wa Iyunga Technical school Secondary kabla ya 2003

Wazee wa Iyunga Technical school Secondary kabla ya 2003

Madumbikaya

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2018
Posts
734
Reaction score
2,272
Enzi hizo Iyunga ilikuwa kama kambi ya JESHI. Viongozi wa shule waliitwa Rais na Mawaziri

Kura ilipigwa kwa Rais tu, Na Rais aliunda Baraza la mawaziri. Hakukuwa na neno kiranja yaani Prefect Iyunga secondary miaka kabla ya 2003.

Viongozi waliishi eneo linaitwa Ikulu au State House. Viongozi wa wanafunzi walikuwa Kama wafalme shuleni zaidi ya walimu.

Kidato cha kwanza ukipangiwa ilikuwa ni Mateso na shida kali wakati huo, Kila jina na Mateso utapata na kuitwa.

Maneno kama Nyoka, Salamander, Kenge na mijusi ilikuwa ni majina ya form one.

Utaitwa wewe Kenge kachote maji ni kawaida kwa form one.

Watu walikuwa wakakamavu muda wote.

Kulikuwa na wahuni wengi lakini pia kulijaa wenye akili sana.

Wanafunzi waliwaza Division one kuliko kitu chochote, Sifa ilikuwa ni kupata Division one.

Shule ilikuwa na walimu wengi mpaka kero, Kwenda ofisini tu kwa walimu unaogopa maana ulienda lazima utafutiwe sababu upigwe fimbo tu za Usafi au kufeli darasani.

Kwa mwaka kulikuwa na siku maalumu ikiitwa Assessment Day, Na hii ni siku ya ukaguzi kwa wanafunzi kitaaluma na nidhamu, Mwanafunzi anapita mbele kwa walimu zaidi ya 100 akihojiwa maswali na kila mwalimu kuongea anachokijua kwa mwanafunzi huyo kibaya au kizuri.

Mazingira ya shule yalikuwa mazuri Sana, kulikuwa na kumbi za kututosha na viwanja vya michezo vya kutosheleza mahitaji yetu, Swimming Pool na Basketball ground.

Nakumbuka majina ya mabweni wakati huo kama Amri Abed, Lumumba, Shaban Robert, Kawawa, Luthuli, Mugabe.

Ufundi wengi tulijifunza siku ya ijumaa Ilikuwa ijumaa ya Furaha sana, Tulishinda karakana na siku ilikuwa fupi sana sana.

Migomo ilikuwa sehemu ya maisha na vurugu, Muundo wa uongozi wa wanafunzi ukaja kubadilishwa kutokana na fujo hivyo wakaanza kutumia viranja.

Hakika Iyunga ilifanya tujiamini na kutoogopa mtu.

Nilishiriki Migomo yote na Fujo zote pale Iyunga Secondary ingawa Mimi ni miongoni wa wale tuliotandika Division one chini ya Point 11 pale Iyunga secondary.

Ni moja kati ya sehemu zilizonifurahisha maishani, Life was real Good, Kila siku lazima usikie Vituko na kituko Iyunga.

All the days we were Happy
 
Acha kuishusha hadhi Iyunga kwa kuiita sekondari. Iyunga ni shule ya Ufundi. Ni Iyunga technical school. Iyunga ina hadhi sawa na law school 😀😀😀
 
Mkuu daa uliyosema yote kweli kabisa, Mimi nilitoka hapo 2002 hakika ileilikuwa kambi ya jeshi.
 
Back
Top Bottom