Jana nilitaka kupost thread kama hii ila kwa mtazamo tofauti kidogo. Kwakuwa umeileta, nitaongezea maana hatutofautiani sana. Nina maswali machache yakuongezea
Hivi wanawapataje hao wazee? Tunapowaita wazee wa Dar, tunawapataje? Dar yenye wakazi karibu 5mil, hao ndio wazee wa Dsm? Nini kigezo cha kuwaalika kwenye mkutano wa rais? Nani anawaalika?
Hao wazee ni kweli wanawakilisha wakazi wa dar? Are they truly representing or the true color for dsm elders. Au wanaaiaisha wenzao?
Kwa hoja alizokuwa nazo rais, ilikuwa sahihi kuzungumza na wazee? Ilikuwa sahihi kweli kuzungumza na taifa kupitia "wazee wa dsm" kwa hoja alizokuwa nazo. Ujumbe umefika kwa njia sahihi? Yaani, rais amefanikiwa kuufikisha ujumbe wake kwa njia ya kuzungumza na wazee wale?
Utaratibu wa rais kuzungumza na taifa kupitia kundi moja tu la jamii kwa kila anapotaka kuzungumza ni sahihi? Kuna wakati anatakiwa kuzungumza na makundi mengine pia anapolihutubia taifa kulingana na hoja alizonazo?
Vipi kuhusu wazee wa maeneo mengine ya nchi? Au ni wazee wa Ddm na Dsm tu? Hao wazee wamaeneo mengine wanajisikiaje?
Naomba kuwasilisha.
..