Wazee wa CCM na mustakabali wa chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wa CCM na mustakabali wa chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by opportunist2012, Mar 29, 2012.

 1. o

  opportunist2012 Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninaunga mkono moja kwa moja maneno ya wazee wa CCM akina mzee Kitime,Kaduma na Butiku kuhusu mustakabali wa chama hiki tawala. Ni ukweli usiopingika chama hiki kinaenda kinyume na itikadi zaHayati Baba wa Taifa,mwalimu Julius K.nyerere.Chama hiki kila kukicha kinazidi kupoteza muelekeo.

  Ufisadi na kila aina ya rushwa ndio msingi wa chama hiki.Huwezi kugombea ubunge mpaka uwe na pesa nyingi.Chama hiki kinafumbia macho vitendo vya ubaguzi.

  Hali ya ubaguzi wanaofanyiwa walimu wasio wazawa manispaa ya Bukoba si ya kuvumiliwa hata kidogo.Viongozi wanaotokana na chama tawala wanawalinda baadhi ya wakuu wa shule zilizopo Bukoba na afisa elimu sekondari wa manispaa ya Bukoba kuwanyanyasa na kuwabagua walimu wasio wazawa.

  Vitendo hivi vya ubaguzi viko waziwazi.Mkuu wa shule ya sekondari Kahororo ni kinara wa ubaguzi huu wa kiukabila.Hii si Tanzania aliyoihubiri Mwalimu Nyerere.Watanzania wanazidi kutokuwa na imani na CCM. Hali hii ikiendelea CCM itajichimbia kabuli lake mwenyewe.

  Maneno ya Nnape Nnauye ni ya kutapatapa,eti maneno ya wazee wa CCM wameyapokea na wanayafanyia kazi.Muda wote kwa nini wasiyafanyie kazi mpaka hawa wazee waliojawa na busara watoe kauli kali dhidi ya mustakabali wa CCM.
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kumbe na wewe ni wakala wa wakoloni walioiba utajiri wetu na kutuachia mashimo kule kwnye migodi ya dhahabu.shame on you
   
 3. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo watanzania wakipewa tshirt, khanga na kilo ya chumvi wanasahau haya matatizo yote. Bukoba unyesheni hasira zenu kupitia sanduku la kura!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ubaguzi wa makabila na maeneo ndiyo sera ya ccm, hata juzi Arumeru Kibajaji Lusinde amesema wazi kuwa Makabila hawatakiwi kuwepo Arumeru, akimsakama V.Nyerere kuwa anatafuta nini Arumeru wakati yeye ni mtu wa Musoma!
  Kwa hivo dawa ni kuachana na chama hiki cha kipagani kwa kutumia sanduku la kura!
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kati ya mwalim Nyerere,kaduma,,Dr kitine na Butiku nani mwenye uzalendo wa dhati?Mwali alikuwa tayari kurudisha kadi zake za chama.leo hawa wazee wana uwezo wa kufanya hivyo?leo wanazungumzia misingi ya chama huku wakiwatumia watoto wao na maagent wao kukibomoa chama ambacho wao ndio wamekifikisha hapo.hawa wazee ni wa kuwapuuza tu.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wazee hawa wana bahati ya kuwepo kwenye serikali zote Nne tangu ya mwalim hadi leo,kwa nini wasije na majibu ya matatizo badala yake wanakuwa walalamikaji??hii ndio maana ya uzee??
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kwanini hasa wasichukue uamuzi mgumu na wa kizalendo kama alivofanya mwalim Nyerere kurudisha kadi na kusema kuwa chama si mama yangu wala baba yangu,mbona wao wanasikika wakipiga makelele tu??
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ivi kina butiku na genge lake wanatoa fundisho gani au wasia gani kwa vijana wao waliowazaa ambao ndiyo wamefanya mabadiliko haya wanayoyalalamikia???????
   
 9. d

  dada jane JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tamuchungu mbona unasema mwenyewe tu.
   
 10. o

  opportunist2012 Member

  #10
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakati umefika kukipiga chini chama hiki cha mafisadi.Wenyewe kwa wenyewe wanapingana...chama kimepoteza diraa.CCM ni chama kilichosaliti Watanzania.......kila kukicha afadhali ya jana.Kuna kundi la watu wachache wanaofanya nchi hii kama yao...Watz tuungane kuondoa CCM madarakani tuache mazoea yanayotugharimu.
   
 11. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wataondoka,mwisho wao umefika.
   
 12. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni huo! Yupo mzee kati ya hao aliwahi kusema watanzania tuache kulalamika,je wao wanaifanyia nini CCM kama siyo kulalamika? Hivi hawawaoni wazee wenzao wa Zambia,Kenya[pentagon?],Mali,Ghana na kwingineko? Naomba wazee hawa washiriki ujenzi wa Tanzania tuitakayo kupitia chama kingine kwani kwa CCM hii ni kumpigia mbuzi GITAA.KARIBUNI WAZEE,HAMTAKUWA MUMEPOTEA!
   
Loading...