Wazee wa bagamoyo wafunguka!!!!!. -->-->--> chadema v

Karibu kwetu chadema,Karibuni Bagamoyo,
Pekeee ni chetu chama, kututuliza mioyo,
Kwa wababa na wamama, vilema na vibogoyo,
CCM ipate zama, dua yetu ndiyo hiyo.


Karibuni magomeni, wananchi tuwashike,
Awape nguvu manani, Chalinze yote mteke,
Mkoa wote wa pwani, Ngome kuu ijengeke,
Kuwa chama upinzani, CCM kigeuke.

Hiyo kwetu ni hedaya, CCM kuanguka,
Hatofurahi Jakaya, kuona tunafunguka,
Lakini jueni haya, tumechoka kupigika,
Pasina hofu na haya, Njooni tutawashika.

Karibu kamanda Mbowe, Karibu na wewe Sugu,
Mkaribie Mbwewe, Chole na Misugusugu,
CCM muing'owe, Mng'oe na zake mbegu,
Waingiwe na kiwewe, waanzilishi vurugu.

CDM Daima.

enzihuru tumesoma, utenzi ulotukuka,
na chadema wanasema, kweli wamefarijika,
bagamoyo si masama, ya ukanda ni kichaka,
hongereni bagamoyo, mnakuwa wakombozi.

msitishwe na nchemba, ni mufilisi kichwani,
yatumieni marimba, rizwani mpuuzeni,
chezeni hata sindimba, lau kama ya wangoni,
hongereni bagamoyo, mnakuwa wakombozi.

kalamu imenigomea, heri niweke kituo,
msitumie mmea, jema kuliita sio,
kiona baya kemea, sitingishie matao,
hongereni bagamoyo, mnakuwa wakombozi.
 
Last edited by a moderator:
Jipeni moyo nyinyi wafa maji, CCM haijawai kutetereka wala haija tetereka na haita tetereka. Tunaendelea na mambo ya kimaendeleo kwa waTanzania, siyo kupiga kelele kwenye mitaa ya watu, Tunamajukum mengi sana na hata nyinyi mnaojiita CHADEMA mnatutegemea kwenye huduma za jamii, ngoja tuhakikishe ustawi wa jamii kwanza.

Ushauri wabure,
mngeanza kuangalia majimbo yenu hali iliyopo kwa sasa na wapiga kura wenu wanavyojutia kujaribu kuchagua upinzani. Siyo kila kukicha mnazunguka kwenye maeneo ya watu wengine, majimboni kwenu hamna jipya hata kidogo.
ni kweli mkuu,ccm haijawaki kutetereka na ndo maana imeanza kujeruhi na hata kuua wapinzani kwa mikuki na mapanga. Kweli ccm ni janga la kitaifa!
 
Back
Top Bottom