mayenga
JF-Expert Member
- Sep 6, 2009
- 4,118
- 1,973
Ndugu zangu,
Nimejaribu kutafakari mwenendo wa wazee wa nchi hii,nami pasi na shaka lolote nasema kwamba,nyinyi ndo mmelifikisha pabaya taifa hili.
Taifa hili baada ya makubaliano ya pale Lancaster House,kijana na kiongozi wa kipindi hicho Mwalimu Nyerere alianza vema sana.Nyerere alikuja na Azimio la Arusha lililokuwa na miiko ya uongozi.Wazee mlioko sasa madarakani,mkaona ni vema kulizika Azimio hili.
Wazee mkiwa viongozi mkaanza kuuza nchi kwa mikataba ya Mangungo na Karl Peters.Wazee mkajimilikisha mashirika ya umma bila kuzingatia kuwa ni mali ya taifa.Wazee mkaua mitaala ya elimu,wazee mkaanza kujipa vyeo zaidi ya kimoja.
Wazee utamaduni wa nchi mkauharibu,mkaona soko huria lisilo kuwa na udhibiti ndo uhuru kamili.Wazee mkaingia kwenye biashara huku mkiwa madarakani na pale mlipoambiwa kutaja mali zenu mkawa waongo.
Wazee mkaruhusu tamaduni za kijinga.
Kumekuwepo na lawama nyingi kwa vijana,lakini uhalisia wa kuharibika kwa vijana na watoto,ni matokeo ya malezi yasiyo na tija.Katika suala la malezi,si wazee wa mjini tu,ila hata wa kule vijijini.Wazee mmebaki na kinga moja ya kujitetea ambayo ni WATOTO WA SIKU HIZI,hii imeleta athari kubwa katika maisha ya watoto.
Wazee mmekuwa wala rushwa wakubwa,na mmekuwa ndo watetezi wakubwa.Wazee mkiwa mpadarakani,mmeunda tume ambazo mmeishia kutozifanyia kazi.
Wazee ndo mmekuwa watu wa kulalamika.Ni wengi raia kwa uongozi wenu wametangulia kwa Mungu kabla ya siku zao.
Hata wazee mliostaafu,mmeshindwa kukemea ufisadi na ufedhuli wa mliowachia madaraka.Wazee mmezitelekeza ndoa zenu na kuwa mfano mbaya kwa watoto wenu.
Wazee mmekuwa kikwazo kwa maendeleo endelevu,mmejenga mtandao wa kirasimu katika ofisi zote za umma.Mmefanya maisha ya watu wa nchi hii kuzidi kuwa magumu.
Wazee mmezidi kuzalisha mbegu mbovu za vijana ambao ndo taifa la kesho la nchi hii.Vijana wote wenye madaraka na kazi nzuri,katika idara nyingi,wamekuwa wanaendesha mashirika, taasisi na idara hizo,kwa mgongo wenu ninyi ambao pengine mpo au mmekwishatoka madarakani.
Kwa kumalizia niwaambie tu wazee wa nchi hii kuwa mkumbuke kuwa,piga ua lazima maisha ya mtu yafike mwisho,uzee ni dalili za kufikia ukingo wa maisha.Mtakuwa na kibarua kwa Mungu kueleza ni kitu gani mmeifanyia nchi nzuri ya Tanzania.Utaulizwa kama uliitumikia vema na kama ulikemea ulipopaswa kufanya hivyo.