Wazee kupewa vyeo, je ni matokeo ya vijana kutojua nafasi na wajibu wao kwa taifa?

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
1,421
4,729
Leo hii vijana wengi wamegeuka kuwa wafuasi wa mawazo na mtazamo wa viongozi (chawa)
Wengi wao hawahoji hata kama wanaona hali si shwari, badala yake wanakubali kila jambo. Je, huenda hii ndio sababu ya kurudishwa kwa viongozi walewale waliowahi kutumikia taifa wakiwa vijana?
 
Hapana huenda wanahoji sana ktk vikao vya ndani ndomana wanaogopwa sana kupewa nafasi zauongozi, ndomana wanaweka wazee walewale ili waje kuwalinda nakuwapitisha watu wao hakuna namna la uchawa nalo nitatizo.
 
Hapana huenda wanahoji sana ktk vikao vya ndani ndomana wanaogopwa sana kupewa nafasi zauongozi, ndomana wanaweka wazee walewale ili waje kuwalinda nakuwapitisha watu wao hakuna namna la uchawa nalo nitatizo.
Nadhani umefika wakati sasa, kwenye hizi nafasi/ vyeo vya kisiasa kuwepo na ukomo wa umri. Ama sivyo vijana wengi wataendelea kukaa bench hasa kwenye nafasi za ngazi za juu.
Au ndio tusemebkwa sasa tz ina wazee wengi kuliko vijana?
 
Simply watakuwa wanaona vijana hawawezi kuwapa viongozi wa juu ushauri chanya, hasa kama mwenyekiti akiwa ameenda umri kidogo, basi ni vyema na makamu wake awe na umri wa kufanana nae ili waweze kuaminiana kwenye kushauriana mipango ya chama chao.

Naona kwa kijana itakuwa ngumu kuaminiwa kwasababu ya umri wake, hajapitia mengi, japo kwa upande wangu naona vijana wangepaswa kusogezwa karibu mapema ili waweze kuyamudu majukumu watakayopewa siku za mbeleni pale wazee watakapostaafu.
 
Vijana wengi ni chawa, hawana hekima, much know na wanataka mafanikio ya haraka.
Angalia tu vijana wengi waliopewa nafasi kwa sasa.
 
Back
Top Bottom