Wazazi wenzangu nishaurini

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Kwa kweli huuu ni mtihani kwangu tena karibu ya kushindwa

Mimi ni baba mwenye watoto 2 wa kiume yuko miaka 5 na wa kike mika 2

Baba mimi nakiri kua nawapenda sana wanangu kwa hali ya uwezo mungu alionijaalia ila ndugu zangu siku zote wananiona siitendei haki familia yamgu kwa kila ninalojitahidi dada zangu wanaona sivyo lawama kwangu ndio dira ya maisha yangu kila siku kutoka kwa familia yangu.

Leo saaa 2 na nusu dada kanipigia simu kua mke wangu hajaenda tulipopanga huku akiwa na mtoto anataka kupita nae majiani huku mukiwa na miti mikubwa kama miembe ambayo ni nyumba mzuri kwa mashetani mara watoto wanazurika dada huyo alipiga simu na kunishambulia haikunipa tabu nikaona wacha nitatue tatizo saaa 3 na nusu napigiwa tena simu naambiwa mi nimelala wakati mwanangu wa kiume hajaingia ndani yeye analala kwa bibi yake kwa vile nimepanga chumba 1 naye namuhisi ni mkubwa si vyema kulala nae chumbani nikatoka kuenda kumtafuta nimemkuta anaangalia tv maskani mtito ni peke yake nikaamua kumrudi kwa mikwaju kwa vile nimeshampa onyo mara nyingi nafika nae home madada wananifokea na kutaka kunipiga eti nimempiga vibaya mtoto.

Ikabidi ningurume kutuliza hasia wakaona nao naweza kuwashambulia nikaekejea home kulala

Kila siku nimekua sina jema nifanyejeeeee?
 
so, whats the problem now? hasira or what?... thread nzima nimesoma kwa mashaka na mang'amu ng'amu na machokomchuzi..
 
Umeandika kwa jazba yan umepanic sana haujaeleweka vizur fanya marekebisho upate ushauri vizuri
 
Kupiga mtoto ni kumfanya awe na nidhamu ya woga, usirudie tena...
 
Maelezo yako ni mengi lkn hieleweki vzr ila wewe kama baba huna msimamo na familia yako!mara dada ,mara wanataka kukupiga!da!kama uko kwako na mke na watoto wako hao dada wanatoka wapi?kama kuja kusalimia lazima kuwe na mipaka sii kuingilia utaratibu wa familia yako.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

anaonekana ni kijana mdogo, na kipato chake ni kidogo hivyo heshima inakuwa ndogo. aangalie sana na hao dada zake wasije kumuuza mkewe, maana wanaonekana ni mcharuko hasa!
 
Du...
Mi nahisi kama you are not serious na the way unavyoihandle familia yako... huna msimamo pia... muoga... hujiamini...
 


Kuna tatizo la manufacturer hapo soft ware zimewekwa ndipo sipo!!!!
 
Cha msingi jamani ninapomkataza mwanangu familia inaniingilia kwa kuona kua nawaonea watoto
 
Yaani dada zako wanakufokea wewe na kutaka kukupiga kwasababu umemchapa mtoto wako?Dada zako wana mamlaka juu ya mtoto wako kuliko wewe mzazi?Una umri gani mahirtwahir utake kupigwa na dada zako?
Mtoto hafunzwi kwa kuchapwa mahirtwahir,tena haswa mtoto mwenye umri wa miaka 5!!:embarassed2:Wewe kama mzazi unapaswa ujue jukumu lako juu ya mwanao.Kumbuka huyo ni mtoto,ameachiwa akawa macho mpaka usiku mwingi na si yeye wakumlaumu.Watoto wanategemea wazazi na walezi kama rolemodells/guides,na watoto hawana uwezo wa kujipangia rutine au kujua muda huu wa kulala,sisi kama wazazi ni jukumu letu kuwalea katika misingi bora,na nikimaanisha sio kuwalisha na kuwavisha tu bali pia kuwalaza on right time.Kwahio wewe baadala ya kumuangushia hasira mwanao ungepambana na hao walokuwa size yako kwanini wamemuacha mtoto macho late.Unamuonea tu malaika wa watu,hapo hajui hata alolikosa kaambulia kipigo tu.Hata mwanangu mie nisipomuhimiza alale hatolala na nakuhakikishia.
 

Safi sana mkuu ndio tofauti ya kulea na kukuza!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…