Wazazi wa Sasa/Baadaye Tunaweza kufanya Haya?

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,974
1,640
Natumaini wote mu wazima wa afya njema. Mie mzima kama jiwe nadunda maisha kwa raha zangu.

Nimewaza sana kulingana na hali ya maisha ya sasa na jinsi mambo yanavyendelea kubadilika nikaona ngoja niwaulize ili nijue ni kwa kiasi gani mambo yakienda na kubadilika. Issue ni kwamba baadhi ya wazazi walikuwa na tabia ya kuwalisha watoto wadogo chakula walichokuwa hawawezi kutafuna kwa kukitafuna kwanza wenyewe na kisha kukitema chakula hicho na kuwalisha watoto wao. Hili lilifanywa kwa baadhi ya vyakula km mahindi, mihogo au viazi vya kuchoma. Binafsi nilishaona baba yangu akiwafanyia hivyo wajuu zake-watoto wa dada zangu- ambao wengi wao sasa ni watu wazima wenye watoto. Ninachokiongelea hapa ni kama vile ndege anavyolisha makinda yake kwenye kiota.

Hilo ni moja, suala la pili nalo nimeona tuliongelee ni hili la wazazi kunyonya kamasi kutoka kwenye pua za mtoto, hasa iilipotokea mtoto alikuwa anasumbuliwa na mafua/makamasi na inakuwa vigumu kuyadhibiti. Wazazi wa zamani walikuwa wanaweka midomo kwenye pua ya mtoto na kuvuta kamasi kwa mtindo wa kunyonya kisha alitema nje. Ikumbukwe mengi ya haya yalikuwa yakitokea kati ya mwanzoni na mwishoni mwa miaka ya 70.

Inawezekaa likawa ni jambo geni miongoni mwa wengi wetu humu jamvini lakini nahisi wapo ambao waesikia au kuona haya mambo mawili nilioyaongelea.

Sasa naomba niwaulize wanaJF wenzangu, kama hukuwahi kuona au kusikia, hebu jiulize kama wewe unaweza kulifanya hilo sasa hivi? Ni wangapi kati yetu hasa wanaume, umeshawahi walau kumsafisha mwanao aliyejisaidia haja kubwa kama sio kumuita msaidizi wa nyumbani aje amsafishe mwanao? Na je kwa mtazamo wako unadhani wazazi walipokuwa wakifanya haya kwa watoto/wajukuu wao ilikuwa ni ulimbukeni wa kutojua madhara ya matendo haya au ilikuwa ishara ya upendo kwa vizazi vyao hivyo?

Tafakari na toa maoni yako!

Alamsiki.
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,772
23,076
mbele ya mtoto wako unafanya. Kama huna mtoto hujui uchungu wake unaweza sema hutothubutu. Ila sie wenye watoto tunajitoa kwa hali na mali
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,542
Mbona bado yanafanyika ndyoko?? hasa vijijini ambako kidogo hali bado haijawa nzuri. Mijini kumtafunia mtoto chakula kigumu wengi wanasaga na mablender; kunyonya mafua kuna macodril kila kona na watu wanayatumia. So sehemu kubwa ya wakazi wa mijini kwa sasa wanatumia njia za kisasa kuliko vijijini au kwenye familia za watu wasiojiweza.
 
Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,066
173
Sasa hv kutafuna na magonjwa haya ni baraaaaaaaaa.......... Zamani acha iwe zamani kulikuwa na raha yake. Enzi hizo mnakula ugali nyama mpo kwa mfano watano, kila mtu na kipande chake umekishikilia mkono wa kushoto mkono wa kulia ni tonge na kuchoveya kwenye bakuli/sahani moja mnayo-share wote......

Nakumbuka ktk ku-share bakuli/sahani, km siku mnakula samaki nlikua na uncle wangu mkono huo huo anaolia ndio analia samaki na mifupa inayotoka mdomoni anawekea mkono huo huo.... Nlikua nauzika na nlikua nashindwa mwambia maana MURA alikua MKARI mno.......

Ila ni uchaafu na magonjwa mengi sana kufanya hayo mambo now....
 
Thanx and understood!
 
Hiyo para ya kwanza uminifurahisha na kunikumbusha mbali masikini. Yaani hapa mbavu sina na machozi ya furaha kibao. Ngoja nchukue lesso njifute machozi mie!!!!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom