Wazazi wa kiafrika

Dejane

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
50,568
71,448
Hivi ni kwanini sisi tumelelewa kwa kuchapwa,kutishwa ,maneno makali
Ukikosea kitu utakalipiwa,,mzazi hawezi tu mwambia mtoto kwa utaratibu akaelewa?unajua hadi vizazi na vizazi vimerithi
Toka nilivyokua kukalipiwa sipendi kabisa
Yaan unakuta mzazi anamchapa mwanae hadi unasema hivii anafikiria nini,kuchapa nimkufundisha?
Ina maana na wenzetu huwakalipia sana watoto wao?
Aisee wazazi tubadilike tuachane na mambo ya kizamani mweleze tu mtoto atakuelewa vyema,sio kumtukana unamuharibu akili mtoto,
Kuna wamama wengine utakuta wanawatisha watoto wao kwa kusingizia baba yako mkali umevunja chupa utamjua leo yaan akija na ulale mapema,sasa hapo mtoto unakua unamuogopa baba unamuona kama adui hiv,,pia kuna zile familia baba akisikika tu sauti anakuja,watoto kama walikua sebuleni wote watakambilia chumbani hawataki kukutana kabisa na baba,kuna kina mama wengine wakali tu kutwa kucha ni kutukana matusi mtoto anayakariri kweli nae akikua hivyo hivyo anarithi
Jamani tubadilikee tuwalee watoti kwa upendo na nidham
Tusiwanyanyase watoto,tuwapende jamanii
 
kukaripia hiyo ni emotion hata wenzetu hufanya hivyo ili kutia mkazo ktk kile ukisemacho lkn wengine hupitiliza na kutukana another level kupiga!
wenzetu naona wanadili sana na emotion i mean wanaongea na mtoto kwa hisia hivyo huwavuta wtt pia kujua kile anachoambiwa kina umuhimu kiasi gani.
 
Mtoto ukimdekeza madhara yake makubwa.bora uwe mkali kidogo sio kupitiliza. Unakuta mtoto ambae hachapwi zaid ya kuonywa anakua na kiburi flani yaan anaweza kukuzaba kibao mbele ya wagen na ukabaki kusema "huyu mtoto jaman", lakin akijua fimbo ipo hawez fanya hivyo.
 
Jiulize kwanza kwanini waafrika pure wana nywele fupi na kichwa ndo kinahidhi akili. Halafu linganisha msitu mnene na msitu wenye nyasi fupi, upi ni productive.

Akili tunazo lakini hazina rutuba, so nguvu ya ziada inahitajika. For that case, viboko is a must.
 
Kumpiga na kumkaripia mtoto sio aina nzuri ya malezi...

Mtoto mkanye na kumuelewesha taratibu na kirafiki zaidi ataelewa

Wengine huenda mbali na kuwaita watoto wao mbwa kitu ambacho kinaharibu mtoto badala ya kumjenga
 
Kumpiga na kumkaripia mtoto sio aina nzuri ya malezi...

Mtoto mkanye na kumuelewesha taratibu na kirafiki zaidi ataelewa

Wengine huenda mbali na kuwaita watoto wao mbwa kitu ambacho kinaharibu mtoto badala ya kumjenga
Yaan kuna wazazi wana matusi wewe,mtoto atapewa kila aina ya jina ,sio vyema kabisa
 
Nivyema mtoto sissies mazingira ya aina zote maana kunawatoto wengine huwezi hata kukaanae huwezi kisa malezi akisemwa kidogo shida mara kazira Kula mara kagoma kutumwa hayo sio malezi binafsi nimechapwa sana tena sana lkn leo nimekua naona faida zake pia kunawenza walikua hawaguswi na mtu tumekua tofauti.........
 
Hata kimafanikio mtu aliepitia shida nyingi na alie zoea raha wanakua tofauti mtu alie piyia shida anakua na akili ya kukabiliana na changamoto kirahisi zaidi
 
Kumbe sisi wakishua ( mboga 7 )
Tumedeka vya kutosha hamna viboko kwanzia shule mpaka nyumbani...
 
Aisee ii kitu imenifanya nikae mbali na ndugu kisa nawapenda watoto wangu ati naambiwa nawadekeza nitakuja kuona baadae madhara ya kupenda watoto ivi ni kweli? Kupenda watoto na kuwajali ni kuaribu future yao? Kucheza na kuogesha watoto naambiwa nimekaliwa na mke aisee uu uafrica kuna saa nauchukia.
 
Mtt ili akuheshim kama mzaz lazma kipigo kitembee anapokosea

Mtt anapishana na babaake seblen amevaa kanga na chupi ndo malez hayo

Hebu.linganisha watt wa mjin na,wakijijin uone n gani wana heshima
 
Tatizo letu waafrika kwa kuwa wazungu wametutawala basi kila kitu wafanyacho sawa sio hivyo iga wanapopatia usiige wanapokosea sasa mtoto usimchape kwa nini anapokosea
 
Back
Top Bottom