osc michael
Member
- Sep 10, 2017
- 57
- 99
Kila mtu anataka ukweli lakini kila mtu hataki kuwa mwaminifu. Ni bora kumuandaa mtoto wa kike kuwa mama bora kuliko kumrekebisha mtu mzima.
Kitchen party ni siku ya kumrekebisha mtu mzima baada ya kushindwa kumuandaa mtoto wa kike kuwa mwanamke bora. Hii ni moja ya mpango mbovu ambao akina mama walibuni kupata zawadi kwa watoto wao.
Familia zetu nyingi tunawaandaa dada wa kazi kuwa wanawake bora kwenye ndoa zao na kuwafuga watoto wetu wa kike kuwa wanawake dhaifu kwenye ndoa zao kwa kutegemea kitchen party kuwaanda kuwa wanawake kwa siku moja.
Jiulize wakat wa COVID-19 mtoto wa kike wa umri wa miaka 9 ,anapikiwa na binti wa kazi wa miaka 15,anafuliwa, anaamshwa kisha anaonyoshewa nguo, anatandikiwa kitanda, anawekewa sukari kwenye chai na mwenzie mwenye miaka 15, Baba una chati na mama unachati na simu.
Maisha ni fumbo na upofu wa fikira,umetunyima kuona fursa ya kuwapa majukumu watoto wetu wa kike wangali wadogo kufanya majukumu yao kuwaandaa kuwa wanawake bora .
Mwanaume mwenye maono uhitaji mwanamke mwenye ndoto ili kuwa na familia yenye afya,mtoto wa kike kwenye familia ya Baba msomi na mama msomi kazi ngumu anayofanya ni kuomba pesa ya swimming pekee.
Siku 1 Nikiwa Kipengere Njombe,macho yangu yanaaona mtoto wa miaka 9 amebeba mtoto mgongoni, anaanika Ngano ,anatwanga kwenye kinu,kisha anapepeta Ngano kusaga kwenye jiwe (Lwila)na kupika ugali
Moyo wangu uliganda kwa furaha kwa hili somo ambalo nallipata sababu ni elimu kubwa ambayo naipata bila gharama.
Watoto wetu wengi wa kiume tunawalea kama mifugo ndio maana baadhi yao wana mauimbile ya kike na ni watoto wa kiume,wanavaa nguo za kubana kama wanawake,hakuna anayejali kila mtu yupo busy kutafuta pesa na sio kumuandaa mtoto wa kiume kuwa Baba bora.
Pesa ambazo tunazitafuta leo ndio tutakazo zitumia kumrekebisha watoto wetu baadaye ,sababu tuna elimu nzuri ila hatuna maarifa ya malezi mazuri..
Hatujifunzi malezi sababu hatuna upendo na ushirika,ndugu mwenye pesa ambaye hana falsfa nzuri ya malezi anamdharau ndugu asiye na pesa mwenye falsafa nzuri ya malezi.
Mtoto wa ndugu asiye na pesa mwenye genge la chakula ambalo anauza binti wa miaka 12 ,anajua bei ya nyanya,kitunguu,limao,kilo ya mchele na kilo ya nyama ,Mungu huweka baraka kwenye kichwa cha huyu binti ja kuja kuwa mama bora sababu ya Vitendo na Tabia za mke kuanza kuzifanya katika umri mdogo.
Mwanao anasoma English Medium umri wa miaka 15,hajui hata kupika chai wala kuhesabu siku zake ,wala bei ya nyanya ila kwenye kitchen party ataambiwa haya yote,kuna haja ya kubadili muundo wetu wa malezi na ukaribu na watoto.
Tujiulize kwa nini tunashindwa endeleza urithi wa mali tunazoachiwa?Sababu ni moja pekee mwanao unamuacha nyumbani anacheza video game na mfanyakazi ,mfanyakazi ndiye anayejua kila kitu kuhusu biashara yako na mwanao anakuwa beast kwenye ps siku ukilala usingizi wa Milele mwenye ujuzi wa Ps hawezi endeleza biashara.
Humkomoi house girl bali unamuandaa kuwa mama bora na mke mwema na mwanao unamundaa kuwa mama asiyena na majukumu na mke mjinga, hatupaswi kufuga watoto wa kiume kwa kuwanunulia skin jeans,kuwaacha kwenye sofa na kuita mtu akuoshee gari wakati una mtoto wa kiume wa miaka 15.
NB.Pesa ni kila kitu na kila kitu kinahitaji pesa ila pesa haiwezi kukupa kila kitu..tuanze kuwaandaa watoto bora sio kuwarekebisha watu wazima. Imani yangu mmejifunza