GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Kwa takribani muda wa siku tatu ( 3 ) zilizopita nilibahatika kufanya ziara zangu za Kikazi na Kiutafiti hasa katika Shule za awali ( Kindergarten schools ) na hizi za Msingi ( Primary schools ) nikiwa katika dhana nzima ya kutaka kujua changamoto kubwa ambazo zinawakabili Walimu wa sasa wanaowafundisha Watoto wetu ili nionanishe na changamoto ambazo zilikuwa zikiwakumba Walimu wa zamani ambao pengine baadhi kama siyo wengi wetu humu ( I inclusive ) tulibahatika kufundishwa nao.
Nashukuru sana niliweza kutembelea Shule kadhaa za Wilaya zote tatu za jijini Dar es Salaam nikianza na ya Temeke, Ilala na kumalizia na yangu inayonihusu kindaki ndaki ya Kinondoni na kupewa ushirikiano mkubwa sana kwa niliobahatika kuonana nao na kufanya nao mazungumzo ya Kitaaluma.
Nilichokipata kutoka huko kote ni kwamba japokuwa Walimu wa sasa wana changamoto nyingi ila kilio chao kikubwa walikipeleka kwa sisi Wazazi huku wengi wao wakisema haya maneno ambayo nitayanukuu.....".
Ndugu Mtafiti GENTAMYCINE sisi Walimu wa hapa... Eneo la Temeke tunapata changamoto kubwa mno kwani karibia 90% ya Watoto / Wanafunzi wanaokuja kuanza kusoma hapa wana tatizo sana la kuelewa kile tunachowafundisha na huwezi amini tunajitahidi kadri ya uwezo wetu lakini wana uelewa mzito sana na inaonekana tatizo hili ni hereditary kutoka kwa Wazazi wao "... "
Ndugu Mtafiti GENTAMYCINE sisi Walimu wa hapa.....eneo la Ilala hakuna jambo ambalo kwa sasa linatukera kama siyo kutuudhi kama la kila mwaka kuletewa Watoto / Wanafunzi ambao tunatumia muda mrefu sana kuwaelewesha lakini ukiwafundisha dakika moja ukikaa nusu saa uwaulize kile kile ulichowafundisha wanakuwa wameshasahau nadhani yawezekana Wazazi wa siku hizi wanakosa madini fulani muhimu ambayo yanawasababisha kuzaa Watoto wagumu wa kuelewa "..."
Ndugu Mtafiti GENTAMYCINE sisi Walimu wa hapa...eneo la Kinondoni nadhani kuna siku mtasikia tumepiga hawa Watoto hadi kuwavunja migongo yao kwani tunajitahidi kuwafundisha kwa kutumia mbinu zetu zote lakini bado kazi bure. Mtoto unamfundisha yeye anawaza tu kula ice cream na wengine unawafundisha huku shingo zao wakiwa wamezielekeza nje dirishani wakiweka oda ya mihogo na kachori kwa wauzaji. Nahisi hapa kuna tatizo la Kibaiolojia kutoka kwa Wazazi wao kwani hawana kabisa upeo Mungu akisaidie tu hiki Kizazi hakyanani ".
Nikaona nisiishie hapo ngoja nifanye balancing kutoka kwa Walimu wa zamani ambapo nilibahatika kuwapata pia wa kutoka maeneo hayo hayo matatu ya Temeke, Ilala na Kinondoni na katika hali ya kushangaza kabisa karibia wote walikuja na majibu ambayo yalikuwa yakifanana.
Niliwauliza tu hao Walimu "wastaafu" wa zamani kuwa wao enzi zao changamoto zao kubwa zilikuwa ni zipi na ni wapi walikuwa wakifurahia Kazi yao ya ufundishaji na majibu yao yakawa ni kama ninavyoyanukuu.."
Mwanangu Mtafiti GENTAMYCINE huko nyuma changamoto kubwa tuliyokuwa nayo ilikuwa tu ni mazingira ya Shule zetu ila tunachokishukuru ni kwamba Watoto / Wanafunzi wa Kizazi kile walikuwa ni WEREVU na wana elewa upesi na haraka sana hadi Mwalimu unasikia raha na burudani kufundisha kwani walikuwa wanaturahisishia Kazi zetu. Na nahisi hii yote ilitokana na uwezo mkubwa wa AKILI au UPEO waliokuwa nao Wazazi wao ambapo labda pia ilichangiwa na lishe yao na mazingira mazuri ya kinidhamu ambayo yaliwajenga wale Watoto kupenda Elimu na kujitahidi darasani "
Sikuona nikae nalo hili na badala yake nikasema nililete na niliwasilishe kwenu Wajuvi / Wana Taaluma tusaidiane kwani Elimu hii inatuhusu wote ili tupate ufumbuzi tutoke hapa tulipo. Je kwa hizo findings zangu chache hapo juu tatizo lipo wapi? Kuna ukweli gani juu ya hayo?
Karibuni.