Wazazi na wale wanaotegemea kuwa na watoto tuliangalie hili


GedsellianTz

GedsellianTz

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2016
Messages
1,288
Likes
1,673
Points
280
GedsellianTz

GedsellianTz

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2016
1,288 1,673 280
Mtoto wa kike azaliwapo tu anatakiwa kuandaliwa kuwa mama bora na mwanamke shupavu mwenye kujitambua,na kujua kuutunza usichana wake na haiba yake ya kike bila kusahau kuwa na shabaha ya kutofautisha kati ya mapenzi na upendo na kujua hila zote za wanaume walaghai na wenye hila za wanaume.

Mtoto wa kike asiyejua kufua nguo zake,kupika chakula ama kufanya kazi za nyumbani basi moja kwa moja jua unamuaanda mtoto wako kuwa demu na sio mwanamke bora sababu ukweli ulio wazi ,wanawake wavivu wametoka familia za kivivu na siku zote kwenye ndoa huwa hawadumu sababu hakuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke mvivu.

Baba anatakiwa ampende mke wake kwa maneno na vitendo ili binti aone na kusikia raha na na faraja ya mama yake ili naye aige tabia nzuri ya mama yake na kujua kuchagua wanaume bora kama baba yake,daima wazazi wa kiume huwa tunawapenda sana watoto zetu wa kike ,ni vyema ukumpa mtoto mapenzi bora akiwa angali mdogo ili ajue kutofautisha mapenzi ya wanaume walaghai.

Mama anayependa kula chips kwa wapemba na wale wanawake mabingwa wa junk food bila kusahau wale wanawake wanaopenda kushinda saloon za wakongo ndio hulea mabinti wanaoitwa mademu sababu mtoto anarithi tabia zote toka kwa mama yake,Mama bora humfunza binti yake kazi za nyumbani,usafi wa mwanamke,mapishi na ustaarabu wa mtoto wa kike.

Tunatakiwa kupanda mbegu bora kwa watoto wakiwa bado wadogo ili kutengeneza future yao nzuri ya baadaye ,kama wewe ndoa au malezi yamekushinda basi mwandalie mtoto wako ndoa nzuri na malezi mazuri ili aje kuishi maisha yake ya ndoa kwa amani na furaha.A good father is a source of inspiration and self-restraint. A good mother is the root of kindness and humbleness.
 

Forum statistics

Threads 1,236,819
Members 475,301
Posts 29,268,951