Wazazi/mzazi wa binti

umenikumbusha mbali mbu,kwa bahati sijui niseme nzuri au vipi sie tumezaliwa mabinti tu kwenye uzao wa mama kwakweli baba wakati huo alikuwa mkali kwelikweli na mama mfuatiliaji wa karibu sana na alitufanya tukawa marafiki wakubwa ile hata muda wa kutoka shule alikuwa anaujua na anakukadiria kwa mwendo wa kutoka shule mpaka nyumbani utafika saa ngapi alihakikisha marafiki tulionao anawajua mpaka nyumbani na wazazi wao.

jambo la pili nililoliona hawakutupa muda wa kukaa bila kitu cha kufanya ukitoka shule utajikuta kuna mwalimu mmeandaliwa wa kuwafundisha ,weekend ndo usiseme tuliandikishwa kwaya ya watoto kanisani ni kwenda kuimba huko na kujifunza neno la Mungu kwenda mbele jumapili ilikuwa ni siku ya wazazi na sie baada ya ibada mchana wake kunamtoko walituweka karibu sana............

tulipofikia age ya kuuanza ujana maana mie na anayenifuta tumeongozana sana hapo hakuna jambo ambalo hawakutueleza na kila weekend mama/Baba akisikia kuna sehemu mpya alitupeleka hata iwe mziki huwezi amini wakati huo mtu anakuja anawatongoza mpaka mama mzazi ..........lakini mama/baba baadaye kwa upole walikuwa anatueleza dunia ndo ilivo na tutakutana na mambo mengi na jinsi gani ya kuona hayo mambo ni ya kawaida na mtu asitudanganye na alikuwa wanatuambia wazi tunaenda na nyie kwenye sehemu za starehe asitokee mtu akawarubuni na kuwaonyesha ni mambo ya ajabu yanayoendelea kwenye hii dunia............madhara ya kufanya mapenzi kwenye umri mdogo na mengine mengi.............hata maisha ya kuridhika na yale unayopata iwe pesa au chochote kuamini kweny chako na sio cha mtu mwingine.

hata zile kazi kama za kubadilisha tairi kwenye gari tulikuwa tunaamshwa alfajiri na mzee anatueleza kuna tairi yake imetoboka huko anajiandaa kwenda kazini akitoka akute imebadilishwa tulifanya akitoka kazi yake ilikuwa kukaza nati peke yake

naweza sema mengi sana lakini kikubwa najivunia ule urafiki uliotengenezwa toka utoto kati yetu na wazazi una maana kubwa sana kwenye malezi ya binti zetu.
 
.
mtm, we acha tu aisee,....ashadii ushuhuda wake umeusoma? dahhh...yaani tangu jana nimezidi kum admire how strong
she is...



Mbu.... AshaD is a gem... and luckily we have like 100 lady gems in MMU, nikianza kuwataja hapa sintamaliza

we learn evryday and our mistakes are the best teachers
 
Mbu I am Soo tired... sijapitia the whole thread, but once i get time i will... Naamini kua mmeongea mengi ya Msingi katika hii thread... and i know sitakua disappointed.... Mie kama kawaida nataka niongee out of experience mie nikiwa kama huyo binti ambae umemuweka hapo...

Nikiwa 18 years i got pregnant.... I was so scared! Sikuweza confide kwa rafiki... ndugu ama mzazi yoyote tokana na ukweli kua i was so passive na nilikua sishirikish mtu mambo yangu... Sikua na makundi... nilikua mpole... nilikua an alone type of person....yaani kati ya wale mabinti role model (mie nilikua katika kundi la Mnamuona Asha?? Kwa nini hamuwezi kua kama Asha??) Imagine how fraustrated i was nilipopata mimba... My boyfriend alichanganyikiwa na kuamua kua tuoane... which i gladly accepted.. Wazazi nilipowambia nimepata mchumba... siku hio for the first time nilishuhudia babangu na mamangu wakigombana... LIVE! It was scary for My dad alikua anam-adore saaana mamangu.... Siku hio alikua anamlaum kua yeye kasababisha nitake kuolewa at such a young age... WHY?? I don't know, but sasa i have grown up naona Dad alikua na hasira alihitaji pakuitulia.... na mom was the closest.... Wakanikatalia i am too young to get married... I thot of abortion... but then i did not have the guts... nikiamini nikitoa mimba nitafariki...

I did what had to be done... told them i was pregnant..... One of the worst experience ever..... Imagine both my parents thot i was still a virgin.. it was a shocker to them... Hawaliamini kama kweli nilikua najua mwanaume yupo vipi.... mamangu the next day was on bed Sick....

Back to the Topic..... Mzazi anaumia.... mtoto anaumia, inahitaji busara ya juu saana upande wa wazazi kuweza pass thru such experiences... and thank GOD! They supported me thou kwa kinyongo.... I can not imagine ya kugundua kua ana HIV/AIDs... I have a daughter na the imagination is killing me!
I never saw this post... How traumatizing for the parents but most of all for you!
Mtoto wa 18 ni mdogo mno kwa experience kama hii, hata haelewi what is happening, let alone what to do...
I am happy you survived the experience and came out stronger!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom