Wazazi acheni kuwaficha watoto wenye ulemavu

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,549
Habari wanajamvi,

Wiki iliyopita nilihudhuria kusanyiko lililokuwa linahusu watu wenye ulemavu, nikatumia fursa hiyo kuchunguzachunguza mambo na kugundua idadi kubwa ya wenye ulemavu wana elimu ndogo huku wengine hawajui japo kusoma tu.

Nikadadisi sababu na kugundua wapo wazazi ambao hawakutaka kuwapeleka shule,sababu zingine ni shule kutokuwa rafiki kwa walemavu na unyanyapaa pia.

Nawashauri wazazi/walezi wenye watoto walemavu muwapeleke shule kwa manufaa yao na familia pia taifa kwa ujumla.
 
Kutowapeleka shule ni kuwanyima haki yao ya msingi. Nadhani jamii yote kwa pamoja inapaswa kupiga vita unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa aina yoyote ile
 
Ni kweli na sababu ingine ni tamaa ya utajiri ilitukumba kizazi hichi...Watu wana hadi vyumba vya siri kwenye mapalace yao kwa ajili ya kuwaficha watoto wao waliowafanya mataaira na kwa kukaa ndani muda mrefu wakapata hadi ulemavu wa viungo...
 
Haswa uko vijijini wanahisi wamelogwa na no laana na aibu kwa familia zao
 
Ni kweli na sababu ingine ni tamaa ya utajiri ilitukumba kizazi hichi...Watu wana hadi vyumba vya siri kwenye mapalace yao kwa ajili ya kuwaficha watoto wao waliowafanya mataaira na kwa kukaa ndani muda mrefu wakapata hadi ulemavu wa viungo...
Inasikitisha sana
 
Wengine wanawaficha sababu eti ndugu zao au wazazi wanaona aibu. Hii ni sababu ya kijinga kabisa.

Pia walemavu wanapaswa kupewa elimu kama watu wengine sababu ni haki yao.

Jamii pia ibadilike iache Imani potofu juu ya walemavu
 
Kuna wazazi mamburula.....
 
Back
Top Bottom