Wazawa na ufisadi Tanzania

Mkata Mtaa

Senior Member
Jun 10, 2016
136
141
Hii nchi ilikokuwa imefikia karibu kila mtu alishafanya ufisadi kwa njia moja au nyingine, kwa kupitia mikataba kutokujua, kwa kujua au kupitia wasaidizi wake, ningekuwa mimi kitu ambacho ningefanya ni kuunda tume ya maridhiamo kama aliyeunda Nelson Mandela baada ya kuwa raisi mweusi kwamba kila mwenye dhambi zake atubu tuanze upya.

Yeye alikuwa analaumu wazungu kwamba ni wabaguzi na wanawatesa wazawa, lakini na yeye alikuwa anaitwa gaidi kwa kichochea kuaribu mali na miundombinu ya nchi,kuna ufisadi umetokea mwingi nchi hii na watu wameumizwa sana na huo ufisadi, ila sio wote waliyoumizwa na ufisadi, na uwezi kuleta usawa kwa kumvuta chini tajiri ili awe sawa na maskini.

Hiyo kitu huwa kigumu, nchi zote duniani kuna ufasadi ila unapishana kiwango hasa nchi zilizokuwa za kijamaa, nchi kama Tz iliyokuwa ni ya kijamaa mpaka miaka 90 uwezi kupata matajiri wazawa ambao wanaweza kushindana na wachina na wahindi kwenye soko huria ikawezekana.

Hawa wachina na warusi matajiri wa sasa hivi wametengenezwa na serikali zao baada ya kuwapa mashirika ya serikali au kufanya ufisadi kwa nchi zao ili nao waweze kushindana na mataifa ya Ulaya na America, tulichokuwa tunatakiwa ni kuwaita wazawa wote waliyofanya ufisadi wa kishua na kuwakalisha chini na kuwaambia kwa sasa mnaanza kufanya biashara halali na kulipa kodi zote kuanzia sasa hivi, tuakiamua kurudi nyuma kufukua makaburi ya zamani tusitegemee kuwa na tajiri mzawa mweusi, nchi hii itakuwa ya wahindi na wachina nk.

Sitetei ufisadi ila mfumo uliyokuwepo zamani ya kuwaita wafanyabiashara wenye juhudi majina kama KUPE, KABAILA WANYONYAJI ndio uliturudisha nyuma wazawa wakaona bora kuajiriwa. Wakati tunashtuka wenzetu weupe walishapiga hatua kumi mbele, Hakuna mzawa mweusi amefanya biashara yenye mafanikio kizazi cha tatu tangu tupate uhuru.

Tuanze upya tulishakosea tangu mwanzo, tutunge sheria kali sasa ambazo watu wataogopa, mimi mwenyewe ni maskini naweza kuwa nimeuzwa na ufisadi lakini tulipofikia inabidi tusameheane tu.Serikali haifanyi biashara sasa tukiwaminya hawa wabongo nchihii matajiri si watabaki wahindi waarabu, wachina nk.

Mungu ibariki Tz
 
mmmmh sijaelewa
Soma hapa utamuelewa lengo lake:
"Hawa wachina na Warusi matajiri wa sasa hivi wametengenezwa na serikali zao baada ya kuwapa mashirika ya serikali au kufanya ufisadi kwa nchi zao ili nao waweze kushindana na mataifa ya Ulaya na America, Tulichokuwa tunatakiwa ni kuwaita wazawa wote waliyofanya ufisadi wa kishua na kuwakalisha chini na kuwaambia kwa sasa mnaanza kufanya biashara halali na kulipa kodi zote kuanzia sasa hivi, Tuakiamua kurudi nyuma kufukua makaburi ya zamani tusitegemee kuwa na tajiri mzawa mweusi, nchi hii itakuwa ya Wahindi na Wachina nk.
Sitetei ufisadi ila mfumo uliyokuwepo zamani ya kuwaita Wafanyabiashara wenye juhudi majina kama KUPE, KABAILA WANYONYAJI ndio uliturudisha nyuma wazawa wakaona bora kuajiriwa. Wakati tunashtuka wenzetu weupe walishapiga hatua kumi mbele, Hakuna mzawa mweusi amefanya biashara yenye mafanikio kizazi cha tatu tangu tupate uhuru."
 
asante mkuu kwa kunielewesha
 
Watu hawajelewa vizuri mada yangu, lakini tulipotoka ilikuwa ngumu wazawa kutoka, ata ikiangalia bendera ya ccm ilikuwa ni chembe na nyundo, maana yake nchi ilikuwa ya wakulima wa jembe la mkono na wafanyakazi au fundi seremara sasa hapo unaingiaje kwenye ushindani wa soko huria kwa watu weupi waliyofanya biashara zaidi ya miongo mitatu, maana Tz ata kama una wazo zuri benki hawakupi mkopo mpaka uwa na mali, je mkulima au mfanyakazi alikuwa na mali ya kuweka dhamana? hakuna, sasa wangetokaje uko? maana ata watu ngazi za mawaziri walikuwa wanafuga kuku kama 300 tu.
 
Back
Top Bottom