Wazanzibari wanaogawanyika waonywa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibari wanaogawanyika waonywa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 17, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][/h]Posted on July 17, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Uzini (CCM), Mohammed Raza nje ya ukumbi wa Baraza la wawakilishi

  WAJUMBE wa baraza la wawakilishi Zanzibar wameonya kuwa mgawanyiko wa wazanzibari katika suala la kutoa maoni juu ya katiba unahatarisha malengo ya wazanzibari katika muungano. Tahadhari hiyo imetolewa wakati wajumbe hao wakijadili hutuba ya bajeti ya wizara ya katiba na sheria iliowasilishwa na waziri wa wizara hiyo Abubakar Khamis Bakari katika baraza la wawakilishi.
  Walisema wakati huu wa ukusanyaji wa maoni ili kuandika katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ni muhimu kwa wazanzibari kutogawanyika na kwamba msimamo wa kudai maslahi ya taifa ni muhimu kuliko misimamo ya vyama au mtu binafsi.
  Waliojitokeza na kutoa tahadhari hiyo ni pamoja na Mwakilishi wa viti maalumu Asha Bakari Makame (CCM) mwakilishi wa jimbo la Uzini (CCM) Mohammed Raza, mwakilishi wa jimbo la mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu, mwakilishi wa jimbo la Kitope (CCM) Makame Mshimba Mbarouk na mwakilishi wa jimbo la Kiembe samaki (CCM) Mansoor Yussuf Himid.
  “Chuki baina yetu ilikuwepo kwa muda mrefu lakini mwenyeenzi mungu akatuleta baraka ya serikali ya umoja wa kitaifa hatupaswi kugawanyika tunapodai maslahi ya taifa” alisema Asha.
  Asha ambaye aliwahi kuwa waziri wa serikali ya Zanzibar alisema mitazamo tofauti juu ya muungano isiwe chanzo cha kuwarejesha nyuma wazanzibari walipotoka na kuomba wanasiasa kuwa ni mfano wa kuwaongoza wananchi katika kutoa maoni kwa kuvumiliana.
  “Huu ni wakati pekee na fursa muhimu sana katika historia ya nchi yetu hatupaswi kugawanyika kwa sababu zisizokuwa na msingi muelekeo uwe mmoja katika kudai maslahi ya Zanzibar ndani ya muungano na tusikubali kugawanywa” Jussa alitahadharisha.
  Jussa alisema umoja wa wazanzibari itakuwa ni kuwaunga mkono viongozi waliotangulia katika kuitetea Zanzibar ambao kwa wakati huo walipata misukosuko katika utetezi wao huo.
  Aliwataja viongozi hao kuwa ni muasisi mwenye wa muungano Mzee Abeid Karume, Mzee Aboud Jumbe, Maalim Seif, na hata Amani Abeid Karume ambao wote walipashikwa majina mbali mbali na kumtaka rais wa sasa Dk Ali Mohammed Shein kutoogopa kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya muungano.
  Akichangia katika hutuba hiyo Raza aliwataka viongozi kuanzia mawaziri wajumbe wa baraza hilo pamoja na wabunge kutoogopa kutetea maslahi ya Zanzibar na kwamba hapajakuwepo uwazi wa makubaliano katika mambo ya muungano ambayo orodha yake ilianzia mambo 11 na sasa ziadi ya 22.
  Raza alisema muungano utakaotoa nafasi ya Zanzibar kujiamulia mambo yake wenyewe ni fursa muhimu ya kuendelea kiuchumi ikiwmeo suala la kujiunga na jumuiya ya Umoja wa Kiislamu (OIC) na mashirika mengine ya kimataifa.
  Makame Mshimba alisema wananchi wa Zanzibe wana matumaoni makubwa na viongozi wao lakini baadhi ya viongozi kuanza kutumia majina na lugha mbaya dhidi ya wenzao wenye mitazamo tofauti ni hatari na inavunja moyo wananchi.
  “Labda tusaidiwe maneno haya yanayoibuka ya mpinzani, si mwenzetu, uamsho, tupumue, maana yake ni nini? Wakati kila mtu ana fursa na haki ya kutoa juu ya muungano?” Alihoji mwakilishi huyo.
  Mwakilishi wa kiembe samaki alisema wazi kwamba muungano wa hivi sasa unahitaji mabadiliko ili wazanzibari wapate fursa ya kumiliki uchumi wao ili kuweza kusaidia vijana wengi ambao hawana ajira hivi sasa.
  Alisema si vyema kwa baadhi ya viongozi wakiwemo wajumbe wa baraza la wawakilishi kuonesha chuki dharau na majigambo na kuanza kutoa majina yasiofahamika dhidi ya wale ambao msimamo wao ni wa kukataa muungano.
  “Huu sio wakati ule wa kutishana kama mtu ana mtazamo tofauti na wako hata wa kukataa muungano basi mwite na umpe hoja za kuunga mkono lakini sio kutumia mabavu na nguvu” alisisitiza.
  Mansoor alisema baadhi ya watu wamefika mbali na kuanza kutoa vitisho kuwa utawala wa kisultani utarudi wakati katiba hazitoi fursa hiyo na kwamba wazanzibari pia walipindua ili kujitawala na hivyo kamwe Zanzibar haitaweza kurejesha utawala wa kisultani.
  “Sisi tunaotaka mabadiliko eti tunambiwa tunataka kumrejesha sultani hii nchi ilipinduliwa na sultani gani anayetaka kurudi Zanzibar? Tusiwatishe mabibi zetu na wazee wetu waliopo huko mashamba kwa kusema maneno ya uongo hapa sultani hawezi tena kurudi” alisema waziri Mansoor.
  Mikakati yawekwa kupambana na madawa ya kulevya
  SERIKALI inakusudia kuweka mikakati imara ya kupambana na madawa ya kulevya visiwani Zanzibar kwa kuwashirikisha wadau mbali mbali ikiwa pamoja na kuwabaini wafanyabiashara wakubwa wa biashara hiyo.
  Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ofisi ya makamo wa kwanza wa rais, Fatma Abdulhabib Ferej wakati akijibu suali kutoka kwa Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu na kusema kwamba vita dhidi ya madawa ya kulevya sio kazi nyepesi.
  Jussa alitaka kujua mikakati ya serikali kupitia ofisi ya makamo wa kwanza wa raia katika kukabiliana na changamoto ya kurudi upya kwa uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya katika mitaa ya mji wa Zanzibar.
  Waziri huyo alisema kuwa tayari ofisi yake imekutana na wadau mbali mbali wanaohusika na udhibiti na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ili kupata maoni yao juu ya namna ya kulikabili tatizo hilo shughuli ambayo ilifuatiwa na mkutano uliozungumzia kwa kina changamoto zilizoibuliwa na wadau hao pamoja na mikakati mipya.
  Alisema ofisi ya makamo wa kwanza wa raia pia iliandaa kikosi kazi kilichojumuisha taasisi mbali mbali za dola zilizo katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na kuandaa njia maalumu (road map) ya utekelezaji wa sheria ya madawa ya kulevya Zanzibar.
  “Naomba mjumbe pamoja an wawakilishi wengine kwa jumla wa baraza hili kuwa na subra kwa kipindi ambacho mchakato wa ukamilishaji wa roadmap hiyo ukiendelea naamini kukamilika kwa mchakato huo kutakuwa ni dira kwa taifa letu katika kupambana na madawa ya kulevya nchini” alisema.
  Aidha waziri huyo alivitaka vyombo vya dola vilivyopewa jukumu kukamiliana na tatizo hilo kuongeza kasi ya utendaji kazi zao ili kunusuru vijana wa taifa ambao ni wahanga wakubwa katika janga la madawa ya kulevya.
  Fatma alisema kati ya mwaka 2010 hadi juni mwaka huu kesi 339 ziliripotiwa ambapo baadhi zimechukuliwa hatua na nyengine zinaendelea kuchukuliwa hatua katika ngazi za polisi na mahakama.
  Aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba sambamba na kudhibiti madawa ya kulevya pia ofisi yake inaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari pamoja na kusaidia vijana ambao wamekusudia kuachana na madawa ya kulevya ambao wapo katika nyumba za soba house Unguja na Pemba.
  “Kwa kutambua mchango wa taasisi zisizo za serikali katika suala zima la mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, ofisi yangu kupitia tume ya kuratibu na kudhibiti madawa ya kulevya ilitoa milioni 9.9 kwa nyumba tisa za soba houses Unguja na Pemba” alisema.
  Waziri huyo alisema ofisi yake itaendelea kuunga mkono juhudi hizo na kutoa wito wa taasisi nyengine mbali mbali za kijamii kwa jumla kuendelea kutoa msukumo na michango katika kuendeleza mbele harakati dhidi ya madawa ya kulevya visiwani Zanzibar.
   
 2. b

  beyanga Senior Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​uamshio
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Ukuta ujengwe katika Bahari ya Hindi utenge kabisa kabisa Zanzibar na Tanganyika tupate kulala usingizi. Tumechoka na kelele, mwe!
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  RAZA ni YANGA sasa ataishangiliaje YANGA wakijitenga? itabidi AOMBE VISA na tutakuwa Wagumu kama UINGEREZA

  Kutoa VISA kuingia Dar-es-salaam; Kwenda Jangwani
   
Loading...