Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,943
- 1,015
Zanzibar wanaserikali yao, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye Wizara yao ya Afya. Hili si jambo la Muungano. Fedha za wahisani juu ya miradi mbalimbali hata mafunzo tunagawana nao sawa. Cha ajabu wanapokuja kutibiwa Tanganyika wanataka kutibiwa katika viwango sawa na watanganyika. Hapana usawa. Waambiwe katika Bunge hili na kwingineko kuwa wazanzibari wanatakiwa kulipia gharama za matibabu katika Tanganyika zinazochangiwa na walipa kodi wa Tanganyika ama wawekezaji katika Tanganyika, wakitaka bwelele waende kwao Zanzibar.
Hili su kwao tu bali na kwa wageni wote. Nilishangaa siku niliyompeleka mkomoro pale Amana Hosp, Ilala. Pamoja na kuwaambia pale mapokezi na hata chumbani kwa Tabibu kuwa huyu ni mkomoro kwa uraia wake, bado walimchaji kwa viwango vya watanzania. Nilighafirika sana. Kwani ni upuuzi kama si ujinga ninyi kujifanya wakarimu sana hata katika huduma mnazowakamua watu wenu kodi. Jaribu kwenda Msumbiji, Malawi, Zambia na Rwanda kwa uchache wa majirani zetu wanaotuzunguka kama utaona mtanzania kulipia gharama sawa za wananchi wa nchi husika. Hakuna kitu hicho. Hata gharama za kuandaa na kutia dawa maiti ni kubwa sana; kwasababu si raia.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii itoe viwango vipya vya gharama za matubabu kwa wageni wote. Na viwango hivyo vitumike kuanzia kwenye Zahanati hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa hadhi ya hospitali husika. Kwa MNH japo wageni wanachajiwa katika viwango vya fast-track, bado haikubaliki kuwa mtanzania alipie gharama hizohizo sawa na mgeni. Viwango kwa wageni lazima viwe juu.