singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
JUMAPILI kesho, wananchi wa Zanzibar wanafanya marudio ya uchaguzi Mkuu baada ya ule wa awali uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana kufutwa kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza.
Maandalizi ya uchaguzi huo yanaelezwa kwamba yamekamilika na tayari karatasi za kupigia kura zimewasili, hivyo wananchi sasa wanasubiri kwa ari kubwa ili kushiriki katika uchaguzi huo mkuu utakaowawezesha kupata viongozi wao.
Lakini wakati hayo yakifanyika, kuna baadhi ya changamoto zimekuwa zikitokea katika maandalizi hayo ikiwemo matukio yanayohatarisha uvunjifu wa amani katika kisiwa hicho. Kati ya matukio hayo ni pamoja lile la kitu kinachosadikika kuwa bomu kulipuka usiku wa kuamkia Machi 5 mwaka huu katika eneo la Michenzani mjini Unguja, eneo linalojulikana kama maskani maarufu ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wakati viongozi na watu wa kada mbalimbali wakiendelea kulaani kitendo hicho ambacho kiliwatia hofu wakazi wa visiwa hivyo wakati wakijiandaa na uchaguzi, nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame iliopo Kijichi, nje kidogo ya mji wa Unguja nayo ilishambuliwa kwa kulipuliwa kwa bomu na kuharibika vibaya sehemu ya paa la juu pamoja na dari.
Huko Pemba nako nyumba tano, ofisi ya CCM na kituo cha afya navyo vilichomwa moto na watu wasiojulikana katika siku hizi za kuelekea uchaguzi wa marudio Zanzibar. Hakika vitendo hivyo na vingine vingi vinavyoendelea katika visiwa hivyo siyo vya kiungwana hata kidogo na si utamaduni wa Watanzania katika kufanya vurugu na machafuko ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kusababisha madhara makubwa.
Ni vyema ndugu zetu wa Zanzibar wasikubali kuendelea kutumika katika kufanya matukio ambayo yanaweza kusababisha uharibifu na hata vifo kwani uchaguzi ni jambo la kupita na maisha yanaendelea.
Wakati Jeshi la Polisi nchini likiendelea kuwatafuta watu wanaoshiriki katika vitendo hivyo ni vyema kila mmoja kwa nafasi yake kujitafakari iwapo Wazanzibari wako tayari kurudi katika machafuko ya miaka iliyopita na kusababisha maumivu makali kwa manufaa ya wanasiasa wachache.
Ni vyema kujiuliza ni faida gani walipata baada ya kushiriki katika vurugu za nyuma ambazo kwa hakika hazikuwa na tija yoyote kwa mustakabali wa watu wa visiwa vya Zanzibar, mintarafu suala zima la kuangalia athari za kijamii na hata kifamilia.
Ni vyema sasa kila mwananchi akajipanga kutumia haki yake ya msingi ya kikatiba kwa kushiriki kupiga kura katika uchaguzi huo wa marudio na kisha kusubiri mamlaka husika kumtangaza mshindi kisha kuendelea kumuunga mkono katika kuleta maendeleo ya visiwa hivyo.
Kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi uliopita ziliwekwa hadharani na kwa namna moja ama nyingine tayari maamuzi yamefanyika kwamba uchaguzi unapaswa kurudiwa. Na kimsingi hakuna njia nyingine mbadala ya kupata viongozi isipokuwa kwa kupiga kura.
Kadhalika, hakuna sababu ya kushiriki katika vurugu na kushiriki kulipua mabomu na vurugu nyingine kwani hazitasaidia kitu zaidi ya kufanya visiwa hivyo kutoendelea na mipango ya maendeleo.
Athari za vurugu ni pamoja na kuwaogofya watalii ambao kwa kiwango kikubwa wanachangia sana pato la Zanzibar. Ni vyema Wazanzibari, kila mmoja akawa mlinzi wa mwenzake bila kujali itikadi za kisiasa. Kwamba unapoona kuna wanaopanga kufanya matukio ya vurugu katika kipindi hiki muhimu, toa taarifa Polisi.