Wazanzibari kudai kiti chao Umoja wa Mataifa...

Wazanzibari kudai kiti chao Umoja wa Mataifa...

Rubawa

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2015
Posts
2,055
Reaction score
3,267
Wazanzibari kudai kiti chao Umoja wa Mataifa

Na Ahmed Rajab

MARA nyingi, kama si mara zote, historia huwa kama mkufu wa matukio ambayo kama yasingekuwa basi mkondo mzima wa historia ungegeuka na kuwa vingine.

Kwa mfano, lau Uingereza isingetoa uhuru kuipa Zanzibar Desemba 10, 1963 pasingefanywa mapinduzi Januari 12, 1964. Bila ya mapinduzi hayo pasingeundwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaojulikana leo kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na kama pangelikuwa na muungano wa nchi hizo basi lazima ungelikuwa wa aina nyingine. Ungelikuwa muungano wenye usawa kwa nchi zinazohusika na usiozinyima au usiozipunguzia nchi hizo mamlaka yao ya kujitawala.

Walioipindua serikali huru ya Zanzibar miaka 55 iliyopita wasingethubutu kuipindua serikali ya kikoloni iliyokuwa ikiendeshwa na Waingereza. Kwa vile wakoloni walikuwa na nguvu, wapinduzi walisubiri mpaka Waingereza walipokuwa hawana tena dhamana juu ya Zanzibar.

Ijapokuwa Waingereza hawakuwa na jeshi la maana visiwani pangezuka matata wakati wa utawala wao wangeweza kuyaita majeshi yao yaliyokuwa nchi jirani ya Kenya kuyazima matata hayo.

Kadhalika, wapinduzi wasingeweza kupindua Zanzibar wakoloni walipokuwa bado wako kwa sababu ingekuwa kichekesho kwa Waingereza kujipindua wenyewe kwani kuna ushahidi kwamba baadhi ya Waingereza waliokuwa Zanzibar wakati huo walisaidia kuyafanikisha hayo mapinduzi.

Ingekuwa hayakufanywa mapinduzi hayo, haielekei kwamba Muungano ungeundwa kwa namna ulivyoundwa bila ya kuwashirikisha wananchi wa nchi hizo mbili. Mapinduzi yalikipa madaraka chama cha Afro-Shirazi Party (ASP), chama ndugu na kile cha Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanganyika.

Hata kabla ya nchi zao kupata uhuru vyama hivyo vilikuwa na nia ya kuziunganisha nchi zao vitapohodhi madaraka.

Kuzaliwa kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar baada ya Mapinduzi kuliyafanya madola ya Magharibi, hasa Marekani, yazidi kuzihimiza serikali za TANU na ASP ziziunganishe nchi zao. Mabeberu hao wa Magharibi wakihofia kwamba Zanzibar mpya itaingia katika kambi ya nchi za Kikomunisti.

Nyaraka za siri za Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), ambazo sasa mtu anaweza kuziomba na akazisoma, zinaonesha jinsi serikali za Marekani na Uingereza zilivyoshirikiana kumhimiza Rais wa Tanganyika, Mwalimu Julius Nyerere, amburure Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kuziunganisha nchi zao.

Nyerere alitumia ujanja na vitisho alipokua akimbembeleza Karume akubali nchi zao ziungane kwa haraka . Hatimaye aliyapata matilaba yake na Tanganyika na Zanzibar zikaungana. Lakini kwa vile muungano huo ulifanywa kwa papara, bila ya matayarisho ya kina yanayostahiki kufanywa nchi zinapoungana, yakiwa pamoja na kuwashirikisha Watanganyika na Wazanzibari, muungano ulioibuka umekuwa muungano wenye dosari chungu mbovu. Kuna wenye kuhoji kwamba hauna hata uhalali wa kisheria au wa kimaadili.

Uzoefu wa miaka 55 ya Muungano unaonesha kwamba kati ya Tanganyika na Zanzibar ni Zanzibar iliyopunjika kwa kuungana na Tanganyika. Kwanza, imekipoteza kiti chake katika Umoja wa Mataifa. Hapakuwa na ulazima wa kuifanya Zanzibar ikipoteze kiti chake katika medani hiyo ya kimataifa. Tanzania ingeweza kuendelea kuwa na viti viwili, cha Tanganyika na cha Zanzibar kama Muungano wa Sovieti ulivyokuwa na viti vya jamhuri zilizokuwa katika Muungano huo.

Miaka 55 tangu uundwe Muungano wa Tanzania bado Wazanzibari wanaupinga muungano huo kama ulivyo sasa. Si kwamba wanataka kuuvunja lakini wanachodai ni kuwepo kwa muungano wenye muundo mwingine na unaozifanya Tanganyika na Zanzibar ziishi kidugu na kwa amani.

Kufikia lengo hilo wanadai kwanza pafanywe kura ya maoni itayowauliza Wazanzibari iwapo wanautaka Muungano kama ulivyo au la.

Juhudi za kudai kura ya maoni zinaongozwa na jopo la wanasheria mashuhuri Wakizanzibari ambao kwa muda usiopungua mwaka wamekuwa wakijiandaa kwa hilo. Pia wamekuwa wakifanya matayarisho ya kuliwasilisha dai lao Umoja wa Mataifa, jijini New York, la kutaka Zanzibar irejeshewe kiti chake katika Umoja huo.

Harakati zote hizi zinafanyika katika wakati ambapo Wazanzibari wanalipa kipaumbele suala hili kushinda ushindani wa vyama vyao vya siasa.

Amour Ali, mmoja wa viongozi wanaowawakilisha Wazanzibari juu ya kura ya maoni ameliambia Raia Mwema kwamba hawataraji ya kuwa Serikali ya Zanzibar itayaridhia kwa urahisi maombi yao.

“Tunafahamu uzito wa serikali zote mbili, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na ile ya Muungano wa Tanzania wa kuitisha kura ya maoni. Hata hivyo, tunatarajia kupata matokeo mazuri kutoka Umoja wa Mataifa ambako hoja hii itawasilishwa muda wowote kutoka sasa baada ya siku 60 kukamilika bila ya majibu yoyote kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,” alisema.

“Sisi tunaamini kuwa viongozi wa serikali zetu wameyapuuza na kutoyafanyia kazi maombi yetu hasa kutokana na ukweli kwamba, licha ya Wazanzibari walio wengi kutaka kuitishwe kura ya maoni, suala hilo kwa SMZ na kwa Serikali ya Muungano ni kama kaa la moto. Hata hivyo, sisi tutaendelea kulipigania kwani tunaamini kuwa suala hilo ni haki yetu kikatiba,” alisema Ali.

Alipoulizwa iwapo viongozi wa serikali ya Zanzibar wanajua iwapo wananchi wao wana mipango ya kuchukua hatua hizo, Amour Ali alijibu:

“Wanafahamu vizuri sana kwa sababu licha ya kuwa, ombi hili tulimfikishia Mwanasheria Mkuu wa SMZ Oktoba 25, 2018 ili yeye amtake Rais aiamuru Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuitisha kura ya maoni, nakala ya maombi yetu hayo pia tuliiwasilisha kwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Katibu wa Baraza la Wawakilishi na Jaji Mkuu wa Zanzibar na wote wameipokea.”

Miongoni mwa hatua za mwanzo walizofanya Wazanzibari hao ni kuzitaarifu nchi kadhaa kupitia balozi zao nchini Tanzania juu ya kuwepo kwa ombi la kura ya maoni.

Balozi hizo ni pamoja na zile za Marekani, Uingereza, Ireland, Ufaransa na Canada.

“Pia tumeitaarifu jumuiya za kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola na Umoja wa Ulaya juu ya uwepo wa ombi letu hilo,” aliongeza Ali.

Amour Ali amesema kwamba swali moja analoulizwa mara kwa mara kuhusu Zanzibar kurejeshewa kiti chake cha Umoja wa Mataifa ni la gharama; iwapo Zanzibar itakuwa na uwezo wa kifedha wa kukisimamia kiti hicho.

“Bila ya shaka yoyote. Zanzibar licha ya udogo wake, ni visiwa vyenye utajiri wa watu wenye mapenzi na nchi yao ambao tunaamini kwa mapenzi yao hayo wako tayari kwa gharama yoyote ile kuirejesha hadhi ya nchi yao iliyopotea kwa miaka 55 sasa. Hivyo, tunaamini kwamba, kutokana na utajiri wa watu wenye moyo huo tulionao ndani ya Zanzibar, Zanzibar ina uwezo wa kukigharimia kiti chake cha Umoja wa Mataifa.”

Amour Ali na wazalendo wenzake hawana matumaini mema kwamba SMZ itayaaunga mkono maombi yao.

“Hata hivyo, tunatarajia kupata matokeo mazuri kutoka Umoja wa Mataifa (UN) ambako hoja hii itawasilishwa” alisema kwa kujiamini.

“Hadi sasa tumefikia hatua nzuri na mambo yote tumeshayaweka tayari na katika utaratibu wake, siku 60 tulizompa Mwanasheria Mkuu kuiomba Serikali ya Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya suala la Muungano zimekamilika hivyo zinatoa fursa kwa hatua nyengine za kisheria kuchukuliwa.”

Amour Ali ameongeza kusema kwamba wanashajiishiwa na wananchi wenzao, ambao alisema wako pamoja nao wakisubiri majibu ya serikali huku wakifatilia kwa karibu kinachoendelea.

“Wazanzibari kama ilivyo kawaida yao, siku zote linapokuja suala linalohusu mustakbali wao na wa nchi yao huwa hawako nyuma katika kuliunga mkono. Hivyo, katika suala hili, ari na mwamko wa Wazanzibari ni mkubwa na matumaini yao yote yapo juu ya suala hili. Wanatusikiliza na kufatilia hatua kwa hatua na, mara kwa mara, tumekua tukikabiliana na maswali kutoka kwao yanayotaka kujua tulipofikia na tunakoendea.”

Baruapepe: aamahmedrajab@icloud.com; Twitter: @ahmedrajab









Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiti chenu alikichukua huyu bwana.Komaeni hadi wakirudishe
papua.jpg
 
Kwa hiyo hizo Nyaraka za C.I.A ndugu mwandishi unazo?!
 
Siku mwingereza akisema mjitawale hata hicho kiti mtapewa tofauti na hapo kubalini tu kuburuzwa
 
Mkienda na mkoa wa Mtwara nao wanakwenda. Jihadhari sana maandishi hayo ni treason tayari. Yaani tutakushtaki kwa uhaini.
 
Tatizo la wazanzibari halitatatuliwa na UN Bali wazanzibari wenyewe.

Zanzibar ilipaswa iwe nchi Tajiri sana Afrika lakini siasa za kisisiem zimerudisha nyuma nchi hiyo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zanzibar ilipaswa iwe nchi Tajiri sana Afrika lakini siasa za kisisiem zimerudisha nyuma nchi hiyo

Naunga mkono hoja ; Visiwa vya Unguja na Pemba kama vingekuwa na AUTONOMY vingekuwa na maendeleo makubwa sana kama ilivyo Mauritius; kukosekana kwa uhuru wa kujiamulia mambo yake yenyewe na sera za kibinafsi za ccm ndio chanzo cha kudumaza maendeleo ya visiwa hivyo!
 
Kimsingi Zanzibar hawataki huu muungano kwao ni kero.
Waliwahi kutaka kushiriki michuano ya kimataifa wao kama Zanzibar na sio Tanzania hapa nazungumzia mpira.
Wazanzibar waliwahi kufungua kesi mahakamani wakiwa kundi la watu 40,000 sijui kesi yao iliishia wapi.
Kwenye michuano ya secafa wanashiriki wao kama Zanzibar sio Tanzania.
Zanzibar wana ligi yao ya mpira badaya la ligi kuu ya Tanzania. Hii sio nzuri nchi inapaswa isimame kama nchi... UK wapo scotland, england, wales ligue zao zinajitegema hii sio nzuri na nadhani ipo sababu ya kufanya hivi.
Mataifa yakiungana huwa taifa moja kama ilivyo marekani "United States of America" wao ni mataifa 50 yameungana sasa embu fikiri kila state ikianza kujitegemea utakua ni muungano tena?
Kimsingi Zanzibar hawautaki huu muungano na hujiita koloni la Tanganyika.
Kwangu mimi huu ni utumwa bora Zanzibar wapate nchi yao wajitawale wenyewe kuliko kuishi wamefungwa mdomo namna hii halafu tunasema umoja ni nguvu sasa umoja gani wakati upande mwingine unadai umetawaliwa?
Kwa namna hii Zanzibar wamechoka...
 
Kimsingi Zanzibar hawataki huu muungano kwao ni kero.
Waliwahi kutaka kushiriki michuano ya kimataifa wao kama Zanzibar na sio Tanzania hapa nazungumzia mpira.
Wazanzibar waliwahi kufungua kesi mahakamani wakiwa kundi la watu 40,000 sijui kesi yao iliishia wapi.
Kwenye michuano ya secafa wanashiriki wao kama Zanzibar sio Tanzania.
Zanzibar wana ligi yao ya mpira badaya la ligi kuu ya Tanzania. Hii sio nzuri nchi inapaswa isimame kama nchi... UK wapo scotland, england, wales ligue zao zinajitegema hii sio nzuri na nadhani ipo sababu ya kufanya hivi.
Mataifa yakiungana huwa taifa moja kama ilivyo marekani "United States of America" wao ni mataifa 50 yameungana sasa embu fikiri kila state ikianza kujitegemea utakua ni muungano tena?
Kimsingi Zanzibar hawautaki huu muungano na hujiita koloni la Tanganyika.
Kwangu mimi huu ni utumwa bora Zanzibar wapate nchi yao wajitawale wenyewe kuliko kuishi wamefungwa mdomo namna hii halafu tunasema umoja ni nguvu sasa umoja gani wakati upande mwingine unadai umetawaliwa?
Kwa namna hii Zanzibar wamechoka...
Nchi zote zenye watu wa dini, rangi na makabila tofauti kama ilivyo Tanzania ili ziweze kuwa na umoja ,undugu,mshikamano, uzalendo na utaifa ni lazima pawe na Demokrasia ya kweli na Mahakama ziwe na nguvu kubwa kuweza kutoa maamuzi ya haki kwa kila mtu bila kujala cheo wala itikadi za vyama.

Chunguza mwenyewe kama hayo yamekaa sawasawa.
Maalima akishinda anaapishwa ili naye na kundi lake wajijue wapo huru kisiasa ?
Zanzibar wakimteua mgombea wao wa Urais kupitia CCM anapitishwa Dodoma?

Hata nchi kubwa zilizoungana bado zina mamlaka yao ya ndani kama ilivyo Zanzibar.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nilidhani mmekuja na mkakati kabambe wa kupigania uhuru wenu kumbe porojo tu, ndugu hakuna uhuru unaokuja kirahisi, lazima damu imwagike, kama sivyo mtaendelea kupiga story za uhuru kwenye vijiwe vya kahawa tu.
 
mimi nilidhani mmekuja na mkakati kabambe wa kupigania uhuru wenu kumbe porojo tu, ndugu hakuna uhuru unaokuja kirahisi, lazima damu imwagike, kama sivyo mtaendelea kupiga story za uhuru kwenye vijiwe vya kahawa tu.

Magufuli hajaribiwi!

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkienda na mkoa wa Mtwara nao wanakwenda. Jihadhari sana maandishi hayo ni treason tayari. Yaani tutakushtaki kwa uhaini.

Wakidai siye tufanyeje???? Tujinyonge????

kwa hiyo????

Kiti chenu alikichukua huyu bwana.Komaeni hadi wakirudisheView attachment 991508


Wakuu hizo kejali zinamwisho wake. Leo wanadai kwa kufuata taratibu za kisheria, siku itakapofika wakachoka kudai kwa hizo taratibu wakaanza kudai kwa kutumia njia nyengine watakazozijua wao ndipo tutapoanza kutafutana.

Ukisikia huko Kashmir, Somali, Congo, yalianza hivihivi kidogokidogo. Dar-es-salaam tutakuja kuiona chungu hii
 
Back
Top Bottom